Kindeena
JF-Expert Member
- Sep 27, 2017
- 11,462
- 21,124
KATIBANani sasa alimwambia kuwa makamu ndiyo anastahili kutangaza kifo Cha Rais?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
KATIBANani sasa alimwambia kuwa makamu ndiyo anastahili kutangaza kifo Cha Rais?
Kwani siasa ina rafiki?Kwanini usimuamini mtu uliemteuwa mwenyewe kuwa mgombea mwenza wako?
Hauna hoja.
Hakuna mahala cdf amesema Kuna watu walitaka rais Samia asiapishwe, Bali alisema kulikuwa na mvutano wa wakati Gani aapishwe eidha baada au kabla ya mazishi,Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapa jukwaani.
Ndugu zangu kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Wakati raisi Samia alipoingia madarakani, haikupita hata miezi sita akaanza pangua pangua ya viongozi wakubwa pale ikulu akiwemo aliekuwa katibu mkuu kiongozi mhe Dr Bashiru ambae alikuwa amechukua nafasi hiyo muda mfupi tu baada ya aliekuwepo kufariki.
Wengi walianza kulalamika na kumlaumu Rais kwa hatua yake hiyo ya pangua pangua pale state house, mpaka wengine wakafikia hatua ya kusema kuwa raisi ana ugomvi sijui na sukuma gang, team Magufuli nk. Ila nyuma ya pazia hawakuwa wanajua ni kwanini raisi aliamua kufanya vile na kwa sababu gani.
Cheo cha katibu mkuu kiongozi ni cheo kikubwa sana kimamlaka, hivyo sio rahisi kuondolewa tu hivi hivi kienyeji bila kuwa na sababu ya msingi. Hivyo raisi kumuondoa mhe Bashiru katika nafasi ile ghafla bin vuu kulikuwa na sababu maalumu ambayo wengi hawakuijua.
Leo hii ukisikiliza kwa makini ile interview ya CDF mstaafu mhe Mabeyo, na kile kilichotokea baada ya mama kuingia (pangua pangua) utaona kabisa ni kina nani ambao walikuwa na mpango wa kupindisha katiba. Nakumbuka CDF Mabeyo wakati wa hotuba yake pale msibani alimwambia mhe raisi kuwa ana ujumbe wake ambao atamwambia pindi watapokuwa falagha kati yake na raisi.
Miezi kadhaa mbele baada ya msiba kuisha Rais Samia akaanza pangua pangua ambayo ilipelekea mhe Bashiru kuwa miongoni mwa waliotenguliwa, huku waziri mkuu na mawaziri wengine wakiendelea kubaki na vyeo vyao hadi leo.
So Rais anapotengua au kutea mtu huwa anafanya hivyo baada ya kupata taarifa za kutosha za anaeteuliwa au tenguliwa.
Leo niishie hapa.
Kuhakikisha hawashiki madaraka au nafasi yoyote ya utumishi wa ummaIngekuwa wewe ndo raisi ungewachukulia hatua gani?
Hahaha jamaa anakwambia "wahusika". Lakini ameshindwa kuweka wazi kuwa hao "wahusika" ni kina nani, na wanavyeo gani katika nchi.Kipande hiki chote ni maneno ya hisia, tuhuma na kuokoteza tu.
Weka ushahidi japo kidogo umetoa wapi n.k.
Makamu wa Rais alikuwa hafuatilii kwa karibu Afya ya Rais mpaka asubiri kuambiwa???..swali langu ni kwanini Mabeyo hakuwa akimpa taarifa Makamu wa Raisi / Kaimu Raisi.
..kwanini aliwataarifu Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi kabla ya Makamu wa Rais ambaye kwa hali ya kiafya ya Rais alikuwa / alipaswa kuwa KAIMU RAISI?
..Suala la maradhi na kuugua kwa Raisi Magufuli ilikuwa ni jambo linalotakiwa kusimamiwa na Makamu wake.
Wewe umeandika kwa kuchagua kwamba nini uandike na kwa niaba ya nani. So itakuwa ngumu kukuelewesha ukaelewa. Jaribu kusoma comment za watu mbali mbali humu walioelewa naamini na wewe utaelewa.Hakuna mahala cdf amesema Kuna watu walitaka rais Samia asiapishwe, Bali alisema kulikuwa na mvutano wa wakati Gani aapishwe eidha baada au kabla ya mazishi,
Acha unafiki
Makamu wa Rais alikuwa hafuatilii kwa karibu Afya ya Rais mpaka asubiri kuambiwa???
Sasa bila kuambiwa atajuaje? Au unafikiri yeye ni malaika, hata akiwa Mwanza anaweza kuona yanayofanyika Dodoma?Makamu wa Rais alikuwa hafuatilii kwa karibu Afya ya Rais mpaka asubiri kuambiwa???
Kwa maelezo ya CDF mstaafu, ni hivyo!Wataka kusema Sa100 alikwenda Tanga na kukaa kule bila kufahamu kinoendelea?
Kwa maelezo ya CDF mstaafu, ni hivyo!
Hapo lazima akwepe kukupa jibu linaloeleweka. Hakuna mtu ambae anaweza kuzifungua hizi kodi moja kwa moja.Oh kumbe former kitengo na yeye muhusika. Mkuu inaonekana una inform za kutosha kuhusu genge hili.
Acha uzwazwa,Mabeyo muda wake ulishafika tamati.Nawafahamu CDFs wote mkuu ila kustaafu kwa Mabeyo kuliibua maswali kadhaa kwa waliokuwa wanajua kinachoendelea, ila mwisho wa siku Jibu likawa tu "amestaafu kwa mujibu wa sheria", na wengi kama wewe waliamini kuwa kweli Mabeyo alistaafu kwa mujibu wa sheria, hivyo nilitegemea comment kama hii wala sishangai, ila acha ibaki hivyo hivyo mkuu
Kwamba mara zote Magufuli alilazimishwa Samia awe makamu wake au? Yaani Magufuli huyu wa 2020 alikuwa akiogopa watu kiasi apangiwe makamu? Samia was the perfect person kwa umakamu na so far ni best president ever kuwa naye.Magufuli hakuwa Mtu wa kumuamini kiongozi wake Kwa uharaka, NI dhahiri Kwa wakati ule makamu hakuwa na power yoyte zaidi ya cheo chake cha umakamu
Sahihi ingawa mjadala hauoneshi kuwa kulikuwa na shida katika kuielewa katiba inasemaje bali kundi la watu kutaka kupindisha katiba kwa mgongo wa jinsia au uzanzibari wake. Hii ndo shida.Exactly!
Safari ijayo ikitokea hivyo tena halafu bado kukawa na makosa, hapo hakutakuwa na excuse yoyote ile tena!