Wapinzani wanashindwa kutumia vizuri Fursa ya mgogoro ndani ya CCM ambao kiukweli umekua mkubwa sana.
CCM walifanikiwa kuisambaratisha CUF kwa dhulma.
Mbinu zile zile za kujenga dhulma zinaendelea kutumika kusambaratishana wenyewe kwa wenyewe.
Hakika Bila CCM kufa kwa muda na kuibuka tena kikiwa Chama chini ya mfumo imara wa Katiba bora itakayoofanya nchi hii ipate viongozi kwa Hoja sio kwa vioja na migogoro.
Tanzania kwa muda mrefu tunanufaika kupata viongozi kupitia migogoro badala ya kupata migogoro kwa Hoja.
Nadhani 2020 iwe Mara ya kwanza kabisa kwa Tanzania kupata viongozi kupitia Hoja zenye agenda ya maendeleo na utaifa.
Hatutegemei kupata viongozi kwa kutumia Migogoro ,hasira, mabomu na kuhujumiana badala yake tutoe Fursa ya kupata viongozi bora kabisa kwa hoja,Historia safi ya kutetea Mali za umma kwa kujitoa sio kwa kushiriki kisha kugeukana.
Wapinzani waungane kwa kujenga itikadi moja kama ile ya Ukawa lakini awamu hii wasiwe na pupa ya Ikulu tu bila kiachiana majimbo na kutumia Rasilimali zao kidogo kuweza kujenga Mtandao.
Mbowe pia ni Tatizo kubwa Mana ana ubinafsi na uroho wa Mali kupindukia.
Hatuwezi kuwa na nchi itakayokuwa kiongozi mkubwa wa Chama mkwepa kodi.
Ikitokea Mbowe kwa uingwana akaachia Chama kwa Tundu Lisu au John Heche na kutoa ushirikiano mkubwa basi CCM ingesambaratika kabisa.
Watu wengi sana wanaipenda Chadema lakini wanamchukulia Mbowe kama MTU asiye na mikakati na mbinu za Kisomi zaidi ya kusubiri matukio ndipo aibuke.
CCM imepoteza dira kwa sasa ila wapinzani wakichelewa wataikuta CCM ikiendelea na safari yake kama kawaida.
Ni Chama kinachocheza na udhaifu wa wapinzani na ujinga wa watanzania.
Mbowe hata jimbo lake ameshindwa kufanya siasa na kuongeza wanachama badala yake wanatimkia CCM na kila kukicha wanazidi kuunga mkono juhudi.
Mbowe amefanya mengi lakini kwa sasa amwachie mwingine.
Akichelewa baada ya mgogoro wa CCM kuisha ataegemee mgogoro mkubwa sana kuobuka Chadema na utakisambaratisha kabisa