Kauli hii ya Kardinal Pengo,inatukumbusha "upande wa pili" wa Kanisa Katoliki

Hakika nimeamini hili jukwaa raia wapo vizuri ktk kuchambua mijadala inayoletwa hapa,big up[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Nenda TEC na Msimbazi miezi ya 5 6 tu 2016.

Halafu ni upumbavu kuanzia hoja kwa kumsingizia mtu na "porojo" baadae unadai ushahidi. Nimekupa ushahidi mpelekee Pengo na jpm.

Hii ni forum ya intelijensia porojo Lumumba.
 
Mkubwa hakoseagi..!

statement ya Polycarp Pengo hajaitoa kwa bahati mbaya.
 
Uliona ile kauli yake ilikua ni ya kuweka mjadala au ilikua"CONCLUSIVE",aisee matunda ya vatican nimeyakubali kabisaa.
 
Amesababisha mijadala kama huu tuufanyao hapa.
Sawasawa hata
* Lusekelo alisababisha Mijadala humu kwa ulevi wake.
*Gwajima alisababisha Mjadala humu kwa mahusiano yake na flora.
*Kuna Mapafri/askofu wamesababisha mijadala humu kwa scandal ya kulawiti watoto.
*Jana askofu Shoo amesababisha mijadala humu kwa kwa kusema hali huku uraini ni tete hakuna ajira.
So hakum mjadala wa maana Pengo aliouleta.
 
Nenda TEC na Msimbazi miezi ya 5 6 tu 2016.

Halafu ni upumbavu kuanzia hoja kwa kumsingizia mtu na "porojo" baadae unadai ushahidi. Nimekupa ushahidi mpelekee Pengo na jpm.

Hii ni forum ya intelijensia porojo Lumumba.

Aisee wewe ni jingalao, kwa taarifa yako pale TEC na Msimbazi ndiyo shughuli za kanisa hasa za jimbo kuu zinafanyikia na hata kanisa la tanzania kama kunahaja ya kukutana. Kwahiyo maeneo hayo kujaa siyo kwasababu ya matumizi ya serikali. Vilevile wakati wa mitihani ya bodi mfn PSPTB NA NBBA (kabla hawajajenga bunju) walikuwa wanafanyia mitihani pale hasa May na October na hii ni kwasababu pale TEC ndiyo sehemu unaweza kupata kumbi na malazi kwa wanaotoka mbali. Tatizo unaongozwa na siasa zilizojaa chuki dhidi ya Rais, Pengo na Kanisa kwa ujumla wake. HALAFU UNADHANI KILA MTU ANAYESEMA KINYUME NA WEWE NI MWANA LUMUMBA? JINGA KWELI
 
Matusi ni ushahidi wa kukosa hoja.

Lete orodha nzima ya mikutano ya miezi hiyo niliyokutajia kama mfano.

Siyo siri awamu hii na kanisa katoliki kupitia Pengo wamechemsha. Kama wewe huoni hivyo mimi nimekutaka ulete orodha ya mikutano ya miezi hiyo miwili kama mfano. Ukitaka na mengine utapewa ukijitia unajua sana mambo ya kanisa katoliki wengine tumo ndani. Ni kweli jpm anachukiwa sana kama hujui; ila kwa tunaomfahamu na magonjwa yake tuliwaonya tulisema na hatushangai na huu ni mwanzo tu.
 

Hivi mwenye kuleta ushahidi ni mimi au wewe uliyesema baada ya serikali kukataza mikutano ya taasisi za serikali kufanyika kwenye mahoteli, yalihamishiwa TEC na MSIMBAZI?, Nilikuomba utaje hata vikao viwili vilivyofanyika huko ukambwela, mimi najua misururu ya matukio yanayofanyika TEC na MSIMBAZI, unajidai uko ndani ya kanisa halafu hujui lolote unabishana hata na watu usiyowajua. Mimi c tu kwamba niko ndani ya kanisa ila kila mwezi hapo TEC na msimbazi centre sikosi kufika walau mara nne au tano. TEC naijua kiundani na kazi zake pamoja na vikao na utaratibu wake, wewe utabaki kuongea siasa uchwara na chuki zako kwa Rais pamoja na Pengo.UNADAI PENGO KUSEMA HELA HAZIJAPOTEA NI KOSA, KWANI WEWE MSHAHARA WAKO UMEPUNGUZWA BAADA YA JPM KUINGIA MADARAKANI?, KAMA ULIZOEA PESA ZA RUSHWA, SEMINA UCHWARA, 10%ZA MIRADI, KUHONGWA NA WEZI WA PESA ZA UMMA, SAFARI ZA HOVYO BASI KWELI PESA IMEPOTEA KWAKO.
 
Taratibu mkuu Blood of Jesus
Tujadili kwa staha
umenikumbusha kitabu nilichokisoma zamani kidogo: Priests and Politicians:The Mafias of the Soul!
Kimeandikwa na Osho!
Kitabu iki kinaongelewa "ndoa" ya Serikali na Kanisa ktk Kutawala Wananchi!
 
Ahsante
 
Mimi mwenyewe sijaamini kama kusema hivyo alikuwa amedhamiria,, inawezekana maneno yalimtoka bahati mbaya.. ila hata kipindi fulani maaskofu walitoa waraka juu ya katiba mpya, ila yeye akaja kupingana nao.. Mungu atusaidie sana..
Hapa kuna kitu nimejifunza!

"Mfumo"
 
Nchi ipo katika kipindi kigumu sana nani hatari sana kwa mtu credible kama yeye kuongea vitu km hivyo ila naamini hata mji wa mwizi waweza ibiwa pia vivyo hivyo hata viongozi wetu wa membalini na altare wanaweza pitiwa na shetani huko huko membalini na altareni kama waumini wengine wapitiwavyo na shetani
 
Haitoshi kumjibu ahsante badala ya kuleta mifano ya mikutano/semina za serikali zilizofanyika ktk hizo kumbi za kanisa katoliki, tuwekee na tarehe za tukio. Tuhuma nzito namna hii hazipaswi kujibiwa kwa jibu jepesi kama hilo. Lete mifano mitano tu. Vinginevyo utakuwa mtu mwongo, mropokaji na mchochezi hatari kabisa ktk taifa lenye mchanganyiko wa dini. Unachonganisha ili watu wakachome moto mali za kanisa katoliki sababu ya hasira?
 

umenikumbusha kitabu nilichokisoma zamani kidogo: Priests and Politicians:The Mafias of the Soul!
Kimeandikwa na Osho!
Kitabu iki kinaongelewa "ndoa" ya Serikali na Kanisa ktk Kutawala Wananchi!
Mkuu ongezea na hivi...Jaribu kuvitafuta;au nikipata wasaa huku nilipo nitakununulia ila uwe tayari tu "kurefund"....Ukisoma hivi,si tu utajielimisha,bali pia imani yako itakuwa,na hutaiegemeza kwa mtu(binadamu/Kiongozi wa dini).

Bali imani yako itaidumisha ktk Kanisa moja,katoliki la mitume...Ambalo lenyewe litaendelea kuwepo na hawa wengine watakuja na kupita.Maana tuliambiwa...Hili ndio Kanisa alilokabidhiwa Petro,na baadae akawaachia makhalifa wake,ambao ndio hao Mapapa...
 
Sibishani na wajinga kama mna uhakika siyo kweli na mimi nina uhakika ni kweli hatuna namna ya kuelewana. Halafu lugha za kishari zinawafaa nyinyi tu. Hamnipati na hambadirishi ukweli. Nina imani mnajua mnachokitetea. Na mimi siyumbi kwa nilichoshudia kwa macho yangu.
 
Mleta mada hii hakujikita ktk hoja za kwamba serikali inaipendelea kanisa katoliki ila kama nimemwelewa amejikita ktk kauli ya Kadinali Pengo jinsi inavyoweza kumsababishia Mh.Raisi akawa complacent kuhusu hali halisi ya kiuchumi au mzunguko wa fedha kwa watu wengi. Pia kumpa angalizo mheshimiwa Pengo kwamba kazi yake ya msingi ni kuwatetea wanyonge na kulinda kiimani au kiroho. Hapaswi kuitetea serikali kiasi cha kuipa upofu ikajisahau wajibu wake kwa umma hasa mambo ya kiuchumi(malazi, chakula, elimu) ambayo hutegemea hali ya uchumi wa mtu husika. Ila kwa hali iliyopo changamoto ni nyingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…