Ni jambo la wazi kabisa kwamba heshima ya Tanzania kimataifa imepotea ktk kipindi hiki cha awamu ya 5.
Rais wa Nchi ndiye mwanadiplomasia nambari one wa nchi yake, na ktk hili tuwe wakweli kwamba tumepungukiwa.
Tatizo la kwanza liko ktk uwakalilishi. Rais wetu amekuwa hahudhurii vikao muhimu vya Jumuiya za kikanda ambazo Tanzania ni mwanachama.
Kwa mfano, sidhani kama JPM amewahi kuhudhuria mkutano zaidi ya mmoja wa SADC uliofanyika nje ya Tanzania.
Tanzania ni kati ya nchi waasisi wa SADC, na tunapakana na nchi nne wanachama wa SADC. Ni muhimu sana kuwachukulia majirani na ndugu zetu hawa kwa umuhimu mkubwa.
Kwa upande wa OAU, JPM amehudhuria mkutano mmoja tu uliofanyika Addis Ababa. Pia Jpm hajawahi kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa UN unaofanyika New York.
Kwa hiyo tatizo la kwanza na muhimu kuliko yote ni mahudhurio yasiyoridhisha hata kidogo.
Tatizo la pili, ni kwamba pale ambapo amehudhuria hotuba zake na uwakilishi wake umekuwa wa kiwango cha chini. Mfano mzuri hapa ni hotuba na hoja alizotoa wakati wa mkutano wa SADC. Ni jambo la kusikitisha kwamba baadhi ya kauli alizotoa ni zile zinazosababisha " miguno " kwa wale wasikilizaji.
Kwa kweli tunahitaji Rais ambaye ana kipaji, weledi, historia, na haiba, ya kurudisha heshima ya Tanzania ktk mawanda ya kimataifa. Tanzania ni taifa changa lakini tuliheshimika kutokana na uwakilishi thabiti na wa viwango wa wana-diplomasia namba one wa nchi hii kama wakati wa Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Ben Mkapa, na Mzee Jakaya Kikwete.
Katika safu inayojumuisha Dr.John Magufuli, Mh.Bernard Membe, Prof.Ibrahim Lipumba, Mh.Tundu Lissu, na Mh.Yeremia Maganja, ni yupi atarejesha heshima ya Tanzania kimataifa?
Kwa maoni yangu ni Tundu Antiphas Lissu.
cc Nguruvi3, Kilatha, Mag3, Erythrocyte , Molemo, tindo