Kauli hii ya Wasira ni matokeo ya CCM kukataa tamaa na kuwa na hasira hivyo kuongea tu kutokana na frustrations

Kauli hii ya Wasira ni matokeo ya CCM kukataa tamaa na kuwa na hasira hivyo kuongea tu kutokana na frustrations

Hawa watu wamelaanika. Ndiyo maana kila siku wanafanya mambo ya kuzidi kumkasirisha Mungu na wanadamu!

Hawa ni sawa na yule mhandisi mkuu aliyesimamia utengenezaji wa meli kubwa zaidi na ya kifahari kuliko zote, meli ya titanic, alipoulizwa kuhusu asalama wa meli hiyo, kwa jeuri akasema kuwa eti kwa namna ilivyotengenezwa, hata Mungu hawezi Kuiangusha. Kilichotokea kila mmoja anajua, inaendelea kubakia kwenye records kuwa ajali mbaya ya meli kuliko zote zilizowahi kutokea.

Wasira na wajinga wengine wa CCM wameota kiburi na jeuri, hata kufikia kumkufuru Mungu, wasubiri, MUNGU atawaonesha walivyo wajinga.
Kweli kabisa mkuu, ni swala la muda tu. Wanatapatapa tu..
 
Kukataa tamaa like how ??
Unawezaje kukataa tamaa kwa hasira bosi ???

Manzi akipita unampiga jiwe au kisiasa Zaid mtu akikupa rushwa unamng'ata mkono ?
 
Nimeona clip ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mzee Wasira katika akaunti ya Godbless Lema kwenye mrandao wa X ambapo Wasira anasikika akisema maneno haya:

"CCM haitatoka madarakani mpaka Yesu arudi".

Msingi wa kauli hii na ile ya hivi karibuni ya Waziri Mchengerwa na nyinginezo za aina hii kutoka kwa viongozi wa CCM na Serikali, si za bahati mbaya, bali ni matokeo ya kukataa tamaa baada ya kuona umma umewakataa sasa wanaamua tu kuonyesha hasira na machungu yao.

Ukitaka kujua ana hasira na ana wivu wa kisiasa kwa wapinzani, anatumia neno "kibaka mmoja " katika kuhutubia wananchi bila shaka akimlenga Lissu ambae sasa yuko gerezani.

Kwa kifupi, wana hasira za kukataliwa na kuchokwa na makundi karibu yote katika jamiii na ndio maana sasa wameamua kubariki huu ukatili unaondelea waziwazi dhidi ya wapinzani(wako frustrated).

Bila kujua, wanatoa kauli za kuonyesha ni jinsi gani CHADEMA walivyo sahihi katika kudai REFORMS kabla ya uchaguzi.

Hakika Mungu fundi sana.
Kuna mengi nyuma ya matamko hayo ya Viongozi wa CCM.

Kwa mfano haiingi akilini kutokukemea vitendo vya watumishi wa vyombo vya Dola kutumia madaraka yao vibaya kama ilivyotokea pale Mahakama ya Kisutu
 
Ni kauli zinazoonyesha waz kuwa chadema wapo sahihi unaposema CCM haitoki madarakani mpaka yesu arudi maana yake hutegemei kushinda Kwa kura tuu Bali una njia nyingine unazitegemea katikat kushinda uchaguzi
 
Kuna mengi nyuma ya matamko hayo ya Viongozi wa CCM.

Kwa mfano haiingi akilini kutokukemea vitendo vya watumishi wa vyombo vya Dola kutumia madaraka yao vibaya kama ilivyotokea pale Mahakama ya Kisutu
Kama haitoshi, saa hizi tunaarifiwa na John Heche kupitia mtandao wa X kuwa usiku wa kuamkia leo Polisi wamezingira nyumba yake na ya Tundu Lissu.
 
Hivi unaziona tofauti kubwa zilizopo kati ya Makamu huyu (Wasira); na yule aliye omba kustaafu (Abdulrahman Kinana)?
Hata katika lugha tu, kuna tofauti kubwa sana.
Huyu Wasira hana mbinu za kushawishi kwa hoja kama alivyokuwa Kinana. Huyu kakaa kishari shari tuu, na kijambazi. Huyu anaweza kukutoa roho waziwazi wakati Kinana anakumaliza huku ukitabasamu.
Mimi ningekuwa wasira wala nisingekikubali hiki cheo tena ktka kipindi hiki kigumu CCM wanataka tu kumuua mzee wa watu majukwaani
 
Mimi ningekuwa wasira wala nisingekikubali hiki cheo tena ktka kipindi hiki kigumu CCM wanataka tu kumuua mzee wa watu majukwaani
Kwanza wamempa kazi ambayo haiwezi; halafu kazi itakayo mwondolea heshima yake yote aliyo jijengea kisiasa wakati wa uhai wake.
Sasa sijui yeye anataka kitu gani katika hatua hii ya maisha yake.
 
Back
Top Bottom