Katika ukoo wetu mimi ndiye wa kwanza kuwa mwajiriwa wa serikali, jifunze kitu hapa

Katika ukoo wetu mimi ndiye wa kwanza kuwa mwajiriwa wa serikali, jifunze kitu hapa

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Kulikuwa na minong'ono kuwa ndugu yetu mkubwa ni mchawi na ana roho ya wivu. Mafanikio anataka yawepo ndani kwake tu. Wengine walikuwa mpaka wanakuwa wa kwanza kiwilaya katika mitihani ya dhihaki (mock) darasa la saba.

Ikifika mitihani ya taifa wenzake aliyowaburuza darasani wanapangiwa Mzumbe, Kilakala, Tabora Boys n.k lakini yeye hata shule ya sekondari ya wilaya hafiki. Akibahatika basi atapata kuchaguliwa shule ya ufundi seremala.

Sometimes mtu anafanya usaili wa kwenda jeshi kila kitu kinakaa sawa, mara mambo yanacease mtu anaendelea kuwa fukara.

Brother wetu mmoja alikubalika sana mpaka aliweza kupewa kuwa kaka mkuu kuanzia la nne mpaka siku anamaliza la saba, kwenye michezo ndiyo alikuwa balaa, kila mchezo anaoshiriki lazima afike mkoani na huko mkoani hakuna wa kushindana naye. Leo hii ni maskini kabisa.

Mimi nikiwa darasa la saba nikampokea Yesu na kuokoka. Kwa mara ya kwanza katika ukoo wetu nachaguliwa kwenda sekondari tena shule ya kitaifa si ya kata au wilaya. Nilihakikishiwa kabisa kuwa sitavuka la saba na kutolewa mifano ya wenzangu, lakini Yesu akavunja mipaka mpaka sasa ni mwajiriwa wa serikali.

Nimesoma mpaka chuo kikuu, ndiyo mtu wa kwanza kuwa na degree katika ukoo wetu na ndiyo mtu wa kwanza kuionja sekondari katika Ukoo wetu, na ndiye mtu wa kwanza katika ukoo wetu kuwa Mkristo.

Yesu ndiye kiboko ya uchawi, laana, mikosi na kila hila. Ukimpokea kwa lengo jema ukiamini kuwa yeye ni njia ya kweli na uzima hatakuacha.

Kuna mambo mengi kanitendea ila napenda kwa leo tuishie hapa.
 
Sandali Ali unazingua mkuu, wewe ni upeo wako na connection ndio umekufa nya umekua hapo ulipo lakini usichokijua maisha yana pande mbili always usilisahau hilo kuna ukiristo na uislam, huku kuna jua na huku kuna mwezi na vyote vinategemeana kimoja kisipokuepo kingine utendaji kazi wake unapoteza maana.
 
Ukiwa huna Yesu unaweza kujidanganya siku zote utaweza bila yeye. Yesu amempa upeo na amemuonyesha hizo connection
Mkuu bado haujanielewa yeye anaifikia hata ROBO tu ya MO au Bakhresa? Najua hawafikii kwa ukwasi walionao hata punje

Amewahi kujihoji hao ni dini gani? Kabla hujaelewa nilichomaanisha jaribu kuuliza kwanza mkuu, simaanishi Yesu sio kitu la hasha but sometimes stop exaggerating things watu wanapigwa sana makanisani kuwanufaisha wachungaji acheni hizi kampeni
 
Tumetofautiana malengo mkuu, inabidi uheshimu hilo.

Si kila mtu ana malengo ya kua na ukwasi wa mo. Huyu mwamba yeye kupata kazi serikalini tu anajiona ana furaha na amani mno, anajihisi ni mtu aliefanikiwa.

Lakini walioajiliwa sio yeye pekee, wapo ambao wanaona hapo bado, ajira kwake haitoshi nk nk..
 
Mkuu bado haujanielewa yeye anaifikia hata ROBO tu ya MO au Bakhresa? Najua hawafikii kwa ukwasi walionao hata punje

Amewahi kujihoji hao ni dini gani? Kabla hujaelewa nilichomaanisha jaribu kuuliza kwanza mkuu, simaanishi Yesu sio kitu la hasha but sometimes stop exaggerating things watu wanapigwa sana makanisani kuwanufaisha wachungaji acheni hizi kampeni
Yeye ameeleza njia zake za mafanikio. Mo naye anajua njia zake. Mtu amepita njia ya kulia kufika mjini wewe unamlazimisha kwamba umefika mjini kwa kupita hewani.
Kwamba kumtukuza Mungu ni mpaka ufike level za Mo?
 
Sasa Yesu ameingiaje au Yesu ndio amempa kazi au Yesu ndio amemuajiri? Sometimes acheni upambe na kampeni za kijinga km hizi watu sio wajinga kiasi hicho hata km ni mfia dini huwezi ukaandika ujinga km huu ulioandikwa hapo, wewe eleza ni juhudi na kutokukata tamaa plus connection ndio vimekupa mafanikio ya kufikia malengo yako stop saying Yesu kanipa hiki Yesu kanipa kile huo ni upotoshaji mnafanya kampeni za kuingiza watu wengi kwa wachungaji wapigaji huku wao wanabaki kua masikini,

Km Yesu angekua hivyo kila anaeenda kanisani si angekua anaenda na RR sasa mbon wengine ni makapuku na kila siku wanatoa Sadaka au Yesu yupi mnaemzungumzia? Msitufanye sisi mazuzu
 
Amen AMEN Mtumishi. Natamani tuishtakie SERIKALI ya CCM kwa MUNGU, this is too much! Hii sio nchi ni pori la vibaka
 
Vipi wale pia Yesu ni tumaini lao. Kila siku wanashinda kuomba kanisani wapate kazi na hawapati. Ni kwamba yesu hawapendi au maombi hayafanyi kazi
Huyu anazingua tu humu eti Yesu watu wanatoa hadi Sadaka za kujimaliza na ajira hawapati, nini Yesu unamzungumzia Yesu yupi? fafanua maelezo sio unataja taja tu Yesu labda una Yesu wako behind the scenes ambae ni tofauti na yule anaefahamika na wengi
 
Back
Top Bottom