The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,778
- 8,232
"Miaka ya 4500 kabla ya Kristo, wakati jamii zilipoanza kuelimika, askari walijitolea kwa moyo wa dhati kuilinda jamii dhidi ya watu wabaya. Walikuwa ngao ya wanyonge, walinzi wa haki na utulivu.
Magenerali kama Hannibal Barca wa Karthage (Tunisia ya sasa), aliyepambana kulinda taifa lake dhidi ya nguvu ya Roma; au Simon Bolivar, aliyeongoza mapambano ya uhuru dhidi ya ukoloni huko Amerika Kusini – hawa walikuwa askari wa dhamira, si vibaraka wa wanasiasa.
Lakini leo – katika karne ya 21 – askari wamebadilisha mfumo, wameacha kutumia akili zao: sasa wanalinda wenye tamaa dhidi ya wananchi waliowaamini. Wanasimama kulinda majumba ya kifahari na mikutano ya hila, huku wakitawanya risasi kwa wanaodai haki.
"Huu si ulinzi, ni usaliti wa asili ya kazi yao."
Nani aliyewaroga?
Mnavaa sare zenu kama miungu wa amri, lakini mioyo yenu imevishwa minyororo ya woga. Mlipoapa kiapo, mliahidi kuilinda katiba, haki, na utu. Lakini leo, mnawaumiza wale mliyoapa kuwalinda. Mnawaogopa wanasiasa, mkawaogopesha wananchi. Hii si kazi – huu ni usaliti wa kiroho.
Mlitumwa kulinda nchi, mkageuka mnalinda matumbo ya wachache. Mlitumwa kudumisha amani, mkageuka chanzo cha vurugu. Mlitumwa kulinda maisha, mkageuka vifo vya raia wasio na silaha.
Je, hamjiulizi?
Kwa nini mnajificha nyuma ya barakoa ya kutotafakari? Kwa nini mnaogopa kuwa binadamu kabla ya kuwa askari? Haki ya mtu haitaamuliwa kwa amri ya mkuu bali kwa sauti ya dhamira.
Mtazame picha hii: nyuso zimejificha nyuma ya tabasamu za plastiki. Kila mmoja anacheka, lakini hakuna anayefurahi. Kila mmoja anatii, lakini hakuna anayefikiri.
Usisubiri historia ikuhukumu. Jihukumu sasa kwa dhamira. Jua: risasi yako leo inaweza kuwa kilio cha kizazi chako kesho.