Kauli ya huyu mpenzi wangu imenitafakarisha sana

Kauli ya huyu mpenzi wangu imenitafakarisha sana

Wakuu siku za hivi karibuni niliutaarifu umma wa JF kwamba niko penzini na single mama mwenye mtoto mmoja ambaye pia nimemkuta na mimba changa. Penzi bado ni tamu ila jana usiku kuna kauli katamka ikanivuruga.

Iko hivi... sisi wote ni wajasiriamali. Mimi nina biashara yangu na yeye ana yake. Sasa katika stori za sisi wapendanao ndo akatamka kuwa huu mji tuliopo ni mgumu kibiashara isingekuwa ni mwanae ambaye yuko shule ya msingi angehama hata kesho. IKANIVURUGA. Ina maana mimi hadi sasa sio lolote kwenye mipango yake kiasi cha kutamka kuwa mtoto wake ndo kizuizi? Kwa kweli hawa single mama wana namna nyingi mno za kukuvuruga.

WanaJF nishaurini ila NATOA ONYO nisisikie ushauri wa kusema niachane na mpenzi wangu ninayempenda kuliko CHADEMA wanavyopenda michango ya wafuasi wao.
Mwambie utamsaidia kufanya uhamisho wa mtoto.
 
Labda nikuambie tu kwa Faida yako na ya Watu (Members) wote hapa JamiiForums kuwa HAKUNA KIUMBE KISICHOAMINIKA WALA KISICHORIDHIKA KWA LOLOTE NA CHOCHOTE KAMA MWANAMKE.

Kama Wewe ni Mwanaume na uko katika Mahusiano na Mwanamke (rasmi au si rasmi) hakikisha tu UNATIMIZA WAJIBU WAKO KWAKE KIUPENDO NA KAMWE USITEGEMEE SIJUI ASANTE AU FADHILA KUTOKA KWAKE kwani hata tu KISAIKOLOJIA WANAWAKE HAWAJAUMBWA HIVYO na ndiyo maana hata mwenyewe (Mwenyezi Mungu) ALIYEWAUMBA katuagiza Sisi WANAUME kuwa TUISHI NA WANAWAKE KIAKILI.

Kama UNAMPENDA basi hakikisha UNAMHUDUMIA hata kama mna KIPATO SAWA au AMEKUZIDI au ana MALI zaidi yako na achana na huu USHAMBA wa KULALAMIKA kuwa humuelewi bali kuwa Mwanaume wa kweli na anayejimbua (Gentleman)
Charismatic Fella mbona umeandika kistaarabu sana leo? Safi sana.
 
Wakuu siku za hivi karibuni niliutaarifu umma wa JF kwamba niko penzini na single mama mwenye mtoto mmoja ambaye pia nimemkuta na mimba changa. Penzi bado ni tamu ila jana usiku kuna kauli katamka ikanivuruga.

Iko hivi... sisi wote ni wajasiriamali. Mimi nina biashara yangu na yeye ana yake. Sasa katika stori za sisi wapendanao ndo akatamka kuwa huu mji tuliopo ni mgumu kibiashara isingekuwa ni mwanae ambaye yuko shule ya msingi angehama hata kesho. IKANIVURUGA. Ina maana mimi hadi sasa sio lolote kwenye mipango yake kiasi cha kutamka kuwa mtoto wake ndo kizuizi? Kwa kweli hawa single mama wana namna nyingi mno za kukuvuruga.

WanaJF nishaurini ila NATOA ONYO nisisikie ushauri wa kusema niachane na mpenzi wangu ninayempenda kuliko CHADEMA wanavyopenda michango ya wafuasi wao.
Kikao kilishaongea sana, kuhusu Viwanja vyenye mgogoro
 
Siku zote mwanaume anamtongoza mwanamke anayemtamani( sio anaempenda) ila mwanamke ndo huwa na upendo wa kweli kwa mwanaume.

Mwanaume anampenda mwanamke baada ya huyo mwanamke kumjali na kumuonesha upendo wake.
Kheeeh kumbee? Mabwakuu, Lol
😂😂😂😂
 
a1916097e3f8a90fcffd05736da62978.png
 
Back
Top Bottom