Uhaba wa taarifa unawafanya watu wakisie sana.
Sijui lawama nyingi ziende kwa nani, ila serikali kwa ujumla wake haiwezi kuzikwepa.
Hivi inajulikana kwa uhakika kwa nini mke wake hakuwepo wakati anavuta pumzi ya mwisho?
Vipi kama alikuwa kaenda tu nyumbani kupumzika kidogo na kuangalia mambo mengine na ikatokea muda ambao hakuwepo wodini ndo mume wake naye akafariki?
Yawezekana kabisa alikuwa yupo hapo kwa Mzena kwa muda mwingi tu lakini si kwa kila sekunde na dakika kwa masaa 24.
Kama umewahi kuuguza, hususan mtu mzima, huwa inatokea muda na wewe unatoka kidogo kwenda labda kuoga, kubadili nguo, na kufanya mambo mengine halafu unarudi tena kuwa na mgonjwa.
Hapa kuna uhaba mkubwa wa taarifa na tunalazimika kuhisi na kukisia baadhi ya mambo maana hata kuugua na kulazwa kwake hatukufahamishwa. Tulisikia habari kupitia njia mbadala.
Tukaja kutangaziwa kifo tu.