Kauli ya Chongolo ni ufedhuli kwa wasomi wa vyuo vikuu. Ipingwe!

yeye alienda huko veta kuongeza ujuzi baada ya kumaliza elimu yake?
 
Bongo wengi wa wanaoitwa wasimo,ni comedian tu.[emoji23][emoji23][emoji23]
Hata wakiwa vyuoni wanasoma Kwa malengo ya kuajiriwa.

Hivi inaingia akilini kweli walimu wanawaza kuajiriwa na mtu aliyeanzisha shule ya nursery chini ya mwembe akiwa mama wa Nyumbani.

Kwa Nini walimu Saba wasiungane wakaanzisha Darasa lao kuanzia chekechea au kama ni sekondari wakaanza Kwa Bei nafuu Kisha jamii ikaona uwezo wao na kuwapelekea ada na kuandikisha mamia ya watoto baada ya miaka Kumi wakawa wanamiliki shule yao wenyewe.

Tatizo uwezo mdogo wa taaluma waliyoipata nao unachagia. Wengi you anataka kuajiriwa SERIKALINI eti ni uhakika wa ajira hata akiwa analala baa na kukesha kwenye pombe hafukuzwi kirahisi . Wanawaza uzembe uzembe TU na ufisadi.
 
Bora veta Kwa kigezo gani cha ajira au kuna kingine?
 
Ni rahisi kupinga hiyo kauli lakini ni kauli nzuri sana.VETA haipo kwa waliofeli kwenda chuo kikuu.Itakua ajabu kwa engineer kurudi veta kujifunza engineering.Lakini kwa mtu aliyehitimu Degree yoyote ile akitaka kuwa na Plan B kama vile ushonaji,usidikahi bidhaa,ufungashaji nk.. sio mbaya kupata ujuzi wa kile unachotaka kufanya.Ukiwa na ujuzi huo na ukachanganya na Degree Yako unakuaa mbali.Wenzetu hasa wachina hiyo ni kawaida sana
 
Wanaogopa kuonekana ! Watajulikana kumbe sio wenzetu !
 
Kama watatoa na pesa kidogo za kujikimu pale VETA itapendeza sana !!
 
Kwakweli !!
 
Ni upumbavu kuukataa ukweli.
Vyuo vikuu wanafundisha ujinga mwingi na ndio sababu tuna wahitimu wajinga wajinga tu.Kama mmeshindwa kuonesha uwezo wenu hata mkiandamana haisaidii.
Kazi yenu imebaki kutengeneza sheria za kuwabagua mnaodhani ni tishio kwenu mkidhani sheria ndiyo itawapa hadhi.

Heshima ya mtu hutokana na huduma anayoitoa kwa jamii na si sheria za kijisifu bure kwa maneno matupu
 
Heshima ya mtu hutokana na huduma anayoitoa kwa jamii na si sheria za kijisifu bure kwa maneno matupu
Veta mkaanaga vitumbua awe na heshima kuliko mhiyimu wa chuo kikuu? Unaijua heshima wewe? Yaani ufundi cherehani ukupe heshima!!?
 
Mjadala kama hii ingependeza wakutane wataalamu wajadili Kwa hoja na maelewano ili jibu lipatikane. Ningeomba mkuu Maxence Melo awe na platform maalum za kukutana wataalamu kujadili vitu vya kitaalmu. Watu wengine wawe wanaona tu na washindwe kuchangia ili mjadala uwe wa kujenga na si kupotosha /kubishana tu.
Mijadala hii watu waambatanishe na CV zao au vyeti ili wapewe nafasi ya kuruhusiwa kujadili. Hiv mm Sir Midabwada atachangia Nn kwenye masuala ya umeme?. Lakini atachangia na nyuzi itajaa koments ambazo hazijengi.
Cc. JamiiTalks
Moderator
YinYang
 
Huyo chongolo anajua malengo ya elimu ya chuo kikuu na malengo ya VETA? au ndo aina ya wanasiasa wakurupukaji waliopo hapa bongolala..........kwa thinking za namna hii haishangazi daktari wa mchongo Msukuma kuomba mdahalo na maprofessa wa chuo kikuu kuongelea mada za kiuchumi.
 
Basi usijivike kitu ambacho hata hukijui. Eti mkaanga vitumbua uheshimike kuliko mhitimu wa chuo kikuu!!. Nyoo! Unajua chuo kikuu wewe!!?
Chuo kikuu kuna nini kinacho kufanya uheshimike kuliko watu wote wasio fika chuo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…