Katika usajiri huu wa dirisha dogo, chama langu Simba naomba muwasajiri hawa wachezaji 3 kuimarisha kikosi

TATIZO MNAENDA KUWAWEKA BENCHI KAMA WAKINA JUNIOR LOKOSA,PETER MUDUHA, DANKANI NYONI, GADIEL MICHAEL, AJIBU WANAISHIA KUISHA VIWANGO
 
RIP Scout Wetu Hanspope
RIP mwamba . Hawa waliobaki na jukumu lako wameanza kuokoteza wachezaji wa mafungu kuwaleta eti kwenye majaribio. Japo usajili ni kamari lakini sikumbuki wakina Okwi, Chama, Luis, Enock, Sakho (nikiwataja wachache) walifanyiwa majaribio lini kabla ya kusajiliwa Simba.
 
Naona makolo mnajifariji humu,kwanza mukoko aondoki Yanga bado yupo kwenye mipango ya kocha nabi,mukoko mkataba wake unaisha july hope hapa kati ataongeza mkataba maana mazungumzo yanaendelea vizuri,halafu kingine makolo wanajitoa ufahamu na kumdharau mukoko mchezaji ambaye anatoka taifa lenye wachezaji zaidi ya 100 wanaocheza ulaya na bado mchezaji huyo akapenya kuitwa kwenye timu ya taifa hilo chini ya mtaalam hector cuper,kocha wa kiwango kama kile amuone mukoko halafu kolo wa mpitimbi ndani ndani huko anakuja kutoa mashudu hapa eti mukoko wa kawaida,kuna baadhi wa makolo wanahitajika mirembe aisee
 
Kiukweli kabisa Mukoko ni mchezaji mzuri lakini kwa aina ya falsafa ya uchezaji wa Simba hataweza kuwika pale Simba. Falsafa ya Simba pale kwa kiungo mkabaji ni kugawa mipira pande zote za uwanja kwa muda wote wa mchezo kama mpishi anavyogawa pilau kwenye Maulid huko uswahilini kitu ambacho kitamuwia vigumu sana Mukoko kuweza kufanya jukumu hilo kwa ufanisi. Na mbaya zaidi Mkude ghafla tu yupo "on fire" na Lwanga yupo mbioni kurudi baada ya majeraha kwa hiyo anachotaka Mukoko kukikimbia Yanga atakutana nacho Simba mara mbili yake zaidi maana atakalia mbao ndefu mpaka sugu zimtoke.

Hata ikitokea viongozi wa Simba wakataka kumsajili Mukoko itakuwa ni matumizi mabaya ya nafasi za wacheaji wa kigeni. Kosa ambalo sidhani kama viongozi wa Simba wanaweza kufanya wakati huu.
 
Kiuhalisia simba bado haijafikia level ya as vita mpira wao hata kama mliwatoa cl,kipindi ambako mukoko alikua sehemu ya kikosi,unadiliki kabisa kusema kumsajili mukoko ni matumizi mabaya ya wachezaji wa kigeni,yan mukoko unamuweka kundi 1 na kina duncan nyoni,mduhwa,lokosa,chikwede n.k,mukoko yuko camp ya drc national team muda huu mkuu,mpe heshima yake mukoko
 
Mukoko ni universal, anaweza kuoffer kitu zaidi ya kimoja uwanjani. Anaweza kucheza kama kiungo wa chini au wa juu. Pia najua kufunga. Lini mzamiru na mkude walifunga? Lini waliassist? Hayo yote Mukoko anakuoffer . Mukoko atasalia Yanga au ataenda Arabuni.
 
Makolo hawanaga akili,yaani wamlinganishe Mukoko na Mkude wa Muhimbili au asiyejua mpira zaidi ya rafu Lwanga?
 
... Mkude ni mzuri sana ila anaitaji viungo wenye nguvu sawa na yeye wasiochoka ili kupambana mwanzo mwisho.
Sijaelewa, Mkude anahitaji viungo wenye sifa hiyo ili iweje?
 
Huyo Mikoko akisajiliwa baada ya miezi mitatu majeruhi, kabla ya kumsajili Mukoko ongeeni na Mkude kwani mpaka sasa Lwanga majeruhi, yule mbrazil nae majeruhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…