Huoni kwamba ndo sababu ya sisi kuchelewa,
ushawahi kufikiri mazingira ambayo viongozi wa kitanzania hupatikana?
Sababu za sisi kuchelewa ni mtambuka.
Zipo za ndani na nje.
Za ndani ukiachana na ubovu wa viongozi wetu pia raia nao ndio wabovu zaidi.
Raia ni wabovu zaidi kwakua hawaoneshi kuchukizwa na matendo maovu ya viongozi wao.
Inatokea kiongozi anafanya jambo kinyume na maslahi ya nchi raia wanazungumza tu chini chini jambo linakwisha bila hatua yeyote kuchukuliwa kwa mhusika.
Sababu za nje , ni taasisi za kifedha na nchi za magharibi.
Taasisi za kifedha IMF na World Bank hizi ni nyenzo za nchi za magharibi zinazotumika kuhakikisha kwamba umaskini hauondoki kamwe katika nchi ,za kiafrika kwa kuweka policies mbali mbali, kushusha thamani za fedha zetu na mikopo ambayo masharti yake yanatufanya tuwe watumwa.
Mikopo ya nje yote inakuja kwa fedha za kigeni, na ili uweze kupata fedha za kigeni ni lazima upeleke bidhaa nje ya nchi , nchi ambazo ndio hizo wanazo control hizo taasisi.
Huko unakopeleka hizo export utauza kwa bei wanazotaka wao na si kwa faida halisi unayostahili.
Mikopo mingi ina masharti magumu ambayo yanazidi kudidimiza nchi husika mifano yake ni kama kenya, Zambia na kwingine ambako.tumesikia hali mbaya za madeni.
Nchi za magharibi nazo zinahakikisha hakuna kiongozi mwenye maono Afrika ana bakia hai.
Wameua Ghadafi, wameua Patrice Lumumba, yote hii ni kuhakikisha kuwa kamwe Afrika haipati maendeleo.
Kuweka pupet leaders , viongozi ambao wapo tayari kusaliti wananchi wao na kutekeleza maslahi ya nchi za magharibi kwa kupewa sehemu ya faida kutokana na uwekezaji na ukwapuaji wa rasilimali. Mifano ni mingi.
Sasa ili tuendelee inapaswa Raia kwanza wabadili mitazamo yao, kwa kutokubali kuburuzwa na viongozi goi goi.
Kuchagua viongozi wazalendo , kulima mazao ya chakula na sio mazao ya biashara pekee.
Kuwa na viwanda vingi, kupunguza matumizi ya fedha za kigeni, kuachana na mfumo wa dola, kutumia vyanzo vya ndani kwenye miradi ya kimkakati.
Kutoa elimu bora yenye kumuandaa mhitimu kupambana na changamoto halisi za kimaisha.
Kuwa na mifumo imara yenye kulinda maslahi ya Taifa.
Kufuta kabisa ufisadi , wizi na rushwa.
Ili tupate maendeleo inatupasa kufanya hayo kwa uchache tu ingawa safari ya maendeleo ni ndefu na mambo ya kufanya ni mengi.
Mungu ni mwema yote yana mwisho.