Uchaguzi 2020 Katika majimbo ya Uchaguzi 264, Lissu kwa mwezi mzima wa kampeni katembelea majimbo 17 bado majimbo 257 ambayo CCM tupo

Uchaguzi 2020 Katika majimbo ya Uchaguzi 264, Lissu kwa mwezi mzima wa kampeni katembelea majimbo 17 bado majimbo 257 ambayo CCM tupo

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Wale mnaopiga kelele kuwa Lissu kamaliza kazi mnaota Lissu mwezi mzima hadi sasa kahutubia kampeni majimbo Tena mijini 17 wakati jumla ya majimbo ya Uchaguzi Tanzania yako 264 Kuna majimbo 257 hajakanyaga sisi CCM tuko kote huko tunadunda Kama kawa tukisubiri kwa nderemo na vifijo tarehe 28 Oktoba tumuonyeshe cCha mtema kuni Lissu

Mwezi mzima majimbo 17!!! Tumebakiza mwezi mmoja wa kampeni hata aende kwa spidi ipi aweza ishia majimbo 35 tu jumla awamu hii ya pili majimbo 222 hataweza kuyafikia kabisa hadi Uchaguzi mkuu ufike

Ushindi wa CCM hauepukiki hiyo ndio siri yetu ya kwanza sisi tuna cover kote hatuachi mahali kuanzia mjini Hadi vijijini vichakani utakuta bendera ya CCM hewani ikipepea na picha za chagua Magufuli

Tambo zote za Chadema mitandaoni humu ni za hayo majimbo 17 aliyopita Lisu Tena kwenye vimiji
 
Hapo umemzungumzia Lissu as individual halafu unamlinganisha na CCM kama chama kwa ujumla kitu ambacho siyo sahihi ingefaa umlinganishe Lissu na mgombea mwenzie Magufuli ili ufanye analysis vizuri mpk sasa wamecover kiasi gani toka wameanza. Maana siyo kwamba Chadema nao wamerelax kwa maana ya chama nao wapo site
 
Kilimanjaro hajafika na wala asipofika atazoa kura nyingi kuliko chama chochote . yaani sisi tumesh MUELEWA tokea day one
Nipo Kilimanjaro, Magufuli anakubalika huku, nitahifadhi hii comment yangu nitarudi Tena, wachaga Sasa sisi tunamtaka Magu na atashinda lissu. Nadhani Katika sehemu ambayo upinzani wataumia Sana Ni mkoa wa Kilimanjaro, hawatapa Jimbo hata moja. Nani anataka ndugu zao kuenguliwa Katika position kubwa kubwa na kutengwa na raisi, tunajuta yaani
 
CCM imetembelea huko Toka 2016 ilipopiga marufuku SIASA, siyo leo na ndiyo maana imechokwa na uongo wake unaomzidi shetani.

Eti maendeleo hayana chama alafu hapo hapo jitu linasema msiponipa ubunge siwaletei barabara, Mungu wangu , bora hata wakoloni akina Carl Peters waliowapiga mababu zetu viboko walikuwa na roho ya utu
 
Back
Top Bottom