Katika usajiri huu wa dirisha dogo, chama langu Simba naomba muwasajiri hawa wachezaji 3 kuimarisha kikosi

Katika usajiri huu wa dirisha dogo, chama langu Simba naomba muwasajiri hawa wachezaji 3 kuimarisha kikosi

Thailand

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2019
Posts
275
Reaction score
795
Kwanza niwe muwazi mimi ni shabiki wa Simba SC haswa. Sasa hatari ninayoiona kwa musimu huu wa ligi kuu, ni ubora alionao mtani wetu Yanga SC, bila unafiki na ushabiki hakika Yanga wanakikosi cha kutisha mpaka na hofu nani wa kuweza kumzuia hasichukue ubingwa.
Kibaya zaidi ninachokiona mbele yetu ni Kichapo tutapewa na Yanga na ubingwa watachukua.
Hilo litakuwa jambo baya sana sisi mashabiki wa Simbab SC kupigwa na mtani na uingwa kunyang'anywa.

Lakini ninaona bado wanasimba tuna muda wa kuzuia mojawapo au yote yasitokee.

Udhaifu wa Simba upo sana sehemu ya katikati hasa baada ya Thadeo Luanga kuumia.
Mkude ni mzuri sana ila anaitaji viungo wenye nguvu sawa na yeye wasiochoka ili kupambana mwanzo mwisho.
Pendekezo la Kwanza ni:
1. TONOMBE MUKOKO
HUyu jamaa ni bonge la kiungo ambaye kule utupoloni hapewi tena nafasi baada ya majukumu yake kuwa covered na wachezaji wengi tu. Simba muwekeeni mzigo huyu jamaa ahamie msimbazi. Itakuwa partnership nzuri endapo MUKOKO, MKUDE NA LUANGA AU KANOUTE wanaanza kwenye game.

2. AMBROS wa Biashara United
Viongozi wa Simba mtafuteni huyu mwamba anajua kupiga ma cross hatar sana halafu ana upepo wa kutosha. Hii wingi sio ya kuicha,

3. ANUARY JABIR wa Dodoma jiji
Tuongeze idadi ya washambuliaji kwenye kikosi chetu. Huyu kijana ana mwili wa kutosha ana kimbia sana tudimuache huyu kijana kwenye msimu huu wa dirisha dogo la usajiri.
Najua viongozi wangu mnaenda kufanya usajiri msije mkafanya tena makosa ya kutuletea watoto wa shule kama BANDA, kumbukeni tunaitaji kutetea ubingwa wetu.
Wachezaji mnaoweza kuachana nao kwenye dirisha hili ni JOHN BOCO, BANDA, KOPE KISHIMBA, PASCAL WAWA.
ASANTENI
 
Wakati mtoa mada unaiwaza Yanga, Wenzio wanaiwazia Bhekane na Kotoko.

Hapa nchini Simba ilishamaliza, kwa sasa wako kimataifa zaidi.

Ilichokifanya Yanga ni kujitahidi kusajiri ili kufikia ubora ilionao Simba.
 
Wakati mtoa mada unaiwaza Yanga, Wenzio wanaiwazia Bhekane na Kotoko.

Hapa nchini Simba ilishamaliza, kwa sasa wako kimataifa zaidi.

Ilichokifanya Yanga ni kujitahidi kusajiri ili kufikia ubora ilionao Simba.
Mnapenda kujifariji!
 
Yaani simba akasajili mchezaji anayekosa nafasi yanga? We kweli matulatula fc
Sio wachezaji wote waliokosa namba Yanga ni wabovu.
Unajua Dilunga alikuwa wapi.
Amir Maftah jaazi Na.17 aliyetisha enzi hizo alitokea wapi. Kwa kifupi kuna wakati mfumo unamkataa mchezaji fulani nyota wakati bado akiwa fireee.
Mukoko bado ni Lulu sana.
Ila Uyo Anuary Jabir hapana, alitumika na jiran akapewa muamala kuumiza Mchezaj wetu muhimu.
 
Watu

255717839062_status_2851490b6bb04cb7b47bc62cec0a6b0f.jpg
 
Kumbe hapo ukoloni kuna chezaji linaitwa kishimba?
Siku hizi mnaokoteza wachezaji wa kinaijeria waliofulia, naskia wanne wanakuja mapinduzi, daah huruma kweli.

Wachezaji wa bure.
 
Kocha wa simba alivyoifunga azam alishangilia utadhani ameipiga Bayern
Polisi tanzania 1:2 Azam
Kmc 2:1 azam
Yanga 2:0 azam
 
Sio wachezaji wote waliokosa namba Yanga ni wabovu.
Unajua Dilunga alikuwa wapi.
Amir Maftah jaazi Na.17 aliyetisha enzi hizo alitokea wapi. Kwa kifupi kuna wakati mfumo unamkataa mchezaji fulani nyota wakati bado akiwa fireee.
Mukoko bado ni Lulu sana.
Ila Uyo Anuary Jabir hapana, alitumika na jiran akapewa muamala kuumiza Mchezaj wetu muhimu.
Kwa status ya simba hawezi kuchukua mchezaji anayekosa namba yanga. Amir maftah wakati anachukuliwa yanga alikuwa si tu ana namba yanga hadi timu ya taifa, dilunga alisajiliwa akitokea mtibwa ni kama kiemba au yusuph mhilu
 
Nafikiri Simba kama itahitahji kiungo mkabaji basi anahitajika mwenye uwezo zaidi ya Lwanga huyo Mukoko wa kawaida sana hana maajabu yoyote. Ni bora hata kumfikiria Fraga arudi iwapo kama atakuwa kapona.

Mapungufu makubwa sana kwa Simba sasa yapo kwa mshambuliaji wa kati. Na wakifanya kosa kama walivyofanya kosa wakati wa usajili wa dirisha kubwa basi waandike maumivu. Wanatakiwa watafute washambuliaji wawili wa kati waliokamilimika mmoja wa nje na mmoja wa ndani. Nikisema waliokamilika namaanisha wawe na uwezo mkubwa wa kufunga na kuamua matokea ya mechi hata pale timu nzima inapobanwa na timu pinzani .

Boko, Kagere na Mugalu kwa kweli toka Luis na Chama waondoke naona wanapata shida sana kufunga magoli. Walizoea kutafuniwa kila kitu sasa waliokuwa wanawatafunia hawapo. Na kama sio mawinga na viungo kufunga basi Simba ingekuwa nafsi ya chini kwenye msimamo. Na ukizingatia tena umri wa hawa washambuliaji pamoja na majeraha ya mara kwa mara basi safu nzima ya ushambuliaji pale Simba inakuwa tatizo. Kwa Simba kuanzia kipa mabeki wa kati, mabeki wa pembeni, viungo wakabaji, viungo washambuliaji na viungo wa pembeni timu ipo vizuri kiasi chake ila shida kubwa ni kwa washambuliaji wa kati tu.

Kwa hiyo narudia tena chonde chonde uongozi wa Simba katika usajili wote wa dirisha dogo tafuteni washambuliaji wawili wa kati waliokamilika wenye uwezo binafsi wa kuamua mechi.
 
Back
Top Bottom