Kauli hii inaashiria madhara makubwa itakayokumbana nayo Urusi na dunia kwa ujumla endapo....

Kauli hii inaashiria madhara makubwa itakayokumbana nayo Urusi na dunia kwa ujumla endapo....

Wewe ni shabiki wa marekani na sio mchambuzi. Mara ngapi Putin ameonya kutumia nguvu zaidi na wewe haujaongea chochote hapa Jf?? Ila baada ya Biden tu kuongea, wewe huyooo Jf..
 
Ni jamaa mmoja mwenye nguvu zake za kutosha na akili madhubuti aliyefanyiwa mobilization hapo Russia, tutegemee kumuona frontline akiwapiga waukraine dhaifu, waliojichokea na wenye nguvu visoda hivi karibuni Jbst
Haya mkuu nimeshakuelewa. Jamaa alieuliza kama hajakuelewa vizuri hapa basi tena.
 
Niwakati SASA wa jeshi la Marekan kumwajibisha putin
Nakubaliana na wewe kabisa, haiwezekani dunia ya leo nchi moja iivamie jirani yake na kuchukua sehemu ya ardhi na kutangaza kuwa ni mali yake, halafu mbaya zaidi dunia nzima na UN wanatazama tuu. Nduli Iddi Amini alituvamia na kutangaza kwamba sehemu ya mkoa wa Kagera sasa ni sehemu ya Uganda,kilichompata hata huko kaburini huwa anakikumbuka na kuwewesuka..
 
Umeandika kishabiki, hata hivo hakuna lolote watalo mfanya zaidi ya vikwazo ambavo hata wasio kuwamo wanaumia, kifupi wanamwogopa, hivi rusia ingekua moja ya nchi za afrika bado tungeendelea kujibishana hapa ,
Sawa Mrusi wa kwa mtogole..
 
Nasikia Putin siku hizi analala na begi lake la nguo pembeni, maana anajua muda wowote Mmarekani anakinukisha katika milango ya kuingilia nchini kwake.
Acha uongo, atakumbuka begi saa ngapi huenda anasahau hata kuvaa boxee
 
Shambulio la Sept 11 liliwezekanaje.??

Muliosomea kwenye mawe mnakazi kubwa kujua Dunia.

Russia knows what will happen. Na Sasa wamebadili move. Maeneo waliyojitwalia Yale manner au matano kama sikosei wame sign tayari Bunge lao lime approve. Hii sio Putin Tena. Jamani urusi sio Libya au Iraq.

It's like wamesitisha vita na Wana msubiri ukrane na wale wakujipachika wasimame. He is done na mapigano. Kilichobaki ni wananchi kusubiri baada ya referendum na utekelezaji. So sio vita ya Putin tena ni Yale majimbo ambayo yameondoa Ukraine..

Guys fuatilieni badala ya kusifia nani anapigwa nani anakimbia. Actually USA amepata sehemu ya kutest vitu vyake. Russia is not stupid. Na kuomba poo Russia si mjinga.

Nirudi kwenye Sept eleven...Jaman pale Washington panapigika tu tuache ushabiki. Na wakati wote USA anajitahidi Kremlin asioneshe kutaka kufanya jambo kama ya pentagon Ile ..


Leo Israel alikuwa akiendelea kujaribu dome nna linavyoweza kumzuia silaha za aduikuingia. Ni kama bakuli la kioo ukirusha Chochote kinazuiwa.
 
Swala la silaha za ulinzi hasa za maangamizi huwa haliongelewi hadharani mjomba. USA sio wajinga mpaka waitangazie dunia kila silaha waliyonayo na idadi yake.
Mfano wanaweza kuwa na ndege zisizo na rubani 100 ila watasema wana 10 ili kuihadaa dunia kuhusu maswala yake ya ulinzi.

Bora Urusi ishaonesha kwamba silaha ilizonazo zimekwama kuleta matokeo chanya ndio maana wanataka kutumia nuclear.
Ukiangalia nani ana nuclear war heads nyingi duniani, anajulikana. Tatizo mmelishwa propaganda. Kama marekani anaweza kumpiga mrusi peke yake, kwanini aungane na nchi 30 kwaajili ya kumkabili mrusi peke yake? Mwenye akili atajua ninaongelea nini hapa
 
Vita uisikie kwa mwenzako mkuu, hakuna mtu aliekuwa anategemea kuwa kuna siku kiongozi kama Putin angekuwa analala na viatu huku begi lake liko pembeni 🤣🤣🤣
Ni hatari sana mkuu 🤣🤣🤣
 
Wewe ni shabiki wa marekani na sio mchambuzi. Mara ngapi Putin ameonya kutumia nguvu zaidi na wewe haujaongea chochote hapa Jf?? Ila baada ya Biden tu kuongea, wewe huyooo Jf..
Amna mkuu, mimi naangalia athari kubwa itakazopata Urusi pale Marekani itapojibu wazi wazi kile kitachofanywa na Russia huko Ukraine.
 
Ni jamaa mmoja mwenye nguvu zake za kutosha na akili madhubuti aliyefanyiwa mobilization hapo Russia, tutegemee kumuona frontline akiwapiga waukraine dhaifu, waliojichokea na wenye nguvu visoda hivi karibuni Jbst
Mpaka Russia ilipoamua kuchukua vijana wa mitaani wakalisadie jesho vitani, ina maana huyo mwamba walikuwa hawajamuona mkuu?
 
Nakubaliana na wewe kabisa, haiwezekani dunia ya leo nchi moja iivamie jirani yake na kuchukua sehemu ya ardhi na kutangaza kuwa ni mali yake, halafu mbaya zaidi dunia nzima na UN wanatazama tuu. Nduli Iddi Amini alituvamia na kutangaza kwamba sehemu ya mkoa wa Kagera sasa ni sehemu ya Uganda,kilichompata hata huko kaburini huwa anakikumbuka na kuwewesuka..
Dawa ya Russia tayari iko jikoni inachemka. Ni swala la muda tu dunia itashangaa jamaa anavyoadabishwa na kuadhibiwa vilivyo.
 
Umeshaangalia zako movie za Yavuz mturuki anaebonga kiswahili basi unahisi kila kitu ni rahisi kama movie za waturuki
 
Za jioni ndugu zangu, kwema.

Ndugu wanajamii forum wenzangu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza clear kabisa hapo juu. Ni kwamba kuna mpango mahususi unapangwa wa kuiadabisha Russia (na kwa bahati mbaya sehem kubwa ya dunia ) kutokana na kiburi ilichonacho Russia dhidi ya mataifa makubwa na yenye nguvu kubwa duniani kama America na washirika wake.

Biden: "THE WORLD WOULD FACE 'ARMAGEDDON' IF PUTIN USES ATACTICAL NUCLEAR WEAPONS IN UKRAINE"

Kauli hii iliyotolewa na raisi wa Marekani mh Joe Biden sio ya kufanyiwa mzaha hata kidogo huko Kremlin. Ni kauli iliyobeba ujumbe mzito unaosubiri utekelezwaji wake muda wowote kuanzia sasa.

Joe Bide anachofanya ni kama vile kuiandaa dunia kisaikolojia ili atapokuja kumuadabisha Putin, Russia na baadhi ya maeneo ya dunia, awe na cha kujitetea kwamba 'tulionya mapema lkn Putin hakusikia, sasa haya ndio madhara ya kiburi chake na Russia yake, na kwamba lawama za uharibifu huu uliyofanywa na vikosi vyetu wakulaumiwa na Putin na genge lake'.

Kihistoria mara nyingi Marekani anapotaka kufanya jambo la kuishangaza dunia hasa lile lenye madhara makubwa kwa nchi au dunia, huanza kwanza kutoa onyo kwa nchi husika huku dunia nzima ikisia ili hapo baadae Marekani wasije kulaumiwa kwa lolote, na kwa vile yeye (Marekani) ndio mwenye nguvu basi linapotokea la kutokea huwa hakuna wa kuthubutu kujitokeza kuibebesha lawama akaeleweka.

Natamani kuona Putin anauelewa ujumbe huu wa Biden na kujiepusha na matumizi ya nuclear huko Ukraine kwani kinyume na matarajio yake, anaweza kuja kujikuta anaenda kuomba ukimbizi huko North Korea (maana mchina hatokubali kumpa hifadhi kwa kuhofia usalama wa nchi yake dhidi ya wababe hao wa dunia) kwahiyo Kiduku yeye atampokea tu maana hana cha kupoteza, huku nyuma atakuwa tayari kawaachia Wamarekani na wa Ukraine nchi yake wakiitawala Russia kwa miongo kadhaa ijayo.

Vita yake na bwana mdogo Ukraine imeshaonesha dunia kwamba Russia iko uchi kivita na kisilaha. Kwahiyo bora asitishe vita, arudishe majeshi yake nyumban, aombe radhi kwa uharibifu mkubwa aliofanya katika nchi ya mwenzake nk.
Mtu mzima akivuliwa nguo huchutama ili kulinda heshima yake.
Ila kwa taarifa Soo rasmi wanataka roho yake kwanza then vita itasimama na majadiliano yataendelea. Juz wamelipua sehem ya daraja Putin alisema likiguswa atatumia nuclear na wanazidi kumpush kwenye majimbo ameyaita ya Urusi. Na akasema mtu akigusa anampa nuke. Chakushangaa mpaka sasa hajarusha na jamaa wanapushi forward.
Kiufupi kauli ya mkuu wa usalama wa Taifa wa Russian sasa inatimia pale alimwambia tutumie zaid intelligence kuliko vita kamili. Upo uwezekano mkubwa CIA wakitumia watu wao ndani ya Urusi wamempa kama wrong information ili jamaa afikie ambition yake while akilirudisha nyuma Taifa miaka 100. Acha kabisa kitu kina itwa intelligence CIA
 
Back
Top Bottom