Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapa jukwaani.

Ndugu zangu kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Wakati raisi Samia alipoingia madarakani, haikupita hata miezi sita akaanza pangua pangua ya viongozi wakubwa pale ikulu akiwemo aliekuwa katibu mkuu kiongozi mhe Dr Bashiru ambae alikuwa amechukua nafasi hiyo muda mfupi tu baada ya aliekuwepo kufariki.

Wengi walianza kulalamika na kumlaumu Rais kwa hatua yake hiyo ya pangua pangua pale state house, mpaka wengine wakafikia hatua ya kusema kuwa raisi ana ugomvi sijui na sukuma gang, team Magufuli nk. Ila nyuma ya pazia hawakuwa wanajua ni kwanini raisi aliamua kufanya vile na kwa sababu gani.

Cheo cha katibu mkuu kiongozi ni cheo kikubwa sana kimamlaka, hivyo sio rahisi kuondolewa tu hivi hivi kienyeji bila kuwa na sababu ya msingi. Hivyo raisi kumuondoa mhe Bashiru katika nafasi ile ghafla bin vuu kulikuwa na sababu maalumu ambayo wengi hawakuijua.

Leo hii ukisikiliza kwa makini ile interview ya CDF mstaafu mhe Mabeyo, na kile kilichotokea baada ya mama kuingia (pangua pangua) utaona kabisa ni kina nani ambao walikuwa na mpango wa kupindisha katiba. Nakumbuka CDF Mabeyo wakati wa hotuba yake pale msibani alimwambia mhe raisi kuwa ana ujumbe wake ambao atamwambia pindi watapokuwa falagha kati yake na raisi.

Miezi kadhaa mbele baada ya msiba kuisha Rais Samia akaanza pangua pangua ambayo ilipelekea mhe Bashiru kuwa miongoni mwa waliotenguliwa, huku waziri mkuu na mawaziri wengine wakiendelea kubaki na vyeo vyao hadi leo.

So Rais anapotengua au kutea mtu huwa anafanya hivyo baada ya kupata taarifa za kutosha za anaeteuliwa au tenguliwa.

Leo niishie hapa.
Hakuna mahala cdf amesema Kuna watu walitaka rais Samia asiapishwe, Bali alisema kulikuwa na mvutano wa wakati Gani aapishwe eidha baada au kabla ya mazishi,

Acha unafiki
 
CCM uwe na ushawishi au usiwe na ushawishi utashinda tu mchana kweupe.
Na ndomaana wapinzani hudai kuwa CCM huwa inashirikiana na tume ya uchaguzi kushinda chaguzi zote.
 
..swali langu ni kwanini Mabeyo hakuwa akimpa taarifa Makamu wa Raisi / Kaimu Raisi.

..kwanini aliwataarifu Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi kabla ya Makamu wa Rais ambaye kwa hali ya kiafya ya Rais alikuwa / alipaswa kuwa KAIMU RAISI?

..Suala la maradhi na kuugua kwa Raisi Magufuli ilikuwa ni jambo linalotakiwa kusimamiwa na Makamu wake.
Makamu wa Rais alikuwa hafuatilii kwa karibu Afya ya Rais mpaka asubiri kuambiwa???
 
Hakuna mahala cdf amesema Kuna watu walitaka rais Samia asiapishwe, Bali alisema kulikuwa na mvutano wa wakati Gani aapishwe eidha baada au kabla ya mazishi,

Acha unafiki
Wewe umeandika kwa kuchagua kwamba nini uandike na kwa niaba ya nani. So itakuwa ngumu kukuelewesha ukaelewa. Jaribu kusoma comment za watu mbali mbali humu walioelewa naamini na wewe utaelewa.
 
Makamu wa Rais alikuwa hafuatilii kwa karibu Afya ya Rais mpaka asubiri kuambiwa???

..Wakuu wa vyombo waliokuwa eneo la tukio ndio waliowajibika kumpa taarifa Makamu wa Rais.

..Pia kwasababu Rais alikuwa mahututi, hawezi kutekeleza majukumu yake, Makamu wa Rais alipaswa KUKAIMU nafasi ya Rais.

..Katika mazingira yaliyokuwepo vyombo vyote vilipaswa kuwa vinaripoti kwa Samia mpaka pale hali ya Magufuli ingetengemaa na kurudi ktk nafasi yake.
 
Nawafahamu CDFs wote mkuu ila kustaafu kwa Mabeyo kuliibua maswali kadhaa kwa waliokuwa wanajua kinachoendelea, ila mwisho wa siku Jibu likawa tu "amestaafu kwa mujibu wa sheria", na wengi kama wewe waliamini kuwa kweli Mabeyo alistaafu kwa mujibu wa sheria, hivyo nilitegemea comment kama hii wala sishangai, ila acha ibaki hivyo hivyo mkuu
Acha uzwazwa,Mabeyo muda wake ulishafika tamati.
 
Magufuli hakuwa Mtu wa kumuamini kiongozi wake Kwa uharaka, NI dhahiri Kwa wakati ule makamu hakuwa na power yoyte zaidi ya cheo chake cha umakamu
Kwamba mara zote Magufuli alilazimishwa Samia awe makamu wake au? Yaani Magufuli huyu wa 2020 alikuwa akiogopa watu kiasi apangiwe makamu? Samia was the perfect person kwa umakamu na so far ni best president ever kuwa naye.

By the way, tangu 1995, kuna makamu gani aliyeheshimiwa na kupewa hadhi ya umakamu hasa? Ulikuwa wapi wakati Dr. Omar, Shein, Bilal wanatembea na mikasi tu?
 
Je, MABEYO AMESEMA YOTE JUU YA NI NINI KILIMSIBU RAIS MAGUFULI KABLA HAJAFA?

'Kisha, baada ya miaka mitatu, nilipanda kwenda Yerusalemu, ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano' - Mtume Paulo (Wagalatia 1:18).

Katika kitabu chake kiitwacho 'Paul and Peter Meeting in Jerusalem', Askofu Prof. Kenneth Cragg wa Church of England alifafanua mstari huo katika kurasa 96. Katika kitabu hicho, Prof. Cragg alijaribu kujibu swali hili: Je, katika siku hizo 15, Kefa (Mtume Petro) na Mtume Paulo waliongea nini? Lakini hoja kwa nini maudhui ya maongezi hayapo katika kitabu cho chote cha Paulo haijajibiwa na Prof. Cragg. Hii ndio sehemu ya utafiti ambao Askofu Mwamakula amekuwa akifikiria kuufanya baadaye.

Wakati Askofu akiwaza hayo, Mkuu wa Majeshi mstaafu wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo aliibuka na kuongea na vyombo vya habari kuhusu kifo cha Rais Magufuli tarehe 17 Machi 2021. Jenerali Mabeyo alitumia muda mfupi (pengine saa 1) kuongea na wanahabari juu ya nini kilitokea kwa Rais Magufuli ndani ya kipindi cha masaa 24 kuanzia kati ya tarehe 16 na 17 Machi 2021.

Jenerali Mabeyo ameacha maswali mengi kwa watu ambayo pengine pia yatahitaji kujibiwa na waandishi wa habari za uchunguzi, watafiti na hata wana usalama katika miaka mingi ijayo. Baadhi ya maswali ni: Je, kwa nini katika saa za mwisho za maisha yake hapa duniani, Rais Magufuli hakuruhusiwa kuwa na familia yake - mke au watoto? Je, ni kitu gani kilichelewesha kuapishwa kwa Makamu wa Rais kuwa Rais hadi baada ya siku mbili badala ya masaa 24?

Je, kwa nini taarifa za msiba asipewe kwanza Makamu wa Rais, badala yake wakapata Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi? Je, kule Tanga alikokuwa Makamu wa Rais na kule Dodoma walikokuwa hao wengine wapi ndio karibu? Je, kulikuwa na 'mzozo' wa kutaka aapishwe mtu mwingine badala ya Makamu wa Rais? Je, huo 'mzozo' kama ulikuwepo na pengine kupelekea kuchelewesha kuapa, ulianzishwa na nani? Je, nani aliyekuwa anakusudiwa kuapa badala ya Makamu wa Rais?

Je, kuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya juu miongoni mwa aliowasema Mabeyo ambaye angeweza kusahau katiba inasema nini juu ya lililotokea wakati alikuwa ameapa kuilinda? Je, maelezo ya msemaji wa familia wakati ule wa msiba na maelezo ya Jenerali Mabeyo kuhusu sala ya mwisho kwa namna gani yanalingana na kwa namna gani yanatofautiana? Kama ipo tofauti, ni makusudi au nahati mbaya? Je, kama kuna tofauti, umma ufuate maelezo ya nani? Je, zile siku kadhaa kabla ya kifo chake (kipindi cha ikimya), Rais alikuwa wapi? Je, alitoa wosia au maelekezo gani? Kama aliweza kutoa amri kutaka arejeshwe nyumbani wakati amezidiwa, alishindwaje kutoa amri ya kutaka familia yake?

Ili kuyajibu maswali yote hayo itahitajika utafiti utakaotoa maelezo ya kutosha kuandika kitabu chenye kurasa 2000. Kuishi na watu wa aina ya Askofu Mwamakula inahitaji uvumilivu mwingi. Ukuikosa uvumilivu unaweza kumtumbukiza katika pipa la tindikali ili kumbukumbu ya mwili wake isiwepo, asipelekwe Itunge katika Isyeto (makaburi) la Chifu Mwamakula. Maswali yake hufanya watu waanze kufikiria kinachofanyika katika 'Sayari ya Mirithi'!

Kama Jenerali Mabeyo, angenyamaza kimya, Mwamakula angekuja na maswali yake haya ya 'kipumbavu'? Je, ni kwa nini watu husema chini chini wakijiuliza maswali kama hayo? Je, watu wanaogopa nini kuyajadili wakati Jenerali pia Mabeyo ameamua kufunua pipa jalalani? Hivi mtu akilifunua pipa jalalani, utawezaje kulaumu na kuwaadhibu kuku wanaochakura wadudu?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 18 Machi 2024; saa 12:25 jioni
FB_IMG_1710800798231.jpg
 
Back
Top Bottom