Katika msimu huu wa uchaguzi mkuu, mitandao ya kijamii itafanya kazi kubwa kuliko traditional media

Katika msimu huu wa uchaguzi mkuu, mitandao ya kijamii itafanya kazi kubwa kuliko traditional media

sopinta

Member
Joined
May 28, 2020
Posts
46
Reaction score
93
Yani lolote litakalofanyika kuzuia hivi vyombo vya habari vya kienyeji kama vile magazeti, TV, radio katika kipind hiki cha uchaguzi ni sawasawa na bure kwani kutokana na mageuzi ya sayansi na tekinolojia zinajulikana kama traditional media haitasaidia.

Social media zina nguvu kuliko hizi traditional media, mambo mengi sana kwa sasa yanatolewa na social media kwa sababu zipo haraka sana, zinamfikia mtu popote alipo bila kujali muda, zinashirikisha mtu yaani mtu akitumiwa naye anaweza akasambaza, zinatoa uhalisia wa jambo bila kuhariri.

Matukio mengi kwa sasa duniani yanatolewa na social media kwa mfano kitendo cha George Floyd kubanwa mpaka kufa ushaidi halisi ulitolewa na social media yaani simu zilizokuwa zinarekodi wakati wa tukio zikarusha tu, mlipuko wa Lebanon -Beirut kabla ya magazeti, radio au tv kutoa tayari social meda ikarusha tena wakati wa mlipuko mdogo tu kuanza.

Yapo mengi, matukio mengi yanaletwa kwa jamii kupitia social media.

Sasa nitoe angalizo tu kwa hizi mamlaka za mawasiliano TCRA, Habari Maelezo, na vyombo vingine kuwa ni ngumu sana kuzuia mambo ya habari, dunia ya leo ni kijiji na ipo kiganjani siku hizi hata mtoto wa miaka mitano anajua kutumia social media, utakaposema nazuia habari ni sawa na kuzuia mafuriko ya maji kwa mkono.

Tuache jamii ipate habari kama dunia inavyotaka.
 
Wametumia akili za kuvukia barabara watu wataenda kwa uwingi kwenye mikutano ambako watalishwa vyakutosha, kuliko kwenye hizo media ambapo mwanahabari atakujuza habari anayotaka yeye tena kwa sekunde kadhaa 'edited news'. Sometimes you may get biased news
 
Vyombo vya habari traditonal vya Tanzania haviwezi kutoa taarifa kwa mizani sawa mzee jiwe kaishavibana.
 
Na ndio mwisho wa Jiwe ukiona mtu kabana Kila kitu ujue mwisho unakaribia

Kuna uwezekano mkubwa wa kuanguka kwake sisi tutajaa kwenye mikutano na tutasikia mengi kutoka kwenye mikutano.
 
Back
Top Bottom