Kauli ya Chongolo ni ufedhuli kwa wasomi wa vyuo vikuu. Ipingwe!

Wewe ndiyo hujamuelewa CG Chongolo. Ukiwa na tertiary education ukipita na VETA unaweza kufanya wonders ktk maisha kiuchumi. Hajasema elimu ya juu haina faida wewe umechukua hoja out of context. 🙏🙏🙏
 
Suluhisho ni wahitimu wote wa vyuo vikuu, wapewe kazi kama interims huko huko serikali au sehemu yoyote at least miezi sita bila malipo ili wajenge CV zao kwenye sehemu ya working experience...
 
Bahati mbaya humu wengi bado awajui mfumo wa Veta unavyo fanya kazi kuna aina mbili za kozi za mda mrefu na mda mfupi ni mtu mwenyewe kuchagua achukue mda mfupi au mrefu kwa kozi ndefu Veta wana mfumo unaitwa CBA ambao una ambatana na baadhi ya masomo ya secondary na mengine ya ki inginia masomo ni hayo
FANI HUSIKA
ENGLISH
COMPUTER
TECHNICAL DRAWING
ENGINEERING SCINCE
ENTREPRENEURSHIP
LIFE SKILLS
MATH

Utasoma kwa miaka miwili ukifahuru una enda mwaka tatu ukifahuru una enda diploma ndani ya miaka hii mitatu mtu wa Veta anakuwa amejifunza kwa vitendo zaidi na ata akienda diploma ni kama masomo ni yale yale
 
Tunatoa ushauri kwa manufaa yenu nyie wahitimu wa vyuo vikuu, maana nyie hata kupika vitumbua kama mimi hamuwezi, mnaishia kulalama tu mkiwa hamjui cha kufanya.
Unalipa ada ili ifundishwe kupika vitumbua? Shame on u!

Kazi zinazofanywa na wahitimu wa veta hazihitaji elimu. Zinahitaji utayari tu. Naweza nikaangalia siku moja mpk wiki moja tu nikajua kufanya hizo kazi.
 
Unalipa ada ili ifundishwe kupika vitumbua? Shame on u!

Kazi zinazofanywa na wahitimu wa veta hazihitaji elimu. Zinahitaji utayari tu. Naweza nikaangalia siku moja mok wiki moja tu nikajua kufanya hizo kazi.
Maneno ya kijiami haya na uoga kwa hiyo una weza kujifunza umeme kwa kuangalia kwa siku moja au ujenzi uselema utengenezaji wa magari? Mkuu una kipaji kikubwa sana
 
Unachanganya mambo hata yasiyohusika kabisa na mada.
Bottomline hapa ni mtu kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yake kiutu; kuwa na pato la kujitegemea halali.

Wewe unakwenda kusoma political science ili uajiriwe, halafu hakuna wa kukuajiri utawalazimisha kwa nguvu?

Ulishawahi kuona wapi duniani mtu anakwenda kusoma digrii akiwa na uhakika wote kabisa kwamba atapata ajira, na asipopata hiyo ajira adai kuajiriwa hata kama hakuna uhitaji wa huo ujuzi wake alioupata kwenye digrii?

Si hata ni bora ungesema ajibidishe atafute kazi kwenye eneo linalokaribiana na hayo aliyosoma, kama kuna nafasi za kuajiriwa huko. Au akawe mwalimu wa hesabu, shule ya msingi mahali fulani kama kuna uhitaji wa walimu wa aina hiyo.
 
Unalipa ada ili ifundishwe kupika vitumbua? Shame on u!

Kazi zinazofanywa na wahitimu wa veta hazihitaji elimu. Zinahitaji utayari tu. Naweza nikaangalia siku moja mpk wiki moja tu nikajua kufanya hizo kazi.
Yes! Shame on me. Lakini wewe mhitimu wa chuo kikuu huelewi hata mifano!

Kupika vitumbua ni mfano wa shughuli za ujasiriamali, moja ya mapungufu ya hiyo elimu yenu hamuwezi kusurvive bila ajira, at the same time unadharau wapika vitumbua.

Wewe umekariri kwamba ukilipa ada hutakiwi kupika vitumbua, ukisoma hutakiwi kufanya shughuli za ujasiriamali, that is what you know!

Unasema kazi zinazofanywa na wahitimu wa VETA hazihitaji elimu! Hii kauli inaonyesha hujui hata maana ya elimu. Mimi naomba niishie hapa Mkuundugu yangu.
 
Unalipa ada ili ifundishwe kupika vitumbua? Shame on u!

Kazi zinazofanywa na wahitimu wa veta hazihitaji elimu. Zinahitaji utayari tu. Naweza nikaangalia siku moja mpk wiki moja tu nikajua kufanya hizo kazi.
Fanya sasa.
 
Wasomi wengi wa vyuo vikuu vya Tanzania wanataka pesa za haraka haraka ndio maana wengi wamekimbilia kwenye bodaboda.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yani ukimwambia msomi akajifunze hata ufugaji wa kuku au kutengeneza sabuni au vifungashio kule SIDO halafu atafute masiko anaona atachelewa kupata Elfu Kumi na Tano Kwa siku . Lakini akipaki kijiweni hakosi Hela kila baada ya nusu saa. Hapo huwezi kumtoa kwenye Biashara ya boda boda Tena.
Lakini boda boda haizalishi Wala kutoa ajira Kwa mtu Mwingine zaidi ya Dereva mmoja tuu.
 
Kwani wahitimu wa vyuo vikuu wanaomiliki first degree na masters wanaweza nini mtaani tofauti na waliotoka vetaa? Kwangu mimi tukija mtaani waliotoka vets ni bora kuliko waliotoka chuo kikuu maana kijana aliytoka veta anauza kazi alizosomea veta kama amesomea ufundi wa kuchomea vyuma anatengeneza milango na grill za madirisha anatengeneza pesa ndefu wa chuo kikuu ana tembea na briefcase kwenye maofisi kuomba kazi asipoajiriwa ndiyo anakuwa hivyo maisha yake
 
Kwani wahitimu wa vyuo vikuu wanaomiliki first degree na masters wanaweza nini mtaani tofauti na waliotoka vetaa? Kwangu mimi tukija mtaani waliotoka vets ni bora kuliko waliotoka chuo kikuu
Sawa. Lkn je, suluhu ndiyo iwe kumpeleka mhitimu wa chuo kikuu veta?

Nilitarajia Chongolo atoe suluhisho mujarabu kama kuboresha masomo ya chuo kikuu yawe kwa vitendo zaidi.

Ama kama serikali yake imeshindwa kupata ufumbuzi wafute vyuo vikuu
 
Chief huo ni ukweli mchungu.....tukubali tukatae ila unbak kuwa ukweli....
 
Field yeyote inayo mpelekea mtu kujiajiri ni Bora zaidi kuliko PhD inayo subiri Ajira.
Kumbuka Kuna skills mtu anazipata application yake mpaka aajiliwe hata Kama amesoma vipi. Lkn pia Kuna skills mtu akipata anajiajiri moja kwa moja hata Kama ni elimu ndogo.

Kama unaamini Ajira imekuwa changamoto nchi hii kwa Sasa lkn bado unaipinga kauli ya chogolo duu sijui nikuweke wapi
 
Kweli mkuu Watoto wa sekondari
 
Ha!haa!haaa!
Yaani ana kidharau hiki!
 
Bongo wengi wa wanaoitwa wasimo,ni comedian tu.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…