Kauli chafu zilizokuwa normalized Jamii Forums ambazo ni adui mkubwa sana kwa maendeleo ya Tanzania

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Sio mara moja sio mara mbili watu wakileta changamoto zinazowakumba Watanzania humu kumekuwa na kauli chafu kutoka kwa baadhi ya wanaJF ambao nao ni Watanzania/Waafrika pia
Mfano, ukileta tatizo linalokumba jamii za Watanzania utakuta mtu anacomment "Waafrika ni nyani waliochangamka"

Kuna siku humu nilileta mada kuhusu namna ya kudeal na mitaa ya Uswahilini nikatoa na solution ambazo binafsi nilihisi zingeweza kubadili maisha ya Watanzania, watu kwenye comments wakawa wanasema "Uchafu ni asili ya Watanzania, hata ufanyeje hauwezi wabadilisha"
Leo tena kuna mada imeletwa, watu wanaendelea na hizi dangerous and destructive comments wakidhani wanaweza kujiondoa kwenye part ya tatizo wakitumia kauli chafu kama hizo

Kauli kama “Waafrika ni nyani waliochangamka” siyo tu criticism ya Tanzania, ni kujishusha thamani kama jamii. Mtu anaweza kukosoa rushwa, uzembe, miundombinu mibovu, elimu, uongozi au utamaduni fulani bila kuhitimisha kwamba watu wa bara zima wana kasoro ya asili.

Kwanza mnapaswa kuelewa madhara ya kauli kama hizi

1. Inageuza matatizo yanayoweza kutatuliwa kuwa “nature” ya watu.
Kama barabara hazijengwi vizuri, taasisi zinafanya kazi vibaya, au miji imepangwa vibaya, hayo ni matatizo ya sera, taasisi, incentives, elimu, historia na maamuzi ya binadamu. Ukisema “sisi ni nyani”, unahamisha mjadala badala ya kufikiria tubadilishe nini unaaminisha watu “hatuwezi kubadilika.”

2. Unajitenga na jamii yako yenyewe.
Mtu anayesema “Waafrika ni wajinga”
huku yeye akiwa Mwafrika analeta mambo ya "Us vs them” ambayo haina mantiki. Mtu anaweza kuwa anakosoa tabia zinazomzunguka, lakini yeye pia ni sehemu ya mazingira hayo na anaweza kuwa sehemu ya suluhisho. Wengi hawataki kuwa part ya tatizo au suluhisho kwenye matatizo ya jamii zao wenyewe kwa hiyo wanajitenga kwa kauli kama hizi as if wao sio part ya jamii

3. Zinaweza kuathiri self-perception.
Ukirudiwa mara kwa mara kwamba kundi lako ni duni, baadhi ya watu wanaweza kuanza kuona mafanikio ya watu wao kama exceptions badala ya ushahidi kwamba uwezo upo. Hapo criticism inaweza kugeuka kuwa fatalism. Unaintroduce mindset ya “Hatuwezi kuwa kama X kwa sababu sisi ni Waafrika.”
Kusifia mafanikio ya nchi nyingine sio tatizo kabisa. Tunaweza kusema "Ujerumani imejenga mfumo mzuri wa vocational training; Tanzania inaweza kujifunza.” Hiyo ni comparison yenye manufaa. Tatizo linaanza pale comparison inapokuwa “Wazungu wana akili, Waafrika ni nyani.” Hapo umeacha kuchambua institutions na umeanza kuweka tofauti kwenye “race.”
Inapuuza mifano inayopingana na generalization hiyo.

Kwanza Afrika sio jamii moja yenye outcome moja. Kuna Waafrika wanaounda kampuni, viwanda, teknolojia, taasisi bora, miji iliyopangwa, tafiti za kisayansi na innovations. Na ndani ya Tanzania yenyewe kuna watu wanaofanya kazi kubwa. Wapo Watanzania wengi tu wana mafanikio kuliko watu wengi wa Ulaya. Tayari ni ushahidi tosha kuwa tatizo sio Uafrika

Kwa mfano hili la uchafu, mbona Rwanda wanakaa Waafrika na nchi yao ni safi na organised? Humu kila mara mtu akileta solution ya matatizo comment section zinaanza kuvamiwa na watu wenye insecurities zao na kujaza destructive comments kupinga jitihada zozote za mabadiliko kama jamii. Unakuta mtu anawaaminisha watu kuwa Watanzania hawawezi kubadilika, mtu anasema haya hata kabla hizo idea zenyewe hata hazijajaribiwa.

Leo kuna mtu nimeona eti anacomment "Watanzania ni wachafu hata ulete sera nzuri na kuimplement, nawapa miezi miwili tu wanarudi vilevile kwenye uchafu". Hizi ndio mindset tunazotakiwa kuzieliminate
Kwanza wewe unayesema hivyo ni Mtanzania, ni part ya tatizo na una uwezo wa kuwa part ya solution, usidhani hauhusiki na matatizo ya Tanzania
Pili kama ukileta sera na zikafeli baada ya miezi miwili, unapaswa kuangalia mlikosea wapi na kutoa suluhisho. Hivyo ndio taifa linavyomove foward. Sio eti kusema Uchafu ni nature yetu, hatuwezi kubadilika. Hata kama mtu anataka kuibadili Tanzania akikutana na comments kama hizi anaweza kukata tamaa

Nachukizwa sana na kauli kama “Hakuna tunachoweza kufanya kwa sababu sisi ni Waafrika". Ni kauli hatari sana kwa taifa. Taifa haliwezi kujengeka kama watu wake wanaamini mapungufu yao ni ya kudumu na ya asili, na hakuna namna ya kuyabadilisha
 
Enzi za utumwa!! Mzungu alimwambia mwafrika anawe mikono kwa sabuni akitoka chooni. Ananawa tu wakati mzungu yupo. Mzungu akimgeuzia kisogo hanawi hata kwa maji, anasakata ugali kwa kwenda mbele. Mzungu akachukia na kutumia fimbo!!
 
Wengi tunaoandika na kuhoji ukweli huu ni watu wa kawaida sana
Mtu anajitolea kuchimba kisima kwa ajili ya majirani ameweka mpaka simtank na bomba kwa sababu serikali imeshindwa kuwawekea watu wake
Halafu anakuja mtu anaiba motor na mwingine anachimbua mpaka bomba
Sasa hao utawaitaje boss
Kiongozi mkubwa tena Top aliuliza eti anashangaa kwanini sisi ni masikini

Kama yeye kaongea hivyo je wa chini wasemeje?

Kama tunaweza kwanini tusubiri serikali izibue mitaro (ingawa ni kodi zetu)
Lakini tusubiri El Niño ivunje nyumba zetu ndio tuanze kulia ooh serikali wakati sasa tunaweza kusafisha wenyewe?

Think about it
 
Wezi wapo kila sehemu duniani hapa. Ukiweka miundombinu ikaibwa kitu sahihi ni kuimarisha security eneo hilo ili kuwadaka wanaofanya huo uharibifu ili wawe put in their place
 
Sijui ndio Sera au Sheria.. Serikali inataka kusimamia kila kitu na imeweka adhabu ni fedha, hilo ni tatizo namba moja.

Pili elimu hasa ya sasa haifundishi namna yakukabiliana namazingira yanayotuzunguka wala kufundisha wajibu wa kila mtu ni upi katika kutatua changamoto zilizopo.

Tatu katika familia jukumu la malezi kwa asilimia kubwa limeachwa kwa Serikali wazazi hawataki kuwajibika na wanaona mzigo. na matokeo yake ndio haya ya kukutana na comment za watu wazima zenye kukata tamaa.

Ubinafsi ni Sumu iliyopandwa na mifumo ya watawala hivyo kila mwenye wazo zuri anachukiwa kwa hofu yakuja kuonekana yeye ni Bora hapo mbeleni pindi wazo lake likifanikiwa.

kwakumalizia. tunaishi katika jamii ya BORA TUKOSE WOTE na si BORA TUPATE WOTE.

Muda ni Mwalimu Mzuri Sana. Nimekaa Paleeee
 
Wa Africa tunajidogosha wenyewe
Unakuta mtu anafanyia bullying mtu mweusi wa ngozi kisa yeye ngozi yake ni ng'aavu
Then akisikia wazungu wana wabagua wa Africa analalamika

Mtu kama huyu mjinga wa mwisho kabisa

Hukusu hoja yako :
Haijalishi zamani huko mababu zetu walijisaidia vichakani
Haina maana na sisi tuendeleze hiyo tabia lazima tukubali ku copy mambo positive na yenye tija

Uchafu kwenye jamii ni ishara ya watu kutostarabika

Na ili ujue kaka watu uchafu wanauchukulia kawaida au kama tamaduni we panda daladala uone
Mtu anafanya kazi ngumu kutwa nzima anatoka jasho baya
Hakuna sehemu ya kuoga lakini hata kufuta kufuta kwapa anashindwa 🙌🙌
 
Sahihi kabisa. Uchafu tumeufanya kama tamaduni Tanzania, sio kwamba ni nature yetu
Hii ni just culture mbaya, na kama tu zilivyo culture nyingine, inaweza kutokomezwa vizuri tu. Jitihada zetu zinapaswa ziwepo kwenye kutokomeza hizo culture na sio kuanza kuaminisha watu kuwa uchafu ni asili yetu
Hata India, watu wake wahindi wanachafua sana miji yao, lakini ukienda state kama Kerala ni pasafi mno na wanaishi haohao wahindi
Same kwa hapa kwetu, miji mingi ya Africa ni michafu ila ukienda Kigali ni pasafi mno na wanaishi haohao Waafrika. Hapa Tanzania pia kuna mitaa ukienda ni misafi sana na wanakaa Watanzania wenzetu
Tatizo sio asili bali ni utamaduni. Umesema vyema, tuna utamaduni mbaya kwenye suala la usafi
 
Kujidharau ndio tatizo letu waafrika. Psylogically hii kitu ina madhara makubwa sana
Madhara makubwa sana. Jamii ikiwa na watu wanaoamini kuwa wao ni duni tu naturally ni ngumu kupata mabadiliko hapo
 
Kama uliwahi kusikia tulijiita mataifa ya wanyonge. How bro? That was a beautiful mistake if you know what I mean. Mimi sio mnyonge. Hata siku moja tusikubali unyonge.
 
Wezi wapo kila sehemu duniani hapa. Ukiweka miundombinu ikaibwa kitu sahihi ni kuimarisha security eneo hilo ili kuwadaka wanaofanya huo uharibifu ili wawe put in their place
Wizi unajulikana lakini huu ni ujinga unafukua pipe ya maji? Kwa thamani gani?
Huo ni msaada kwa wananchi
Tatizo ni malezi
Yaani kuna vitu sio vya kuiba kwa kweli
Duniani kuna wezi sawa lakini mabomba ya plastic huo ni roho mbaya tu
 
Mkuu ni kweli uchafu ni asili ya waafrica ushaona wapi mzungu anakunya vichakani? Alafu kwenye nyani hapo mkuu mbona ni kweli sisi ni nyani tuliochangamka wewe huoni Hadi Tlaatlaah anatumiaga hii 🐒
😹😹😹😹 Mtsiewwww
 
Back
Top Bottom