Nilikuwa sehemu fulani naangalia mechi kati ya Yanga na Namungo, baada ya mechi kuisha kwa Yanga kupata ushindi wa goli moja, mashabiki kadhaa wa Simba wakawa wanashangilia kwa nguvu wanadai Yanga imeshinda kwa ushindi wa goli moja na siyo 5 kama ilivyo kawaida π π π
Nataka niwakumbushe kuwa mpira una matokeo ya aina tatu 1.kushinda 2.kushindwa na sare/suluhu
Vilevile kila timu huwa inajiandaa kupata ushindi, so hakuna mteremko,
Nb. aliyewaita mbumbumbu aliona mbali sana.