KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 3,250
- 5,509
Natumia jukwaa kuelezea kauli tata ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Mhe. Chatanda na kumtaka aliyoitoa kuomba radhi kwa kauli hiyo na akemewe.
Sina mashaka na uwezo na uzalendo wa Mhe.Chatanda katika kazi zake za kukiimarisha Chama lakini kauli zenye mashaka daima lina chimbuko la kusudi la kauli hiyo.
Nanukuu kipande cha kauli hiyo tata "... angenipa nchi hii ndani ya dakika moja ningeimaliza CHADEMA".
Tafsiri ya utata wa kauli hiyo:
1. Ni kauli iliyojaa dharau kubwa kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wetu kuwa kama Mwenyekiti ameshindwa kudili na CHADEMA ila yeye ataiweza ndani ya dakika moja yaani sekunde 60 tu.
2. Ni kauli inayoonesha kwa kiwango kikubwa hayupo sawa na Rais ambaye anataka maridhiano. Kauli ya kusema utaifuta ndani ya dakika moja maana yake ungetumia nguvu kubwa mno.
3. Ni kauli inayoonesha na kuitafsiri vibaya mamlaka ya urais ,kwamba Rais kwa kutaka tu anaweza kufuta Chama Cha Siasa.
Swali kuu la kujiuliza: ikatokea kweli CHADEMA imefutwa kutoka na mienendo yake, si itaonekana ni Rais kafanya hivyo?
Hivyo basi , kulingana na tafsiri ya utata niliyotoa juu ya kauli hiyo ninamuomba
Kwanza, Mhe. Chatanda aombe radhi kwa kauli hiyo.
Pili, viongozi wasitoe kauli zenye kutafsiri vibaya mamlaka ya viongozi hususani Rais
tatu, naomba Chama kikemee kauli hiyo na kauli nyingine kama hizo.
Ahsante
Pia soma: PostGE2025 - Mary Chatanda: Samia angenipa nchi dakika moja, ningeimaliza CHADEMA