Katika mapambano ya kisiasa, uwepo wa wanaharakati au "radicals" ni msaada mkubwa kwa "moderates"

Katika mapambano ya kisiasa, uwepo wa wanaharakati au "radicals" ni msaada mkubwa kwa "moderates"

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Ukiona mtu anadai anataka mabadiliko halafu wakati huo huo anawapinga "radicals" au wanaharakati, huyo mtu ni ama hajui umuhimu wao au ni kibaraka wa upande wa pili.

Uwepo wa radicals au wanaharakati unawasaidia moderates hata katika meza ya maridhiano au majadiliano maana upande wa pili utaona ni bora kuwasililiza moderates na kuwapa wanachotaka kuliko tishio la wanaharakati kupata nguvu zaidi na kuwaondoa moderates.

South Africa ni mfano mmoja wapo wa umuhimu wa wanaharakati au radicals. Uwepo wa radicals kama kina Steve Biko na Chris Hani kulimsaidia sana mtu kama Mangosuthu Buthelezi maana makaburu waliona ni bora wampe anachokitaka kuliko kuja kudili na watu ambao hadi walihubiri sera za kutaka makaburu wafukuzwe kabisa South Africa. Baadae ANC ya kina Mandela iliporudi katika njia za maridhiano, ilipata nguvu kutokana na matishio ya radicals au radical approaches.

Marekani ni mfano mwingine. Uwepo wa Malcolm X na Nation of Islam pamoja na movements zingine za wale walioonekana ni radicals kama kina Fred Hampton na Black Panther Party ulikuwa msaada mkubwa kwa movement ya watu kama Martin Luther King, Jr walioonekana ni "moderates". Mwisho wa siku mfumo wa Marekani ukakubali sera na hoja za kina MLK lakini hilo lisingewezekana bila msukumo na matishio ya radicals.

CHADEMA inahitaji sana uwepo wa wanaharakati, ama wapo ndani au pembeni ya chama, ila haihitaji uwepo wa viongozi ambao wanawazunguka viongozi wenzao na maamuzi ya chama ambao matendo yao yanadhoofisha misimamo ya chama.

CHADEMA wanahitaji kwenda kwenye meza ya maridhiano wakiwa na turufu ya matishio ya radicals au wanaharakati kama sauti mbadala. Ukiwaondoa au kuwasimanga hao unapoteza "bargaining chip" muhimu sana katika meza ya majadiliano.

NB. Nadhani kuna umuhimu mkubwa wa CHADEMA kutengeneza strategically a radical wing ndani ya mfumo wao wa kudai haki na kuwaacha waende kwenye offence ili kuwajengea moderates ndani ya chama nguvu katika meza ya majadiliano siku hiyo itakapofika.
 
Kuna quote moja nimesahau ngoja nitafute inahusu uyu ambae anajifanya yupo nutro uyu anakuwa yupo opposite side.

Kila mtanzania mwenye akili timamu kwa sasa anadai mabadiliko,haki na uwajibikaji.

Nitashangaa sana kumuona mtu anatia maanani kwa yale matapishi ya lema kwenye ile conference ingawa nimeangalia kwa clip fupi fupi lakini kiujumla mwamba ni pandikizi la viua vijeshi
 
Back
Top Bottom