Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Je, kulikuwa na 'mzozo' wa kutaka aapishwe mtu mwingine badala ya Makamu wa Rais? Je, huo 'mzozo' kama ulikuwepo na pengine kupelekea kuchelewesha kuapa, ulianzishwa na nani? Je, nani aliyekuwa anakusudiwa kuapa badala ya Makamu wa Rais?
Pitia top profile iliyopururwa kwa mizengwe ya kimtindo labda utapa majibu mkuu.
 
Kwani kwa mujibu wa Katiba, ni CDF ndiye mwenye wajibu wa kufanya hivi? Je kuugua kwa JPM kuliwekwa bayana? Kama hakukuwekwa bayana, ni mazingira gani yangewezesha kumtangaza Samia kama Kaimu Rais?
 
Samia she's misfit to the position.Dhaifu mno,hatoshi.
 
Umewaza na kumjibu vile vile kama nilivyomjibu mimi huko juu. Hawa vijana wengi hawakuwepo hiyo 1995, wala 2000.

Wamezaliwa na kukulia katika kipindi hiki cha siasa za majitaka, hivyo usishangae mtu kuja na habari za hovyo dhidi ya raisi Samia akiwa raisi na kabla hajawa raisi.
 
Maswali ni mengi na mazito, lakini yanahitaji ujuzi, ueledi na ufahamu mzuri kuyajibu. Let's wait wenye sifa za ujuzi, ueledi na ufahamu mzuri waje wayajibu. Hata kama sio leo basi kesho, keshokutwa na kuendelea...
 
Mabeyo hana lawama hapa
 
Viongozi wengi kuanzia state house hadi mjengoni hawajui katiba.Wanajua kutumia mabavu tuu.Hivi kiongozi mkubwa anaposema KATIBA NI MAKARATASI, Unaona ni jinsi gani tulivyo na viongozi wakubwa wasioijua katiba au wasioiheshimu katiba yetu.
 
Hii itakuwa igp hakutaka samia awe na rais
Na mimi nimegundua alikuwa sawa shida katiba

Lakini ukweli hafai kabisa, asante cdf
 
Baada tu ya Magufuli kufariki, mambo hayakuwa rahisi kama unvyofikiri.
Kina Bashiru, wanaohisiwa kuwa hata siyo wazawa wa nchi hii, walikuwa wametanda uongozini nchini.
Uraia wa magufuli wenyewe tatizo.
Baba yake unamfahamu?
 
Watumishi wengi wa uma hawajui na wala hawatendi kwa mujibu wa katiba na sheria (kuanzia chini hadi Rais). Husikiliza matakwa ya Rais au upepo wa siasa za ndani na nje.
Hii ndiyo changamoto kubwa. Tunatakiwa kujenga fikra za wananchi kuhoji na kuwashighulikia wale wote wasiofuata katiba na sheria.
 
Kwann jpm alimuita cdf badala ya makamu? Mjue mam alikuwa na shida
Nafikiri wewe haukufuatilia kwa makini yale mahojiano ya cdf.

Ni kwamba cdf yeye hakuitwa, bali alikuwa pamoja na mgonjwa muda wote kama mwenyekiti wa vyombo vya ulinzi na usalama akishirikiana na igp pamoja na mkuu wa kitendo cha wavaa suti. Wakati huo makamu yeye alikuwa ziarani kikazi huko Tanga.

Hivyo raisi alimtumia Mabeyo kama mwenyekiti wa vyombo vya usalama pale hospital kumpa maelezo yote ili na yeye ayafikishe sehemu husika. Ni kama vile mzazi akilazwa hospital, inapotokea dharura fulan basi mtoto au mtu aliekaribu na mgonjwa ndo hupewa maelezo ya nini kifanyike kwa muda huo.
 
Kwani wakati wa JPM vyombo vya kijeshi si ndio aliviweka mbele zaidi ilikuwa sawa kwa wakati huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…