Kauli ya Jaji Tiganga kwamba huenda Shahidi Ling'wenya alikuwa anapewa majibu ya maswali aliyoulizwa yawaibua Wadau

Kauli ya Jaji Tiganga kwamba huenda Shahidi Ling'wenya alikuwa anapewa majibu ya maswali aliyoulizwa yawaibua Wadau

Mkuu, hiyo ndio thamani ya ukweli. Haihitaji kufikiria sana, ni kuusema tu!

Unaweza kuona hata wasiwasi wa Jaji kuwa mhutumiwa anafundishwa majibu. Hivi kweli jambo hilo lingewezekana? Jaji aligundua maandalizi. Advantage pekee aliyokuwa nayo mtuhumiwa ni kuwa aliwasikia kwa masikio yake mashahidi wa mashtaka na maana yake siku zote amekuwa akijipanga kuzungungimzia hiyo story. Unlike mashahidi wengine ambao hawakuwa mahakamani siku zote. Ilinishangaza Jaji kutotambua hili!

Cross examination and re-examination za leo zitavutia sana. Utetezi utakusudia kutia matundu katika ushahidi woooote ulitolewa mpaka sasa. Na ni bahati nzuri mpaka sasa mashahidi wamekuwa ni wa ukamataji, usafirishaji, upelelezi, Central na Mbweni!! Na mshitakiwa mhusika!
 
Shahidi: Nimeona Nakala ya Barua Leo, aliyeandika ni Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi

Matata: Sasa Umejuaje kama Kaandika Kibatala

Shahidi: Tangu kesi inaanza ndiye alikuwa wakili wa Washtakiwa wote tangu tupo Kisutu, na ndiye aliyekuwa anatuandikia Mabarua yetu kwenda sehemu mbali mbali.

Matata: hiyo Barua Ukiiona utaitambuaje?

Shahidi: Kwa Kuona Majina na Sahihi ya Kibatala kwa Sababu Kaniandikia Barua Nyingi sana sahihi yake naifahamu

Matata: ina nini Kingine

Shahidi: Muhuri wa Naibu Msajili

Matata: Naibu Msajili wa wapi

Shahidi: Mahakama ya Divisheni

Jaji: Nina Wasiwasi kuna watu wanamsaidia shahidi kutoa majibu

Matata: shahidi ikijibu muangalie Jaji kumtoa wasiwasi wa majibu yako

MHENGA.jpg
 
Teknolojia ni jambo la kuliogopa sana.

Hii kesi inaripotiwa tofauti na zama za zamani.
Ndio maana wanapinga, kwasababu watakuwa hawana kidhibiti, chakuonyesha kuwa walifika central polisi Dar. Wakiambiwa walete CCTV ya tarehe zile waakina Ling`wenya wakiingia watakuwa hawana.
 
Huyo jaji labda kuna mizimu ya kwao ambayo yeye jaji anaiona ipo na shahidi pale kizimbani. Kizimbani shahidi anakuwa pekee yake, sasa huyo jaji kuna watu anawaona wamesimama na shahidi kizimvani?

Labda huyo naye ni kama Mpina, alikuwa miongoni mwa vichaa wenzake aliowateua kuwa majaji.
 
Huyo jamaa wa jana, alidhihirisha na kuwadharilisha upande wa mashtaka na kuwaonyesha kuwa. Jeshi zima la policcm ni majuha. Kuanzia juu mpaka chini. Hii kesi inawaanika ujuha wao. Wakae watumie mishahara wanayoliowa kupitia jasho la Watanzania.

Hakika tuna serikali mbovu xana tangu 2016 even now.

Wanahitaji ugaidi Tanzania, naimani Mungu atawawezesha kuupata ili wapambane nao vizuri, cos inainekana askari waliosomea hawana kazi hivyo kupelekea kufanya kila njia kujikipu bize.

Mwanakulitafuta mwanakulipata. Mungu tuepushie na MAJUHA HAWA.
 
Leo Jaji kaongea hayo maneno! Je wanasheria kwa uelewa wenu hayo maneno yanaweza kuja kutumika kukatiwa rufaa au kwa sasa hivi kumkataa Jaji?

View attachment 2023472
Wasajiwe kabla ya kupanda kizimbani teknlojia iko juu aweza kuwa na kielektronic gadget akiulizwa swali mtu anamwambia yeye anasikia kwenye ki
microphone chake

Jaji Yuko sahihi
 
Mm ninavyojua sina imani na viongozi wa nchi hii ndiyo wanatuingiza chaka au kaa la moto
 
Wasajiwe kabla ya kupanda kizimbani teknlojia iko juu aweza kuwa na kielektronic gadget akiulizwa swali mtu anamwambia yeye anasikia kwenye ki
microphone chake

Jaji Yuko sahihi
Atakuwa amekipata wapi hicho kifaa wakati siku zoote yupo Magereza?

Bottom line kesi hii ni ya kubambikwa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
KWANINI JAJI ASIONE KIBAO KINAWAGEUKIA,JAMAA ANATIRIRIKA UKWELI MTUPU.
Matata: tuje sasa Safari ya 9/8/2020, Je ilikuwa ni Safari ya Kuelekea Wapi

Shahidi: Sifahamu Kuwa tulikuwa tunaelekea Wapi, walifungua Milango wakanipandisha Nikiwa Nimewekwa Katikati, Goodluck akiwa ananigusa na Bastola akisema Kwamba Nikileta Ujanja Ujanja watanipoteza.

Shahidi: Baada ya Kufika Wao walitangulia kushuka, Mimi nikiwa Ndani ya Gari, baada ya Muda nikasikia Sauti Mshushe huyo, Baada Kuingia Ndani nikafahamu kwamba Tupo Kituoni, Aliyekuwa amenikamata Suruali nilikuwa Namfahamu, Akaja Jumanne akanipa kikataratasi

MATATA: twende taratibu

Shahidi: Alikuja Jumanne hadi nilipo, Akanipa kikaratasi akaniambia kuanzia leo wewe utaitwa JOHNSON JOHN

Matata: Ile Safari ya kwenda Mpaka Kwenye Kile Kituo Mlikuwa Watu wangapi

Shahidi: Shahidi Siwezi Kukumbuka watu wangapi ila najua Mahita aliyekuwa amenishika, Jumanne aliyeniletea Kikaratasi..

Matata: Baada ya Hapo

Shahidi: Alikuja Kuniambia Askari Mmoja Baada ya akimuuliza Hapa ni wapi? Akasema Kwamba hupajui Enhe, Utapajua tu na utasema yote mbona.. Baada ya Muda Mfupi alirudi kaanza Kuniuliza particular zangu, naitwa nani na natokea wapi..

Shahidi: Nikiwa Kituoni walikuja Wote kwenye sello Yangu Goodluck, Mahita, Jumanne na Kingai

Matata: Baadae Ulikuja Kufahamu ni Kituo gani Cha Polisi

Shahidi: Baadae nilikuja Kufahamu Kwamba Pale ni Kituo cha Polisi Mbweni

Shahidi: Nikawa naongea naye pia Nikamwambia kwamba nilikuwa Mwanajeshi Kutoka 92KJ

Matata: Ukisema 92 unamaanisha nini

Shahidi: Kikosi cha Jeshi 92. Kikosi cha Makomandoo hicho

Matata: Akasemaje

Shahidi: Kama wewe ni Komando basi Mmeshafika watatu hapa

Matata: Akaendelea Kusemaje

Shahidi: Akasema Mmoja Umekuja naye wewe na Mmoja kaletwa Muda Mrefu, Nimeongea naye kasema ni Luteni wa jeshi Kutoka KJ92 Komandoo..

Matata: eh!

Shahidi: Akasema Kwamba kuna Mwingine pale nimempita pale yeye hanisemeshi kakaaa tu Pembeni, Nikamwambia kwamba waambie Mimi nipo hapa.. Akarudi akasema sawa ila Denis Urio anasema kwamba aliwatafutia kazi kwa nia njema tu haya mengine hayajui yametokea wapi
 
[emoji16][emoji16][emoji16]jaji kapangwa.
Mbona yule aliyeingia na nondo hakuwa na wasiwasi nae?
 
Mna visingizio sana tulieni dawa iwaingie maana mlitamba sana mama anaupiga mwingi.

Mkome kabisa tabia ya kuingilia mahakama.
Wewe unaona kweli ni kazi ya jaji kusema shahidi anapewa majibu wakati mawakili wapo. Kizimba kimekaaje hasa kuruhusu hali hiyo.


Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Simply jaji haamini shahidi anachoongea, yani kwa maana nyingine jaji kaamua kuweka "objection" kuwasaidia mawakili wa serikali, hii kesi iishe tu, mahakama ya rufaa ndio kimbilio lililobaki
Ni kama ametiwa hofu na huo ushahidi. Ukiusikiliza hauoni chembe ya kudanganya na hata akiambiwa arudie atasema yale yale. Huenda jaji ameshangazwa na hilo hadi asiamini kinachotokea.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Jaji lengo lake ilikuwa kumtoa shahidi kwenye mtiririko
 
Mimi sidhani kwamba haamini, ninadhani kuwa shahidi katoa maelezo mazuri na kwa ufasaha hadi jaji akahisi kuwa anafundishwa majibu, inshort jaji alitamani Ling'wenya avurunde, ndio maana baada ya kuona majibu ni mazuri akaweka pingamizi.
Huenda pia alifurahishwa na mtiririko mzuri hadi asiamini na kusema vile. Kwa walimu wanajua hali hiyo mwanafunzi anapofanya vizuri sana watohoji hivi wewe hukuwa na majibu kweli.

Tusimkumu tu kwanza.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom