Tujadiliane:
1. Je, ‘sheria’ hii ya "Miaka 3" inaweza kutekelezwa bila kuathiri ustawi wa familia (ndoa) na afya ya akili ya watumishi?
Jibu: Nini kutekelezwa hata kupitishwa kama muswada rasmi wa sheria haiwezi kutokea kwasababu ya maslahi mapana ya wahusika. Huwezi kulazimisha kundi kubwa la watendaji kwa kauli za mihemko ambazo sio sheria.
2. Serikali inapaswa kufanya nini ili kuvutia watumishi kubaki maeneo ya pembezoni (Retention strategy) badala ya kutumia shuruti ya kuzuia uhamisho?
Jibu: Inatakiwa kutoka madarakani iachie wengine wenye uwezo wa kubadili mfumo na kujenga mazingira rafiki yatakayo mrahishia mtumishi kufanya majukumu yake. Vinginevyo, wahesabu maumivu na huduma mbovu kwa walengwa.
3. Nini kifanyike kurahisisha na kuweka uwazi kwenye mchakato wa uhamisho wa kumfuata mwenza ili kunusuru ndoa za watumishi wa umma?
Jibu: Kuundwa kwa Mfumo usio na upendeleo wa upande wowote. Uwezo upo lakini Serikali haiko tayari kuutekeleza kwa kuhofia kuingia matatizoni kwa kukiuka usawa na haki za kibinadamu.
4. Kama wewe ni mtumishi au una ndugu/mwenza mtumishi, umepitia changamoto gani katika suala la uhamisho?
Jibu: Ndiyo, mimi ni mtumishi na nimepitia changamoto katika maombi yangu ya uhamisho hasa katika suala la kwamba nina stahiki zote za kutakiwa kuhamisha yaani kwa lugha nyingine nimetimiza vigezo vyote na kufanya maombi kwa njia zote yaani kwa mfumo na kwa makaratasi lakini nimenyamaziwa kimya kana kwamba maombi yangu hayana msingi. Matokeo yake, hasara ninayoendelea kuisababisha... Ni kubwa kiasi cha kutokujulikana chanzo hivyo kuendelea kupoezeana muda na rasilimali mpk ntakapostaafu.
NINA CHUKI YA NDANI KUBWA NLIYOAMUA KUITUMIA KIMKAKATI KUMUUMIZA ADUI KILA IITWAPO LEO. AHSANTE!