Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Dkt. Festo Dugange, ametoa agizo kuwa waajiriwa wote wapya wa Serikali lazima wafanye kazi kituo kimoja kwa muda usiopungua miaka mitatu (3) kabla ya kuruhusiwa kuomba uhamisho, isipokuwa kwa changamoto za kiafya zilizothibitishwa na jopo la madaktari.
Lengo la Serikali ni Kuhakikisha vituo vilivyopangiwa watumishi (hasa maeneo ya pembezoni) vinapata huduma stahiki na kudhibiti wimbi la watumishi kukimbia vituo hivyo muda mfupi baada ya kuripoti. Hili ni jambo la msingi kwa maendeleo ya Taifa letu.
Uhalisia na Kilio cha Watumishi: Watumishi wa Umma kupitia JamiiForums na mitandao mingine ya kijamii, wamekuwa na kilio cha muda mrefu kuhusu changamoto za uhamisho. Malalamiko haya yameenda mbali zaidi ya "kutaka tu kubadili mazingira" na kugusa msingi wa maisha yao:

- Kuvunjika kwa Ndoa/Kutengana kwa Familia: Watumishi wengi (hasa walioko kwenye ndoa changa) wametenganishwa na wenza wao kwa miaka mingi. Kuomba uhamisho wa kumfuata mwenza (spouse transfer) kumekuwa na ukiritimba mkubwa. Hii inatishia uhai wa ndoa nyingi na makuzi ya watoto wanaokosa malezi ya wazazi wote wawili.
- Afya ya Akili na Msongo wa Mawazo (Depression): Upweke, matatizo ya kifamilia, na mazingira magumu yanasababisha msongo mkubwa wa mawazo kwa watumishi wengi, jambo ambalo linaathiri moja kwa moja ufanisi wao kazini.
- Urasimu na Rushwa: Baadhi wanadai kuwa mchakato wa uhamisho umekuwa mgumu kwa wanyonge, huku wenye "kujuana" wakipata uhamisho kwa urahisi hata kabla ya hiyo miaka mitatu.
- Je, ‘sheria’ hii ya "Miaka 3" inaweza kutekelezwa bila kuathiri ustawi wa familia (ndoa) na afya ya akili ya watumishi?
- Serikali inapaswa kufanya nini ili kuvutia watumishi kubaki maeneo ya pembezoni (Retention strategy) badala ya kutumia shuruti ya kuzuia uhamisho?
- Nini kifanyike kurahisisha na kuweka uwazi kwenye mchakato wa uhamisho wa kumfuata mwenza ili kunusuru ndoa za watumishi wa umma?
- Kama wewe ni mtumishi au una ndugu/mwenza mtumishi, umepitia changamoto gani katika suala la uhamisho?