Katles za nyama

Katles za nyama

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji

1) Nyama ya kusaga robo
2) Viazi mbatata kg 1
3) Karoti 1 kubwa
4) Pilipili hoho 1
5) Ndimu/limao 2
6) Pilipili manga ya unga 1 tea spoon.
7) Uzile wa unga 1 tea spoon
8) Kitunguu thomu nusu
9) Tangawizi kiasi
10) Chumvi kiasi..
11) Mafuta nusu lita
12) Mayai 4.
14) Unga wa ngano robo

Namna ya kutaarisha
1) Katakata hoho ndogo ndogo na karoti
2) Saga thomu na tangawizi kwa pamoja
3) Weka nyama kwenye sufuria safi then add chumvi,limao,uzile na pilipili manga.iache iwive kwa dakika 10..
4) Weka karoti na pilipili hoho changanya vizuri baada ya kuwiva opoa weka pembeni
5) Chemsha viazi vyako ulivomenya hadi viwive lainiii
6) Viponde ponde
7) Changanya viazi vyako pamoja na nyama hadi vichanganyike
8) Viringa viringa viwe vya duara au shepu kama ya yai
9) Pakaaa unga wa ngano juu yake
10) Weka mafuta kwenye karai hadi yapate moto
11) Vunja mayai yako na uyakoroge vizuri
12) Chovya viazi vyako ambayo umetengeneza shepu kwenye mayai na ukaange kwenye karai hadi viwe brown...

Katles tayari kwa kuliwa.
 
mimi49 Swts King'asti Heaven on Earth... BAK MziziMkavu 24hrs donlucchese..
1383861837053.jpg
1383861848802.jpg
 
Last edited by a moderator:
nikipata muda napika hakyanani! sasa can i skip eggs coz i dont eat eggs?!will they test good without?
 
My dia nyama dk 10 inakuwa imeiva......au itaiva wakati waikaanga

Nyama ya kusaga/kima ina wiva mda mfupi sana ....yaani hapo itachukua dakika20...wakat karoti zinawiva nayo itaendelea kuwiva
 
nikipata muda napika hakyanani! sasa can i skip eggs coz i dont eat eggs?!will they test good without?

Pole sana...ukiwa hujatia mayai nahisi zote zitavurugika wakati unaziweka kwenye karai...
 
Mahitaji


1)nyama ya kusaga robo
2)viazi mbatata kg 1
3)karoti 1 kubwa
4)pilipili hoho 1
5)ndimu/limao 2
6)pilipili manga ya unga 1 tea spoon.
7)uzile wa unga 1 tea spoon
8)kitunguu thomu nusu
9)tangawizi kiasi
10)chumvi kiasi..
11)mafuta nusu lita
12)mayai 4.
14)unga wa ngano robo

Namna ya kutaarisha
1)katakata hoho ndogo ndogo na karoti
2)saga thomu na tangawizi kwa pamoja
3)weka nyama kwenye sufuria safi then add chumvi,limao,uzile na pilipili manga.iache iwive kwa dakika 10..
4)weka karoti na pilipili hoho changanya vizuri baada ya kuwiva opoa weka pembeni
5)chemsha viazi vyako ulivomenya hadi viwive lainiii
6)viponde ponde
7)changanya viazi vyako pamoja na nyama hadi vichanganyike
8)viringa viringa viwe vya duara au shepu kama ya yai
9)pakaaa unga wa ngano juu yake
10)weka mafuta kwenye karai hadi yapate moto
11)vunja mayai yako na uyakoroge vizuri
12)chovya viazi vyako ambayo umetengeneza shepu kwenye mayai na ukaange kwenye karai hadi viwe brown...

Katles tayari kwa kuliwa.

dah,haya sasa mashikolo.hivi pale kwa mama muuza tandale pale hii kitu inapatikana na mimi nikaionje?
 
Back
Top Bottom