Kauli, matamko ya Rais Samia yaliyoleta umoja na utulivu wa nchi

Kauli, matamko ya Rais Samia yaliyoleta umoja na utulivu wa nchi

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,207
Reaction score
17,674
Amani iwe nanyi,

Kuna kauli mbalimbali ambazo zilitolewa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan zilizopelekea Watanzania kuwa wamoja zaidi na kuifanya nchi kutulia mara baada ya msiba mzito wa kuondokewa na rais Magufuli.

Binafsi ninazo kauli mbili ,kama na wewe unazo weka hapa.

1. Mimi na Magufuli ni kitu kimoja

Ikumbukwe mara baada ya kufariki rais Magufuli liliibuka kundi likiongozwa na Tundu Lissu na Lema likawa linashangilia kifo hicho, hali hiyo ilienea hadi kwa baadhi ya wabunge kama Nape na Makamba, badala ya kujadili bajeti wakawa wanajadili nani ni zaidi kati ya Magufuli na Samia!

Hali hiyo iliwakera sana wazalendo wa nchi yetu na rasmi likaibuka kundi jingine lililobatizwa jina la walinda legacy ya Magufuli, moja ya watu wa kundi hili waliojitokeza hadharani kukemea ni mbunge Lusinde, pia Lazaro Nyalandu aliyekuwa kada wa Chadema alikemea hadharani na kutangaza kuachana na Chadema kwa kitendo chao cha kumtukana alipohudhuria msiba Chato.

Katikati ya mvurugano huo aliibuka rais Samia na kuwachana live Wabunge na Chadema kwa ujumla kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja na serikali yake ya awamu ya sita haijatokana na uchaguzi mbali imetokana yeye Samia kuaminiwa na hayati Magufuli na kufanywa kuwa makamu wa rais.

Kauli hii ya Samia ililifanya kundi la walinda Legacy kuibuka kidedea dhidi ya kundi la washangilia kifo hivyo nchi kutulia.

2. Wala rushwa, wazembe majambazi na mafisadi kuendelea kubanwa
Rais Samia alitangaza hadharani kwamba katika masuala ya rushwa atasimama imara na akamtumbua mkurugenzi wa bandari na kuagiza Takukuru wafanye uchunguzi BOT na wizara ya fedha. Pia kuwajibisha wote waliojaribu kuchezea mifumo ya Tanesco, TRA na bandari.

Hatua hizi zilifanya nchi kutulia kwa sababu watanzania wengi waliona rasilimali zao bado ziko salama kama ilivyokuwa wakati wa awamu ya tano chini ya hayati Magufuli.
 
No 1 Chadema haina wabunge hadi sasa nikusahihishe
 
Kutoka kumtegemea Mungu wa Mbinguni mpaka kutegemea barakoa na chanjo, ndipo alipotufikisha kama Taifa. Hachanjwi mtu hapa! Ndio.!!

Kama ambavyo tulifanikiwa kuhepa sharti la chanjo ya Homa ya Manjano mbinu hizi hizi zitatumika kwenye corona. Mawakala wampinga Kristo kazini.
 
Chanjo ni hiari sio lzm, corona ilikuja kuchukua watu wake ishaondoka na ondoa hofu chapa kazi
 
Kutoka kumtegemea Mungu wa Mbinguni mpaka kutegemea barakoa na chanjo, ndipo alipotufikisha kama Taifa. Hachanjwi mtu hapa! Ndio.!!

Kama ambavyo tulifanikiwa kuhepa sharti la chanjo ya Homa ya Manjano mbinu hizi hizi zitatumika kwenye corona. Mawakala wampinga Kristo kazini.

Kwahiyo ukimtegemea Mungu hutakiwi kuchukua hata tahadhari?
 
Kwahiyo ukimtegemea Mungu hutakiwi kuchukua hata tahadhari?

Hakuna cha tahadhari hapa wanatulazimiashia kutupiga chapa ya mpinga Kristo sisi Wakristo ili tuishie jehanamu kama wengine.
 
Hakuna cha tahadhari hapa wanatulazimiashia kutupiga chapa ya mpinga Kristo sisi Wakristo ili tuishie jehanamu kama wengine.

Mpinga Kristo unamjua wewe au unaongea tu.
 
Mmeshamaliza mkutano wenu!
Kumbe nae ni miongoni mwao?
Mbona hajasema na matendo ya mama yanazidi kufanya nchi itulie kwa sheria kufuata mkondo wake... maana wale waliokuwa juu ya sheria na hawakugusika... wakijikweza na kuumiza raia wasio na hatia msumeno sasa unaanza kukata...
 
Hakuna cha tahadhari hapa wanatulazimiashia kutupiga chapa ya mpinga Kristo sisi Wakristo ili tuishie jehanamu kama wengine.
Mbona watafuta pesa? Mbona una chanjo za ndui, manjano, tb na bado wajisahaulisha kwamba ulishapigwa chapa???
 
Hakuna cha tahadhari hapa wanatulazimiashia kutupiga chapa ya mpinga Kristo sisi Wakristo ili tuishie jehanamu kama wengine.
Unasahau kuwa hata huyo Kristo ni hawa hawa wanaotuletea chanjo ndio walituletea. Unajua kama kina Pope Francis na ma don wote wa ukristu wameshachanjwa?
 
Mbona watafuta pesa? Mbona una chanjo za ndui, manjano, tb na bado wajisahaulisha kwamba ulishapigwa chapa???

Mambo ya Kiroho haya. Ndui ilikuwepo miaka maelfu ulisikia wapi Mkristu yeyote akisema chanjo ya ndui ni chapa ya mpinga Kristo. Hujui kuwa ili usafiri safari za kimataifa lazima uwe na cheti cha chanjo ya homa ya manjano? Ulishasikia chanjo hiyo ikitwa ni chapa ya mpingi Kristo. Kwa nini corona?
 
Back
Top Bottom