Kauli ya Jaji Tiganga kwamba huenda Shahidi Ling'wenya alikuwa anapewa majibu ya maswali aliyoulizwa yawaibua Wadau

Kauli ya Jaji Tiganga kwamba huenda Shahidi Ling'wenya alikuwa anapewa majibu ya maswali aliyoulizwa yawaibua Wadau

Mna visingizio sana tulieni dawa iwaingie maana mlitamba sana mama anaupiga mwingi.

Mkome kabisa tabia ya kuingilia mahakama.
Mtu mwenye akili timamu hawezi kuitetea Serikali hii ya Wala rushwa dhidi ya kudorora kwa Umeme pamoja na maji.

MTU yoyote anayetetea hilo anaongozwa na tumbo,anaongozwa na Uroho pamoja na tamaa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ole wenu mchekao sasa maana siku yenu yaja mtalia na kusaga meno.
Wewe na mmeo mlikenua sana Sabaya alipofungwa, sheria ni msumeno tulieni dawa iwaingie
 
Komandoo wa JWTZ wamefunzwa vyema mafunzoni jinsi ya kuongoza, kutoa amri, ukamataji, movement orders, chain of command na wanazizingatia sana wawapo kazini na kuziota usiku kiasi wanazifahamu kwa ufasaha hata wawapo katika misheni za ulinzi wa amani kimataifa askari na maofisa wa JWTZ / TPDF wanazifuata kwa umakini na ndiyo maana wanatambulika na Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia kanuni, sheria vizuri .

Tofauti na polisi ambao hata PGO inayowaelekeza watende kazi vipi kipolisi tumeona hazifuatwi ndani ya jeshi hilo la Polisi. Hakuna movement orders, kuandika kumbukumbu vizuri ktk shajara za kipolisi n.k

Hivyo mtu yeyote pamoja na Jaji inatakiwa watambue nidhamu iliyopo ktk JWTZ / TPDF wa utendaji kazi ukiotukuka na wa kufuata kanuni na sheria .

07 October 2021



Source : Mashariki TV
Hivi najiuliza ilikuwaje makomandoo wa jesh kuninginizwa kirahisi rahis hivi na polisi kama si udhalilishaji wa jeshi la wananchi hasa hawa makomandoo wa 92kj?
 
Jaji kashindwa kujizuia kutoonysha dhamila yake. Ana dhamila mbaya sana dhidi ya washitakiwa. Washitakiwa wamkatae huyu jaji
 
Hivi najiuliza ilikuwaje makomandoo wa jesh kuninginizwa kirahisi rahis hivi polisi kama, si udhalilishaji wa jeshi la wananchi hasa hawa makomandoo wa 92kj?

Askari wakakamavu shupavu wa TPDF waliokula kiapo kuwa walinzi wa Taifa pia askari wa jeshi la akiba wakiacha jeshi, ni wavumilivu na wenye nidhamu hivyo walikuwa wanakariri udhaifu wa utendaji kazi wa Polisi wasiofuata PGO , sheria , kanuni ,katiba na kusubiri wakati muafaka watapopata uwanja wa kujitetea na kujiepusha kufanya jambo lolote litakalo wafanya waonekane "wahuni" .

Mvumilivu komandoo wa TPDF sasa anatoa ushahidi ya jinsi jeshi la Polisi linavyohitaji kusukwa upya kuanzia maofisa mpaka askari Polisi wa kawaida ILI nchi iweze kwenda sawa. Bila uvumilivu wa makomandoo wetu sisi raia wengine tungejua vipi jeshi la Polisi lisivyofuata PGO na kanuni zingine kibao za kiutendaji ili haki ipatikane .
 
Nadhani ameshangazwa na umakini wa shahidi mshitakiwa. Kama shahidi mashitakiwa kaamua kusema ukweli anaoujua yeye, ni lazima wenye hila wajiulize kwanini yuko na mtiririko huo!!

Kinachoshangaza kwa sisi maamuma wa sheria ni kama kuna ushahidi usiokuwa na mashaka kuwa mashitaka yatathibishwa - kina haja gani ya mshitaki kuweka pingamizi la kutaka mshitakiwa asijieleze??!!

Ajabu zaidi sababu wanazotumia kupinga upatikanaji wa document ya shahidi wa mashitaka (mpaka ikapelekea kuhoji kama mahakama imewasiliana na mshitaki kinyume cha taratibu) ndio wanazotumumia kuhoji barua anayotaka kuwasilishwa imemfikiaje mahabusu asiyekuwa huru!! Wanasisitiza hata kuhusu chain of custody ni shida, jambo ambalo hawakuonesha ni shida upande wao.

Leo wanasema Kibatala ni wakili wa mshitakiwa wa nne (Mbowe) hivo hakupaswa kuandika barua. Anasahau mawakili hawa hawajiwakilishi bali kampuni zao kama wao wasiviwakilisha isipokuwa serikali! Wanasahau hawajapinga Kibatala kuhoji mashahidi wao ambao walikuwa wanatoa ushahidi kuhusu walivowakata washitakiwa 1-2 na wala sio hata 3.

Mawakili wa serikali wameshindwa hata kutambua kuwa hata wao hawana mawakili dhidi ya mshitakiwa mmoja mmoja. Wamesahau washitakiwa wote wako katika kesi moja 16/2020 na wote wanashitakiwa kwa makosa yanayofanana isipokuwa mmoja kuhusu silaha na risasa!!
Hii Kesi mbona Siuoni Ugaidi? MBOnA HAIENDI STRaIGHT KWeNYe KOSa? KOSA MBONA HALIFIKIWI?
 
Sidhani kama una akili timamu , na kwa kweli kuna haja sana ya JF kutumia ujasusi wake kutambua kama baadhi ya wachangiaji wake ni wazima kichwani au La
Wee una uzima gan.mnatabia ya ujuaji kweli kuwa kila kitu manjua ninyi
 
kama sikosea huyo ni jaji wa tatu kwenye hii kesi.... na kila Jaji akija malalamiko ni yaleyale... sasa muafaka ni nini?.....wafuasi wetu uelekeo upi wafuate..., tunaendeleaje kufuatilia kesi na kusubiri matokeo yake ilihali tunaamini jaji yupo kimkakati.... Je tutasemaje mwishoni jaji huyu akimuachia mtu wetu?...

..suluhisho ni kuleta Jaji toka nchi mojawapo ya Jumuiya ya Madola.

..Kuna wakati Tz tulikuwa na Jaji Mkuu toka nje, nadhani Trinidad and Tobago.

..pia Jaji Samatta na Jaji Mfalila waliwahi kuhudumu mahakamu kuu ya Zimbabwe.
 
Hivi najiuliza ilikuwaje makomandoo wa jesh kuninginizwa kirahisi rahis hivi na polisi kama si udhalilishaji wa jeshi la wananchi hasa hawa makomandoo wa 92kj?
Wale watu walikuwa hawajajiandaa kwa lolote wao walikuwa wameenda pale ili wapate ajira walishtukizwa, lakini hata ukiwa komandoo ukifungwa pingu na ukawekewa silaha utafanywa chochote.
 
jaji kaona isiwe tabu, kaamua kuweka mpira kwapani.
 
Kabla hamjajifunua, sheria zinasemaje kuhusu kauli ya jaji?

Kama sheria zinakataza, kwanini mawakili wa utetezi walikaa kimya?
 
Back
Top Bottom