Katoro ni Business center inayokua kwa kasi ya ajabu

Katoro mji utakuwa sana sema mipango miji wajipange.Nyumba zinakuwa kama uyoga.Vijana wadogo wamefanikiwa.
 
Nakuja Katoro mwezi wa 10 kusaka fursa
 
Veep kuhusu biashara ya miamala ya mitandao ie mpesa, halopesa, airtel money, NMB, crdb inaenda hapo Katoro??
 
Katoro ni pazuri sana kwa biashara ni eneo ambalo watu kutoka maeneo mbalimbali wanafuata bidhaa,after Mwanza na Kahama, Katoro ni next kwenye ukuaji Kanda ya ziwa, miji kama Bukoba, Kigoma, Nyakanazi, Runzewe, Biharamulo, Geita, Wafanyabiashara wake wanafuaata bidhaa katoro
 
Veep kuhusu biashara ya miamala ya mitandao ie mpesa, halopesa, airtel money, NMB, crdb inaenda hapo Katoro??
Inaenda Mkuu, Pale kuna wafanyabiashara wengi sana uhitaji wa transction Lazima uwe mkubwa, Naona kuna watu wachanganya hiyo biashara pamoja na biashara ya kuuza Simu na accesories zake kama Charger, SD Cards, USB Cables, Covers E.T.C
 
Sawa ngoja nijipange mkuu.
 
Sema ina kaeneo kadogo sana ambako ndio sphere of interest.
 
Pamoja na uzuri wake kibiashara lakini ndiyo mji wenye huduma mbovu ya maji (wengi wanategemea maji ya visima), barabara ya lami ni moja tu(barabara kuu), vumbi la ule mji ni hatari, usalama pia ni mdogo, nyaya za umeme zinaning'inia kama kamba za kuanikia nguo vile, ufinyu wa vyakula, ufinyu wa maeneo ya starehe baada ya kazi... Tegemea kufanya biashara kwa kupata faida ndogo ndogo sana kulingana na ushindani, unless ujiingize kwenye madini ndiyo utoboe haraka

By the way ni mji mzuri kiutafutaji ila sio kuishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…