Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Kauli ya CDF mstaafu kuhusu waliotaka kupindisha katiba ili Rais Samia asiapishwe inanipa picha halisi ya kwanini Bashiru na wenzake walitenguliwa

Sababu mojawapo nimeshaizungumzia pale kwenye comment yangu ya kwanza mkuu, it is up to you to take it or leave it, Mabeyo alitumia sababu ile ile ya siku zote na utaratibu ule ule wa ma CDF kustaafu

Lakini nyuma ya pazia hiyo haikuwa sababu kubwa, 'Wahusika' wanadai yeye na Magufuli walishapanga mwaka atakaostaafu, (endapo angeendelea kuwa hai) ambapo haikutakiwa kuwa 2022

Na CDF mpya alikuwa ameshaandaliwa Major General Charles Mbuge, ambaye naye alikuwa ni pro Magufuli, ndio maana kustaafu kwa Mabeyo kuliibua maswali kwa waliokuwa wanajua kinachoendelea
Naona ni maneno tu yasiyo na uthibitisho wowote ule.

Haina shida, hata hivyo. Ni haki ya watu kusema, iwe uzushi au la!
 
Mkuu kama ulimsoma katikati ya mistari ya kauli zake utaona mjadala ulikuwa unafanya kwingine yeye Mabeyo anafanya maamuzi kwa manufaa ya Taifa!

..kosa la Mabeyo ni kutokumpa taarifa Makamu wa Rais.

..Rais anapokuwa hawezi kutimiza majukumu yake iwe kwa ugonjwa au sababu nyingine Makamu anatakiwa kuziba pengo lililojitokeza.

..hiyo " mijadala " isingekuwepo kama Mabeyo angefuata na kuheshimu katiba tangu awali.
 
Yale mahojiano pengine yamefanywa kwa wema ila yameniacha na maswali mengi sana juu ya uongozi wa nchi yetu na hatma ya Katiba yetu.

Ina maana wakati wote wa ugonjwa hadi rais hawezi tena kuongea, nani alikuwa anaongoza nchi?
Hapo ndiyo ujue nchi yetu inawezesha kujiendesha yenyewe hata ikiwa na viongozi war-tar-two.
 
Naona ni maneno tu yasiyo na uthibitisho wowote ule.

Haina shida, hata hivyo. Ni haki ya watu kusema, iwe uzushi au la!

Misiba ya mwaka huu ya Lowassa na Mwinyi imenifanya nifuatilie maongezi ya Watanzania wengi mitandaoni na kuthibitisha zaidi hofu yangu moja.

Watanzania wengi wanapenda maneno ya uzushiuzushi, ya majungumajungu, ya kuokotezaokoteza.

Wengi wao ni watu unaoweza kuwaanzishia conspiracy theory wanayoioenda tu, mfano dhidi ya viongozi, wakaunga mkono bila hata kuhoji premise yenyewe.

Kwa sababu hawawezi majibizano ya kimantiki, yaliyo fact based, yanayoweza kufanyiwa verification.

Wanakubaki maneno yasiyo na source wala uthibitisho. Mradi unashambukia wasiyemoenda tu.

Sijui ni kitokana na kuishi katika jamii ambayo haitoi habari rasmi au nini.

Hali hii inaleta sintofahamu kubwa.

Maneno mengine ni ya kweli na hayatolewi rasmi, au yanachelewa sana kutolewa rasmi. Nimeangalia digital archive ya Dr. Salim Ahmed Salim, kuna vitu kibao vya 1960's na 1970's huko ambavyo leo havina umuhimu wa kuwa classified, lakini vilikuwa classified mpaka archive hii inaanzishwa.

Watu wetu wengi nao wana hasira na serikali, lakini hawajui kui critique kwa hoja na mantiki.

Mwisho wake unasikia habari ambazo zingekuwa za kuchekesha kama
si za kusikitisha.

Ndiyo hapo unaambiwa wale wauza madafu Ikulu ni watu wa usalama wa taifa. Hiyo nayo inakuwa story ya kushika watu akili.Au Rais Ali Hassan Mwinyi akiacha wosia azikwe Mkuranga, lakini mwanawe Hussein kamzika Zanzibar kisiasa, au Lowassa alitumwa kwenda CHADEMA kuvuruga upinzani tu.

Totally bonkers stories, kama vile tuna ukame wa scandals legitimate za hawa viongozi.
 
Nimewahi kusema tena humu, kwasababu ya ubinafsi wa watu wanaoteuliwa kugombea urais hasa ndani ya CCM, huwa wamekuwa na utaratibu wa kuteua wagombea wenza wenye ushawishi mdogo ndani ya chama na hata kwa wananchi.

Kwa lugha nyepesi ni kwamba, marais wamekuwa wakipenda makamu wa rais ambao hawawezi kuwafunika. Si unaona hata Rais wa sasa alimteua mtu gani kuwa makamu wake?

Upatikanaji wa makamu wa rais unapaswa kuzingatia kwamba, huyu mtu muda wowote anaweza kuwa Rais wa nchi!
Labda hofu kwamba itakuwa sawa na kusaini kifo chake mwenyewe?
 
Kuna kitabu kinaandikwa juu ya haya!?
Sielezei kuwa kuna kitabu kinaandikwa, nasema kuwa kikiandikwa tutashangaa mengi.

Haya mambo yote yatakuja kujulikana, si unaona wanazidi kujifungua kila muda unavyokwenda?

Hawa wazee wengine wakifikia karibu na kufa wanafunguka na kuweka mambo wazi.

Wakati tunafumua mambo ya EPA mitandaoni, nani alijua kwamba Mkapa atakubali kwamba walipiga pesa za EPA? Lakini kakubali, kaandika kwenye kitabu chake.
 
..kosa la Mabeyo ni kutokumpa taarifa Makamu wa Rais.

..Rais anapokuwa hawezi kutimiza majukumu yake iwe kwa ugonjwa au sababu nyingine Makamu anatakiwa kuziba pengo lililojitokeza.

..hiyo " mijadala " isingekuwepo kama Mabeyo angefuata na kuheshimu katiba tangu awali.

Hii issue ina mambo mengi sana ambayo hayajawekwa wazi.

Hata Mabeyo mwenyewe kuna mengi bado hajaweka wazi.

Hapa kama anatuonjesha zile habari "declassified" tu, zile nyeti kabisa ambazo bado ziko classified anaziacha.

Hiyo amri ya kumtenga Makamu wa Rais inaonekana kuwa ilitoka kwa Rais mwenyewe.

Haiwezekani Rais atake Makamu wa Rais apewe taarifa halafu Mabeyo akatae.

Hii dhana inapata nguvu zaidi ukizingatia kwamba kulikuwa na habari muda mrefu tu kwamba Ofisi ya Makamu wa Rais ilikuwa imetengwa kwenye maamuzi mengi.

Habari ambayo January Makamba kaja kuthibitisha kwa kuisema wazi hivi karibuni.

Kwa hivyo, unaweza kutaka kumlaumu Mabeyo kwa kumtenga Makamu wa Rais, wakati hiyo ilikuwa amri ya Mkuu wa Majeshi Magufuli mwenyewe ambayo yeye Mabeyo aliona inambidi aitekeleze.
 
Okaaay...

Kumbe mada hiyo ilianzia kwake mwenyewe?

Na lazima akaweka pendekezo la jina. Upande ule wakazingua? Dah!
Hakuwa na chagua tayari alikuwa na chaguo lake lakini akashauriwa ( na kwa kutofahamu hila akakubali) na badala yake akawa Sa100.

Haya mambo hayahitaji Phd kuyadadavua ni kuunganisha dots tu.

Hivyo akiwa hoi akaona nchi yarudi kulekule na kwa kutaka kuyaendeleza aloyaanza akasahau kwamba kuna katiba na akataka BHR (yaani kiaina kuwe na serikali ya muda)awe makamu na ndipo zogo lilipoanza.

Zogo lilikuwa ni kubwa kwelikweli na kulikuwa na patashika nguo kuchanika.

Kwa hilo CFD alitekeleza jukumu lake la kusimamia katiba.

Ila kiukweli kwenye nchi yenye mfumo wa Kleptokrasia ni lazima wababe aka wapigaji wangeshinda.
 
..Mabeyo anastahili lawama.

..Kwanini MAKAMU WA RAIS hakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa kuwa Rais amefariki?

..Nimemsikia Mabeyo akisema eti kulikuwa na mjadala wa nani atangaze kifo cha Rais.

..Hivi Mabeyo na usomi wake, kutumikia jeshini kwa miongo kadhaa, na kutembelea nchi mbalimbali, hajui nani ana mamlaka ya kutangaza kifo cha Raisi? Kwamba walihitaji majadiliano?
Mkuu unatuangusha.
Mabeyo kasema vizuri Makamu hakuwepo alikuwa Tanga na inaonekana kumjulisha kwa njia ya simu walijuwa itavuja taarifa mambo ya kudukuana, eavesdropping, n.k.
Kumbuka katiba haijasema nani awe wa kwanza kupewa taarifa za kifo cha raisi bali imesema nani anatakiwa atangaze taarifa za kifo cha raisi.
 
Watu wanamsifia mobeyo ila kwa wachache tuliosomea Cuba tunaona hata yy alikua kwenye Dillema, na nahisi anajilaumu
Kuna mdau amesema huenda aliwaambia lianzisheni tuone upepo unavyoenda, ila sasa upande wa pili ukawazidi nguvu.

Hivyo akaamua kufanya kama hakuwa mmoja wao.

Ni kama mwalimu aliyewachorea mpango wa mgomo, ila mambo yanapovumburuka mkabambwa, ndiye wa kwanza kuwatembezea kipondo cha kufa mtu ili auepuke msala.
 
Misiba ya mwaka huu ya Lowassa na Mwinyi imenifanya nifuatilie maongezi ya Watanzania wengi mitandaoni na kuthibitisha zaidi hofu yangu moja.

Watanzania wengi wanapenda maneno ya uzushiuzushi, ya majungumajungu, ya kuokotezaokoteza.

Wengi wao ni watu unaoweza kuwaanzishia conspiracy theory wanayoioenda tu, mfano dhidi ya viongozi, wakaunga mkono bila hata kuhoji premise yenyewe.

Kwa sababu hawawezi majibizano ya kimantiki, yaliyo fact based, yanayoweza kufanyiwa verification.

Wanakubaki maneno yasiyo na source wala uthibitisho. Mradi unashambukia wasiyemoenda tu.

Sijui ni kitokana na kuishi katika jamii ambayo haitoi habari rasmi au nini.

Hali hii inaleta sintofahamu kubwa.

Maneno mengine ni ya kweli na hayatolewi rasmi, au yanachelewa sana kutolewa rasmi. Nimeangalia digital archive ya Dr. Salim Ahmed Salim, kuna vitu kibao vya 1960's na 1970's huko ambavyo leo havina umuhimu wa kuwa classified, lakini vilikuwa classified mpaka archive hii inaanzishwa.

Watu wetu wengi nao wana hasira na serikali, lakini hawajui kui critique kwa hoja na mantiki.

Mwisho wake unasikia habari ambazo zingekuwa za kuchekesha kama
si za kusikitisha.

Ndiyo hapo unaambiwa wale wauza madafu Ikulu ni watu wa usalama wa taifa. Hiyo nayo inakuwa story ya kushika watu akili.Au Rais Ali Hassan Mwinyi akiacha wosia azikwe Mkuranga, lakini mwanawe Hussein kamzika Zanzibar kisiasa, au Lowassa alitumwa kwenda CHADEMA kuvuruga upinzani tu.

Totally bonkers stories, kama vile tuna ukame wa scandals legitimate za hawa viongozi.
Hiyo ya wauza madafu ilinichekesha sana aisee.

Unajua kuna mystique flani hivi ambayo watu wa usalama wa taifa bongo, wanayo.

Sijui hata sababu ya hiyo mystique ni nini hasa.

Si ajabu hata wewe Kiranga kuna watu humu wanakuona usalama wa taifa kisa tu huwa unahoji uwepo na nguvu za Mungu.

Kuna university graduates humu [udsm] ambao hoja za kupinga uwepo wa Mungu wamezisoma kwako kwa mara ya kwanza.

Kwao, haiwezekani mtu wa kawaida tu kuhoji uwepo wa Mungu namna hiyo. Lazima atakuwa ni mmoja wa watu wa ‘kitengo’ 🤣.

Kwa ujumla tuna tatizo la upashanaji habari, tatizo ambalo limetengeneza ombwe ambalo linakuja kuzibwa na stori za vijiweni.
 
Yeye alijua katiba inasema makamu anakuwa Rais so huwezi kumtaarifu haraka sbb kiusalamanhuwezi kujua kama issue ya kumuondoa jiwe ilikuwa imeandaliwa na kuratibiwa na makamu kwa manufaa yake hivyo unamuweka pembeni ili kupata taarifa za usalama zaidi za nchi la sivyo mkienda kifala nchi inaweza vamiwa na wao wangeuawa na group jingine,,so ni strategy Bora amabyo mabeyo wliifanya
Hoja yako ingekuwa na mashiko fulani kama naye anaamini hakikuwa kifo cha kawaida.

Lakini mratibu wa tukio, halafu tena asijue yanayojiri katika njama zao wenyewe?

Na katika mazingira kama hayo, utamwamini nani na kumtuhumu nani? Kwa uhakika gani?

What if usiowadhania ndio wahusika hasa?
 
Hiyo ya wauza madafu ilinichekesha sana aisee.

Unajua kuna mystique flani hivi ambayo watu wa usalama wa taifa bongo, wanayo.

Sijui hata sababu ya hiyo mystique ni nini hasa.

Si ajabu hata wewe Kiranga kuna watu humu wanakuona usalama wa taifa kisa tu huwa unahoji uwepo na nguvu za Mungu.

Kuna university graduates humu [udsm] ambao hoja za kupinga uwepo wa Mungu wamezisoma kwako kwa mara ya kwanza.

Kwao, haiwezekani mtu wa kawaida tu kuhoji uwepo wa Mungu namna hiyo. Lazima atakuwa ni mmoja wa watu wa ‘kitengo’ 🤣.

Kwa ujumla tuna tatizo la upashanaji habari, tatizo ambalo limetengeneza ombwe ambalo linakuja kuzibwa na stori za vijiweni.
Umenikumbusha jamaa mmoja alikuwa jirani yetu.

Yule jamaa alikuwa anamuona mama yangu anaingia na kutoka nyumbani, very simple lady hana makuu.

Kuna siku ikawa vipi sijui, yule jamaa akagundua kuwa mama anafanya kazi Ikulu. Alistuka vibaya sana.

Akaja kuniuliza "Wewe, Mama yako anafanya kazi Ikulu siku zote hizi?" Nikamwambia ndiyo, kwani vipi? Akasema dah, mimi nilikuwa namuona simple tu, lazima atakuwa usalama wa taifa.

Nilishindwa hata kumwambia kwamba ni civilian non-intelligence worker tu Ikulu, yeye alishajiwekea kuwa yule mama ni usalama wa taifa, na ile kuwa simple ndiyo disguise yake.
 
Back
Top Bottom