Katika makuzi yangu nilikua nikiaminishwa kuwa viongozi wa nchi huchaguliwa na Mungu

Katika makuzi yangu nlikua nkiaminishwa kua viongozi wa nchi huchaguliwa na Mungu,

Pindi nasoma advance bahati nzuri uchaguzi wa rais, wabunge pamoja na madiwani nlikua kidato cha sita pale shinyanga high school maarufu kama SHY BUSH , nlishiriki kupiga kura lakin majibu yaliyobandikwa ktk kituo nlichopigia kura, hayakushabihiana hata kidogo na matokeo nliyoyayaaikia redioni (jecha style)

Haitoshi; hata siku izi mambo yamegoma kabisa kubadilika, bado kura zinazopigwa haziendani na zile zinazotangazwa, wachungaji hutambua hilo lakin ajabu hawajawahi kuwafukuza sehem za ibada hasa kipindi ha harambee,

Samia
Mwiguru
Kakamba
Nape
Lowasaa nk. Hawa ote ni saham ya mfano kwa MUSSAna wana wa Israel?
Hapana, kuna viongozi wengine huchaguliwa na shetani.mfano huyu wasasa amechaguliwa na shetani kabisa. Mungu hawezi tupa kiongozi bomu kiasi hiki.
 
Wachungaji ndo walinaminisha ivo, walisema "mamlaka zote duniani huwekwa na MUNGU" tena wakasisitiza ni lazima tuheshim mamlaka.

Apo unapaonaje, ukikutana na mzee wa kanisa akakpa hizi story utamwambiaje?
Huwa unaamini hizo dini na hao wazee wa kanisa? Mbona umejiingiza kwenye ujinga wa kujitakia?
 
Kabla ya kwenda mbali, unaamini Kuna Mungu, yukoje na anafananaje?
Binafsi naamin ktk uwepo wa MUNGU, lakin kwa imani yangu ukiristo na uislam ni upotoshaji,

Hii inakuja baada ya kuzingatia uajenti wa ukoloni issue za hizi dini zinashika namba mbili baada ya swala la upelelezi kua namb 1, apa kwa kiwango kikubwa tumepigwa sana
 
Enzi hizo walikuwa wakichagukiwa na mungu lakini Sasa tangu SHETANI aingie nchini kwetu.....woooote ni wake
 
Mungu anasingiziwa tu ili kuhararisha matendo yao (mabaya au mazuri).

Mungu hawezi chagua kiongozi ambaye anakwenda kutesa watu wake.
 
Hakika nlipigwa na kitu kizito
Mamlaka zote zatoka kwa Mungu.

Hata Pilato na Herode walitoka kwa Mungu. Yesu alimwmabia Pilato pale Praitorio, usiku ule, isingelikuwa baba yangu, usingalikuwa kiongozi.

Hata mfalme Sauli, alichaguliwa na Mungu.

Sio kila anayetoka kwa Mungu basi hutenda yale Mungu anataka, wengine hufanya yao.
Hata Adamu aliumbwa na MUNGU .
 
Hua anachagua kwa kubet au Mungu huchukulia poa mahitaji ya watu wake, imagine fisadi anaejulikana vema anashika nafasi ya uongozi kwa zaidi ya mihula miwili au mitatu.

Hii ni kwakua kuna uhaba wa watu wema wenye uchungu na vizazi vingine?
 
Ni kweli mkuu,

Mungu ndio huchagua viongozi.

Hata akiwa mbaya ila kuna kusudi la Mungu ambalo anataka litimie.
 
Huoni kwamba ndo sababu ya sisi kuchelewa,

ushawahi kufikiri mazingira ambayo viongozi wa kitanzania hupatikana?
 
Sababu za sisi kuchelewa ni mtambuka.

Zipo za ndani na nje.

Za ndani ukiachana na ubovu wa viongozi wetu pia raia nao ndio wabovu zaidi.

Raia ni wabovu zaidi kwakua hawaoneshi kuchukizwa na matendo maovu ya viongozi wao.

Inatokea kiongozi anafanya jambo kinyume na maslahi ya nchi raia wanazungumza tu chini chini jambo linakwisha bila hatua yeyote kuchukuliwa kwa mhusika.

Sababu za nje , ni taasisi za kifedha na nchi za magharibi.

Taasisi za kifedha IMF na World Bank hizi ni nyenzo za nchi za magharibi zinazotumika kuhakikisha kwamba umaskini hauondoki kamwe katika nchi ,za kiafrika kwa kuweka policies mbali mbali, kushusha thamani za fedha zetu na mikopo ambayo masharti yake yanatufanya tuwe watumwa.

Mikopo ya nje yote inakuja kwa fedha za kigeni, na ili uweze kupata fedha za kigeni ni lazima upeleke bidhaa nje ya nchi , nchi ambazo ndio hizo wanazo control hizo taasisi.

Huko unakopeleka hizo export utauza kwa bei wanazotaka wao na si kwa faida halisi unayostahili.

Mikopo mingi ina masharti magumu ambayo yanazidi kudidimiza nchi husika mifano yake ni kama kenya, Zambia na kwingine ambako.tumesikia hali mbaya za madeni.

Nchi za magharibi nazo zinahakikisha hakuna kiongozi mwenye maono Afrika ana bakia hai.

Wameua Ghadafi, wameua Patrice Lumumba, yote hii ni kuhakikisha kuwa kamwe Afrika haipati maendeleo.

Kuweka pupet leaders , viongozi ambao wapo tayari kusaliti wananchi wao na kutekeleza maslahi ya nchi za magharibi kwa kupewa sehemu ya faida kutokana na uwekezaji na ukwapuaji wa rasilimali. Mifano ni mingi.

Sasa ili tuendelee inapaswa Raia kwanza wabadili mitazamo yao, kwa kutokubali kuburuzwa na viongozi goi goi.

Kuchagua viongozi wazalendo , kulima mazao ya chakula na sio mazao ya biashara pekee.

Kuwa na viwanda vingi, kupunguza matumizi ya fedha za kigeni, kuachana na mfumo wa dola, kutumia vyanzo vya ndani kwenye miradi ya kimkakati.

Kutoa elimu bora yenye kumuandaa mhitimu kupambana na changamoto halisi za kimaisha.

Kuwa na mifumo imara yenye kulinda maslahi ya Taifa.

Kufuta kabisa ufisadi , wizi na rushwa.

Ili tupate maendeleo inatupasa kufanya hayo kwa uchache tu ingawa safari ya maendeleo ni ndefu na mambo ya kufanya ni mengi.

Mungu ni mwema yote yana mwisho.
 
Mungu huwa anatumika kama kichaka Cha kufichia maovu ya watawala. Ukianza kuwakosoa watawala hao waovu, utasikia: "Heshimuni mamlaka, maana mamlaka zote hutoka Kwa Mungu. ". (Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Warumi 13:1)

Wanapenda kutumia kifungu hicho Cha biblia ili kujilinda dhidi ya mashambulizi ya mahasimu wao..... Wakati huo huo watawala hao ni wanachama wa vyama Vya kutenda maovu.

Binafsi, siamini kama Mungu anahusika kuwasimika watawala wabadhirifu ilihali tunajua njia haramu wanazotumia kujipatia madaraka; kisha Mungu anakuja kutumika kama Kinga yao.
 
Huoni kwamba ndo sababu ya sisi kuchelewa,

ushawahi kufikiri mazingira ambayo viongozi wa kitanzania hupatikana?
Sababu za sisi kuchelewa ni mtambuka.

Zipo za ndani na nje.

Za ndani ukiachana na ubovu wa viongozi wetu pia raia nao ndio wabovu zaidi.

Raia ni wabovu zaidi kwakua hawaoneshi kuchukizwa na matendo maovu ya viongozi wao.

Inatokea kiongozi anafanya jambo kinyume na maslahi ya nchi raia wanazungumza tu chini chini jambo linakwisha bila hatua yeyote kuchukuliwa kwa mhusika.

Sababu za nje , ni taasisi za kifedha na nchi za magharibi.

Taasisi za kifedha IMF na World Bank hizi ni nyenzo za nchi za magharibi zinazotumika kuhakikisha kwamba umaskini hauondoki kamwe katika nchi ,za kiafrika kwa kuweka policies mbali mbali, kushusha thamani za fedha zetu na mikopo ambayo masharti yake yanatufanya tuwe watumwa.

Mikopo ya nje yote inakuja kwa fedha za kigeni, na ili uweze kupata fedha za kigeni ni lazima upeleke bidhaa nje ya nchi , nchi ambazo ndio hizo wanazo control hizo taasisi.

Huko unakopeleka hizo export utauza kwa bei wanazotaka wao na si kwa faida halisi unayostahili.

Mikopo mingi ina masharti magumu ambayo yanazidi kudidimiza nchi husika mifano yake ni kama kenya, Zambia na kwingine ambako.tumesikia hali mbaya za madeni.

Nchi za magharibi nazo zinahakikisha hakuna kiongozi mwenye maono Afrika ana bakia hai.

Wameua Ghadafi, wameua Patrice Lumumba, yote hii ni kuhakikisha kuwa kamwe Afrika haipati maendeleo.

Kuweka pupet leaders , viongozi ambao wapo tayari kusaliti wananchi wao na kutekeleza maslahi ya nchi za magharibi kwa kupewa sehemu ya faida kutokana na uwekezaji na ukwapuaji wa rasilimali. Mifano ni mingi.

Sasa ili tuendelee inapaswa Raia kwanza wabadili mitazamo yao, kwa kutokubali kuburuzwa na viongozi goi goi.

Kuchagua viongozi wazalendo , kulima mazao ya chakula na sio mazao ya biashara pekee.

Kuwa na viwanda vingi, kupunguza matumizi ya fedha za kigeni, kuachana na mfumo wa dola, kutumia vyanzo vya ndani kwenye miradi ya kimkakati.

Kutoa elimu bora yenye kumuandaa mhitimu kupambana na changamoto halisi za kimaisha.

Kuwa na mifumo imara yenye kulinda maslahi ya Taifa.

Kufuta kabisa ufisadi , wizi na rushwa.

Ili tupate maendeleo inatupasa kufanya hayo kwa uchache tu ingawa safari ya maendeleo ni ndefu na mambo ya kufanya ni mengi.

Mungu ni mwema yote yana mwisho.
 
Umeeleza mambo mengi na muhim, lakin pia kupitia maelezo yako nmeona MUNGU haweki viongozi Africa bali viongozi wetu huletwa na watu, ndio maana hata kura zetu hazina maamzi
 
Back
Top Bottom