Uchaguzi 2020 Katika wagombea Urais, Tundu Lissu ndiye mwenye uwezo, historia na haiba ya kupaisha heshima ya Tanzania katika diplomasia na ushirikiano wa kimataifa

Uchaguzi 2020 Katika wagombea Urais, Tundu Lissu ndiye mwenye uwezo, historia na haiba ya kupaisha heshima ya Tanzania katika diplomasia na ushirikiano wa kimataifa

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Ni jambo la wazi kabisa kwamba heshima ya Tanzania kimataifa imepotea ktk kipindi hiki cha awamu ya 5.

Rais wa Nchi ndiye mwanadiplomasia nambari one wa nchi yake, na ktk hili tuwe wakweli kwamba tumepungukiwa.

Tatizo la kwanza liko ktk uwakalilishi. Rais wetu amekuwa hahudhurii vikao muhimu vya Jumuiya za kikanda ambazo Tanzania ni mwanachama.

Kwa mfano, sidhani kama JPM amewahi kuhudhuria mkutano zaidi ya mmoja wa SADC uliofanyika nje ya Tanzania.

Tanzania ni kati ya nchi waasisi wa SADC, na tunapakana na nchi nne wanachama wa SADC. Ni muhimu sana kuwachukulia majirani na ndugu zetu hawa kwa umuhimu mkubwa.

Kwa upande wa OAU, JPM amehudhuria mkutano mmoja tu uliofanyika Addis Ababa. Pia Jpm hajawahi kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa UN unaofanyika New York.

Kwa hiyo tatizo la kwanza na muhimu kuliko yote ni mahudhurio yasiyoridhisha hata kidogo.

Tatizo la pili, ni kwamba pale ambapo amehudhuria hotuba zake na uwakilishi wake umekuwa wa kiwango cha chini. Mfano mzuri hapa ni hotuba na hoja alizotoa wakati wa mkutano wa SADC. Ni jambo la kusikitisha kwamba baadhi ya kauli alizotoa ni zile zinazosababisha " miguno " kwa wale wasikilizaji.

Kwa kweli tunahitaji Rais ambaye ana kipaji, weledi, historia, na haiba, ya kurudisha heshima ya Tanzania ktk mawanda ya kimataifa. Tanzania ni taifa changa lakini tuliheshimika kutokana na uwakilishi thabiti na wa viwango wa wana-diplomasia namba one wa nchi hii kama wakati wa Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Ben Mkapa, na Mzee Jakaya Kikwete.

Katika safu inayojumuisha Dr.John Magufuli, Mh.Bernard Membe, Prof.Ibrahim Lipumba, Mh.Tundu Lissu, na Mh.Yeremia Maganja, ni yupi atarejesha heshima ya Tanzania kimataifa?

Kwa maoni yangu ni Tundu Antiphas Lissu.

cc Nguruvi3, Kilatha, Mag3, Erythrocyte , Molemo, tindo
 
Kimataifa tumepwaya sana. Kwa bahati mbaya hakuna mwenye uthubutu wa kusema wakiwemo wastaafu

Sisi kama nchi changa tulikuwa na 'silaha' yetu moja, ushawishi wa siasa za kanda na kimataifa. Tuliheshimika

Tuliambiwa sababu za Rais kutosafiri ni kubana matumizi. Hata hivyo, kadri muda unavyosonga tunashudia hoja hiyo ikijiua yenyewe. Vipi ndege inaweza kumchukua msanii Nairobi iwe kubana matumizi? Vipi kumtuma VP au PM kuwe kubana matumizi?

Katike eneo tulilopoteza ni hili la diplomasia! tumepoteza 'silaha' yetu muhimu sana.
 
Tulipokwenda Uganda, mwandishi wa The Reuter’s aliuliza swali, ilibidi Museveni alitafune kidogo ili tuweze kumeza.

Zimbabwe waliposikia Kiingereza Chetu cha Ze Comedy walishindwa kutuelewa wakati tulijinasibu kuwa Mnanangwa ni best yetu.

Kagame ameshatuona waluga luga ametupiga Tanzanite na kusepa.
 
Uhusiano wa kimataifa sio raisi kusafiri au kuhutubia kwenye international diplomatic conferences.

Uhusiano wa kimataifa ni bilateral agreements, multilateral agreements, Signing up to UN conventions, Regional relationship and all other things which allows Tanzania to be considered part of the international community.

Na mpaka sasa tupo kwenye makubaliano yote ya kimataifa kama ilivyokuwa huko nyuma.

Halafu unapokuwa raisi wa nchi kila unaposafiri unakuwa na experts wa hayo maeneo unayotembelea kutoka wizarani wao ndio wanaku guide uonge nini, uwe na tabia gani kulingana na tamaduni zao etc with diplomatic protocols; raisi anakuwa ni symbolic tu representative wa nchi.
 
Hamna siku serikali itakuletea ugali na hela ya mboga nyumbani kwako View attachment 1558721
Lissu alikuwa anazungumzia ndege katika muktadha tofauti kabisa. Hata siku moja hakuwa kusema tusiwe na ndege yoyote nchini kwetu.

Alikuwa anazungumzia huu ununuzi wa ndege za ATC bila mipangilio yoyote. Wewe ni mfano mzuri sana wa akili za wahitimu wa hizi shule za kata za Bongo. Wahitimu wengi walikuwa wanakariri hivyo jambo dogo tu la kutafakari linawashinda.
 
wananchi hawataki shobo ya kimataifa bali utatuzi wa shida zao locally
 
Uhusiano wa kimataifa sio raisi kusafiri au kuhutubia kwenye international diplomatic conferences.

Uhusiano wa kimataifa ni bilateral agreements, multilateral agreements, Signing up to UN conventions, Regional relationship and all other things which allows Tanzania to be considered part of the international community....
Si kweli tumejitoa kwenye mhakama, tumefuta makubaliano ya biashara za kimataifa kuhusu arbitration n.k. Lakini pia lazima utambue kuwa viongozi wanapokutana kuna mengi wanaongea na hasa 'deal' za biashara na mashirikiano. Ndiyo maana viongozi wote wanaokwenda UN huwa wana mikutano ya pembeni kukutana na wenzao ambao si rahisi kuwapata wote katika muda mfupi.

Huwezi kutenga Diplomasia na uchumi na huwezi kufanya diplomasia kwa 'virtual'. Diplomasia ni pamoja na uchumi na usalama. Haya ni mambo muhimu sana kwa Taifa lolote

Tulikuwa tunaheshimika kwasababu tulikuwa na ushawishi wa diplomasia za kimatifa licha ya umasikini wetu. Kwa kuheshimiwa ilikuwa rahisi sana kwetu kufikiwa na jumuiya ya kimataifa, umasikini haukuwa kovu.

Kwasasa hivi hata mikutano ya Corona ya EA hatupo, huko SADCC ndiyo hala hala tunasetiriwa kwa 'legacy'

Nchi yetu ina survive kwa diplomasia ya akina Nyerere, Mkapa ,Mwinyi, Kikwete. Dplomasia iliyojengwa na akina Malecela, Salimu Ahmed, Balozi Mahiga n.k.

Hali ikiendelea kama ilivyo, ipo siku wapo watakaouliza kama Tanzania imechukua nafasi ya Pluto katika idadi ya sayari
 
Nguru6582077 said:
Si kweli tumejitoa kwenye mhakama, tumefuta makubaliano ya biashara za kimataifa kuhusu arbitration n.k. Lakini pia lazima utambue kuwa viongozi wanapokutana kuna mengi wanaongea na hasa 'deal' za biashara na mashirikiano. Ndiyo maana viongozi wote wanaokwenda UN huwa wana mikutano ya pembeni kukutana na wenzao ambao si rahisi kuwapata wote katika muda mfupi..
Hakika katika mahusiano ya kimataifa Tanzania tuna viwango vya chini mno
 
Endelea kushabikia ccm sjui chadema nccr wala act

Hamna siku serikali itakuletea ugali na hela ya mboga nyumbani kwako
Wewe ni mjinga hakuna mtu anaetaka serikali imletee ugali watu wanataka mifumo huru yakutafuta Hela wenyewe
 
Ni jambo la wazi kabisa kwamba heshima ya Tanzania kimataifa imepotea ktk kipindi hiki cha awamu ya 5.

Rais wa Nchi ndiye mwanadiplomasia nambari one wa nchi yake, na ktk hili tuwe wakweli kwamba tumepungukiwa...
Umetumwa na Robert Amstardam?
 
Si kweli tumejitoa kwenye mhakama, tumefuta makubaliano ya biashara za kimataifa kuhusu arbitration n.k. Lakini pia lazima utambue kuwa viongozi wanapokutana kuna mengi wanaongea na hasa 'deal' za biashara na mashirikiano. Ndiyo maana viongozi wote wanaokwenda UN huwa wana mikutano ya pembeni kukutana na wenzao ambao si rahisi kuwapata wote katika muda mfupi.

Huwezi kutenga Diplomasia na uchumi na huwezi kufanya diplomasia kwa 'virtual'.
Diplomasia ni pamoja na uchumi na usalama. Haya ni mambo muhimu sana kwa Taifa lolote

Tulikuwa tunaheshimika kwasababu tulikuwa na ushawishi wa diplomasia za kimatifa licha ya umasikini wetu.
Kwa kuheshimiwa ilikuwa rahisi sana kwetu kufikiwa na jumuiya ya kimataifa, umasikini haukuwa kovu.

Kwasasa hivi hata mikutano ya Corona ya EA hatupo, huko SADCC ndiyo hala hala tunasetiriwa kwa 'legacy'

Nchi yetu ina survive kwa diplomasia ya akina Nyerere, Mkapa ,Mwinyi, Kikwete. Dplomasia iliyojengwa na akina Malecela, Salimu Ahmed, Balozi Mahiga n.k.
Hali ikiendelea kama ilivyo, ipo siku wapo watakaouliza kama Tanzania imechukua nafasi ya Pluto katika idadi ya sayari
Tumejitoa kwenye arbitration ipi? ingekuwa ivyo ndege zisingekuwa zinakamatwa nje ya nchi.

Hayo mengine labda kama una muamini Membe na story zake. Sitoongelea sana kuhusu diplomatic rituals za China na nchi za Africa kwa ujumla wake kwasababu sina uelewa nazo kivile.

Hila kwa West raisi awezi kuingia deal na nchi au kusamehe mkopo yeye mwenyewe; diplomatic imejikita kwenye ku facilitate mambo na kufuata standpoint yao juu ya nchi fulani.

Mfano nakumbuka enzi Kalaghe akiwa balozi UK nilikuwa nawafahamu watu waliokuwa wanashinda ubalozini; sehemu kubwa ya kazi yake ilikuwa kushiriki warsha mbali mbali za kibiashara ambazo anaweza shawishi wawekezaji. Sasa sijui kama mama Mighiro nae anafanya ivyo maana hao jamaa nao nishapunguza kwenye maisha yangu.

The point is there official diplomatic communication channels, the only benefit of one 2 one is either to influence support on international matters, but the rest as far as the west is concerned you need to follow appropriate channels.

Tender tu za UK zilizofanyika miaka ya 70 kuuzia ndege Saudi Arabia kwa zaidi ya $40 billion dollars pamoja na kutengeneza ajira kwao, mpaka leo zinachunguzwa kama zilifuata taratibu sahihi za kisheria na kuna nguvu kubwa ya kuzuia upelelezi.

Sasa sijui ni kiongozi gani wa West atatoa ahadi bila ya kufuata taratibu zao za kufanya mambo labda kama anataka kuchukua headlines for wrong reasons.

Kusafiri kwa raisi sometimes ni symbolic tu the real dimplomatic negotiations occurs behind closed doors.
 
Hizi ndizo naita akili za kikojozi. Lissu alikuwa anazungumzia ndege katika muktadha tofauti kabisa. Hata siku moja hakuwa kusema tusiwe na ndege yoyote nchini kwetu. Alikuwa anazungumzia huu ununuzi wa ndege za ATC bila mipangilio yoyote. Wewe ni mfano mzuri sana wa akili za wahitimu wa hizi shule za kata za Bongo. Wahitimu wengi walikuwa wanakariri hivyo jambo dogo tu la kutafakari linawashinda.
Yaani kuna wakati unajiuliza hawa vijana hizi degree wanazipataje unakosa majibu?
 
Ni jambo la wazi kabisa kwamba heshima ya Tanzania kimataifa imepotea ktk kipindi hiki cha awamu ya 5.

Rais wa Nchi ndiye mwanadiplomasia nambari one wa nchi yake, na ktk hili tuwe wakweli kwamba tumepungukiwa...
Wachaaa Tujenge nchi Kwanza ushirikiano Wa kimataifa upon tu hatujagombana na MTU Tutakapiwahitaji tutawasiliana nao watakapotuhitaji wanakaribishwa TUNAIHITAJI MAENDELEO YA NDANI KWANZA HUTATI RAIS MZURULAJI SISI TUMEONA HASARA ZAKE
 
Ni jambo la wazi kabisa kwamba heshima ya Tanzania kimataifa imepotea ktk kipindi hiki cha awamu ya 5.

Rais wa Nchi ndiye mwanadiplomasia nambari one wa nchi yake, na ktk hili tuwe wakweli kwamba tumepungukiwa...
Kwani hayo mataifa yana shida gani na tanzania?
Kama ni misaada yanatoa na mikopo yanatoa, sasa nyie uhusiano gani mnataka?
Mnataka wawakoromee shingoni ndo mtaona mahusiano mazuri au?
Tumieni bakiri zenu basi.
 
Ni jambo la wazi kabisa kwamba heshima ya Tanzania kimataifa imepotea ktk kipindi hiki cha awamu ya 5.

Rais wa Nchi ndiye mwanadiplomasia nambari one wa nchi yake, na ktk hili tuwe wakweli kwamba tumepungukiwa...
Hivi wewe na andiko lako reeeeeefu unategemea Tundu awe Amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama.Hebu kuweni serious chadema msidhalilishe nchi na watanzania bana.
 
Ni jambo la wazi kabisa kwamba heshima ya Tanzania kimataifa imepotea ktk kipindi hiki cha awamu ya 5.

Rais wa Nchi ndiye mwanadiplomasia nambari one wa nchi yake, na ktk hili tuwe wakweli kwamba tumepungukiwa.

Tatizo la kwanza liko ktk uwakalilishi. Rais wetu amekuwa hahudhurii vikao muhimu vya Jumuiya za kikanda ambazo Tanzania ni mwanachama...
Mimi john magufuli nimefanya dhambi gani hadi mnataka kuninyima miaka mitano mingine ?

Jameni muwage na huruma basi.
 
Sasa mabalozi walikuwepo wa kazi gani yaani bado uko nyuma kimawazo mtoa mada
 
Back
Top Bottom