Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Huko kwenye nchi za ulimwengu wa kwanza kiongozi au mwanasiasa kudanganya au kuandika taarifa za kubumba katika CV yako hasa suala la elimu ikugundilika ni suala linaloweza kupelekea hata kupoteza nafasi yako ya uongozi. Hili ni suala ambalo utakuta linajadiliwa hadi katika vyombo vikubwa vya habari kama CNN, Fox News n.k
Mwaka juzi huko Marekani mbunge mmoja kijana aitwaye George Santos wa bunge la wawakilishi la kitaifa alilazimika kujiuzulu baada kugundulika aliweka taarifa za kubumba(ikiwemo kudanganya kuhusu elimu yake) katika CV yake aliyoitumia kupitishwa na chama chake cha Republican kugombea na kupata ubunge. Kwetu pia haipaswi kuwa jambo la kawaida kuachiwa lipite tu.