Katika nchi 35 zilizokataa kupiga kura suala la Urusi kuvamia Ukraine 50% ni za Afrika, ikiwemo Tanzania

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Niliweka thread humu JF kwamba suala la Urusi na Ukraine ni dogo sana kwa mtu asie na ukahaba wa kisiasa wa kufuata bwana atakaekupa maslahi bila kujali utu wa mtu huyo.

Nilisema wazi, leo hii wakati tunamkumbuka Nyerere tutafakari angesimamia wapi katika suala la Urusi na Ukraine. Nyerere alisema siku zote mipaka ya nchi zetu inayotambulika kimataifa tunaweza tusiipende, lakini sio sababu za kuvamia nchi nyingine.

Hilo moja, pili ni kwamba, hatupaswi kuwa watumwa wa nchi fulani kwa sababu ya misaada yake, kwamba kwa kuwa tunasaidiwa au tulisaidiwa na nchi fulani, basi hiyo nchi inapofanya mambo kinyume cha maumbile tutakuwa upande wake. Huo ni umalaya wa kisiasa. Dhambi ni dhambi, ifanywe na rafiki au adui.

Angalia kura zilivyopigwa Umoja wa Mataifa juu ya suala la Urusi na Ukraine, na angalia Tanzania ilisimamia wapi. Aibu tupu kwa nchi iliyojiita nchi ya mstari wa mbele kwenye ukombozi wa nchi nyingine. Nasema wazi, tulichofanya hapa ni umalaya wa siasa za kimataifa

Katika hotuba ya mwisho ya Nyerere Umoja wa Mataifa, alisema hiki anachofanya Samia leo hatutafanya hata siku moja! Lakini ndio hivyo tena. Tunafanya. Samia ame-surrender our freedom and dignity. Angalia video hapo chini.

Nchi kama Zambia, Kenya, Rwanda nk wanajitambua sana



Msimamo wa nchi za Afrika juu ya suala la Urusi na Ukraine ni jambo dogo sana linalopaswa kuongozwa na kanuni, sio maslahi ya nchi zetu

 

Attachments

  • VID-20221014-WA0000.mp4
    1.9 MB
Waafrika hawajielewi, hawajui umuhimu wa kuwa na sheria za kimataifa zinazoheshimiwa.

Ndiyo maana hata nchi zetu zenyewe zimejaa madikteta yanayoingia madarakani kwa mapinduzi au wizi wa kura


Halafu kitu kingine tunachokiamini ni kuwa Urusi na China zinawapenda Waafrika, hakuna nchi ya kibaguzi kama Urusi, hata timu ya taifa hawaruhusiwi kuchukua wachezaji weusi
 
Bora ya Urusi kuliko jambazi la dunia US
 
Hizo zote shobo.Mambo yao waachie wenyewe.

Badala ya kutumia fursa ya matajiri kuwa katika migogoro wenyewe kwa wenyewe ili nchi masikini ziamke kujitafuta, ndiyo kwanza tunazidi kufa njaa eti kisa matajiri wanapigana.

Ukishakuwa masikini uwezekano wa kuwa mpumbavu ni 90%.

Nipo busy na kutafuta ugali wangu sio kuingilia migogoro isiyonihusu.
 
Sisi sio ndege wala mnyama. End
 
Mmmh, kwa hiyo trump aliposema we are nothing but shitholes he was right
 
Mkuu umesema kitu ambacho watu wengi hawajui. Warusi ni wabaguzi wabaya wa watu weusi hata kaburu hafai? Hebu google racist killings of blacks in Russia utaona wasivyo watu hawa!
 
Unamtukuza Nyerere lkn hujui philosophy zake. Nyerere ndo mwanzilishi na muumini wa "siasa za kutofungamana na uoande wowote" na huo ndo msingi wa Tanzania. Ulitaka Samia aende kinyume na misingi yenu alafu muanze kumnanga?!
 
Mimi nadhani kafanya vzr, sisi hatuegamii upande wowote,ndio Sera yetu kitambo.

Bado hatuna misuri katika nyanja nyingi mpaka tuwe na jeuri kuchagua upande.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…