Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna kitabu kinaandikwa juu ya haya!?Haya mambo yalijulikana na tuliyajadili hapa.
Mabeyo kaja kuweka rekodi wazi tu na hata hiyo kaweka kwa summary tu. Kuna mengi sana hajasema.
Kitabu kizima kikitoka mtastuka sana.
Naona ni maneno tu yasiyo na uthibitisho wowote ule.Sababu mojawapo nimeshaizungumzia pale kwenye comment yangu ya kwanza mkuu, it is up to you to take it or leave it, Mabeyo alitumia sababu ile ile ya siku zote na utaratibu ule ule wa ma CDF kustaafu
Lakini nyuma ya pazia hiyo haikuwa sababu kubwa, 'Wahusika' wanadai yeye na Magufuli walishapanga mwaka atakaostaafu, (endapo angeendelea kuwa hai) ambapo haikutakiwa kuwa 2022
Na CDF mpya alikuwa ameshaandaliwa Major General Charles Mbuge, ambaye naye alikuwa ni pro Magufuli, ndio maana kustaafu kwa Mabeyo kuliibua maswali kwa waliokuwa wanajua kinachoendelea
Mkuu kama ulimsoma katikati ya mistari ya kauli zake utaona mjadala ulikuwa unafanya kwingine yeye Mabeyo anafanya maamuzi kwa manufaa ya Taifa!
Hapo ndiyo ujue nchi yetu inawezesha kujiendesha yenyewe hata ikiwa na viongozi war-tar-two.Yale mahojiano pengine yamefanywa kwa wema ila yameniacha na maswali mengi sana juu ya uongozi wa nchi yetu na hatma ya Katiba yetu.
Ina maana wakati wote wa ugonjwa hadi rais hawezi tena kuongea, nani alikuwa anaongoza nchi?
^Tumafua-mafua^Wataka kusema Sa100 alikwenda Tanga na kukaa kule bila kufahamu kinoendelea?
Naona ni maneno tu yasiyo na uthibitisho wowote ule.
Haina shida, hata hivyo. Ni haki ya watu kusema, iwe uzushi au la!
Labda hofu kwamba itakuwa sawa na kusaini kifo chake mwenyewe?Nimewahi kusema tena humu, kwasababu ya ubinafsi wa watu wanaoteuliwa kugombea urais hasa ndani ya CCM, huwa wamekuwa na utaratibu wa kuteua wagombea wenza wenye ushawishi mdogo ndani ya chama na hata kwa wananchi.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba, marais wamekuwa wakipenda makamu wa rais ambao hawawezi kuwafunika. Si unaona hata Rais wa sasa alimteua mtu gani kuwa makamu wake?
Upatikanaji wa makamu wa rais unapaswa kuzingatia kwamba, huyu mtu muda wowote anaweza kuwa Rais wa nchi!
Sielezei kuwa kuna kitabu kinaandikwa, nasema kuwa kikiandikwa tutashangaa mengi.Kuna kitabu kinaandikwa juu ya haya!?
..kosa la Mabeyo ni kutokumpa taarifa Makamu wa Rais.
..Rais anapokuwa hawezi kutimiza majukumu yake iwe kwa ugonjwa au sababu nyingine Makamu anatakiwa kuziba pengo lililojitokeza.
..hiyo " mijadala " isingekuwepo kama Mabeyo angefuata na kuheshimu katiba tangu awali.
Hakuwa na chagua tayari alikuwa na chaguo lake lakini akashauriwa ( na kwa kutofahamu hila akakubali) na badala yake akawa Sa100.
Haya mambo hayahitaji Phd kuyadadavua ni kuunganisha dots tu.
Hivyo akiwa hoi akaona nchi yarudi kulekule na kwa kutaka kuyaendeleza aloyaanza akasahau kwamba kuna katiba na akataka BHR (yaani kiaina kuwe na serikali ya muda)awe makamu na ndipo zogo lilipoanza.
Zogo lilikuwa ni kubwa kwelikweli na kulikuwa na patashika nguo kuchanika.
Kwa hilo CFD alitekeleza jukumu lake la kusimamia katiba.
Ila kiukweli kwenye nchi yenye mfumo wa Kleptokrasia ni lazima wababe aka wapigaji wangeshinda.
Kama alitubu? Au alisazishwa kimkakati kwa masharti magumu na nafuu?Namba 2 mtoe hapo.. ndomaana unaona mpaka leo hakuguswa.
Mkuu unatuangusha...Mabeyo anastahili lawama.
..Kwanini MAKAMU WA RAIS hakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa kuwa Rais amefariki?
..Nimemsikia Mabeyo akisema eti kulikuwa na mjadala wa nani atangaze kifo cha Rais.
..Hivi Mabeyo na usomi wake, kutumikia jeshini kwa miongo kadhaa, na kutembelea nchi mbalimbali, hajui nani ana mamlaka ya kutangaza kifo cha Raisi? Kwamba walihitaji majadiliano?
Kuna mdau amesema huenda aliwaambia lianzisheni tuone upepo unavyoenda, ila sasa upande wa pili ukawazidi nguvu.Watu wanamsifia mobeyo ila kwa wachache tuliosomea Cuba tunaona hata yy alikua kwenye Dillema, na nahisi anajilaumu
Hiyo ya wauza madafu ilinichekesha sana aisee.Misiba ya mwaka huu ya Lowassa na Mwinyi imenifanya nifuatilie maongezi ya Watanzania wengi mitandaoni na kuthibitisha zaidi hofu yangu moja.
Watanzania wengi wanapenda maneno ya uzushiuzushi, ya majungumajungu, ya kuokotezaokoteza.
Wengi wao ni watu unaoweza kuwaanzishia conspiracy theory wanayoioenda tu, mfano dhidi ya viongozi, wakaunga mkono bila hata kuhoji premise yenyewe.
Kwa sababu hawawezi majibizano ya kimantiki, yaliyo fact based, yanayoweza kufanyiwa verification.
Wanakubaki maneno yasiyo na source wala uthibitisho. Mradi unashambukia wasiyemoenda tu.
Sijui ni kitokana na kuishi katika jamii ambayo haitoi habari rasmi au nini.
Hali hii inaleta sintofahamu kubwa.
Maneno mengine ni ya kweli na hayatolewi rasmi, au yanachelewa sana kutolewa rasmi. Nimeangalia digital archive ya Dr. Salim Ahmed Salim, kuna vitu kibao vya 1960's na 1970's huko ambavyo leo havina umuhimu wa kuwa classified, lakini vilikuwa classified mpaka archive hii inaanzishwa.
Watu wetu wengi nao wana hasira na serikali, lakini hawajui kui critique kwa hoja na mantiki.
Mwisho wake unasikia habari ambazo zingekuwa za kuchekesha kama
si za kusikitisha.
Ndiyo hapo unaambiwa wale wauza madafu Ikulu ni watu wa usalama wa taifa. Hiyo nayo inakuwa story ya kushika watu akili.Au Rais Ali Hassan Mwinyi akiacha wosia azikwe Mkuranga, lakini mwanawe Hussein kamzika Zanzibar kisiasa, au Lowassa alitumwa kwenda CHADEMA kuvuruga upinzani tu.
Totally bonkers stories, kama vile tuna ukame wa scandals legitimate za hawa viongozi.
Most likely aliamini kama alivyoamini bosi wake, ndiyo maana akafanya alivyofanya.Jiulize kama alijua makamu ndie second kwa nn wamuite waziri mkuu kwanza? Je na yy alikua anaingiwa na kile kishawishi cha kina bashiru?
Ningekua Mobeyo ningekaa kimya tu, nikala benefit of the doubt
Hoja yako ingekuwa na mashiko fulani kama naye anaamini hakikuwa kifo cha kawaida.Yeye alijua katiba inasema makamu anakuwa Rais so huwezi kumtaarifu haraka sbb kiusalamanhuwezi kujua kama issue ya kumuondoa jiwe ilikuwa imeandaliwa na kuratibiwa na makamu kwa manufaa yake hivyo unamuweka pembeni ili kupata taarifa za usalama zaidi za nchi la sivyo mkienda kifala nchi inaweza vamiwa na wao wangeuawa na group jingine,,so ni strategy Bora amabyo mabeyo wliifanya
Umenikumbusha jamaa mmoja alikuwa jirani yetu.Hiyo ya wauza madafu ilinichekesha sana aisee.
Unajua kuna mystique flani hivi ambayo watu wa usalama wa taifa bongo, wanayo.
Sijui hata sababu ya hiyo mystique ni nini hasa.
Si ajabu hata wewe Kiranga kuna watu humu wanakuona usalama wa taifa kisa tu huwa unahoji uwepo na nguvu za Mungu.
Kuna university graduates humu [udsm] ambao hoja za kupinga uwepo wa Mungu wamezisoma kwako kwa mara ya kwanza.
Kwao, haiwezekani mtu wa kawaida tu kuhoji uwepo wa Mungu namna hiyo. Lazima atakuwa ni mmoja wa watu wa ‘kitengo’ 🤣.
Kwa ujumla tuna tatizo la upashanaji habari, tatizo ambalo limetengeneza ombwe ambalo linakuja kuzibwa na stori za vijiweni.