Kauli ya Julius Malema kuhusu kifo cha Malkia Elizabeth inasikitisha na kuhuzunisha

Kauli ya Julius Malema kuhusu kifo cha Malkia Elizabeth inasikitisha na kuhuzunisha

Haya majitu ya ANC yote ni Marxists watupu. Najuta siku zote kuyapigania yajitawale. Yamerithi nchi tajiri kupita zote Latin America na bara la Africa lakini kuna ziki sana huko kwao S Africa kwa sababu ya vinyongo vyao kwa Ulaya na Marekani.
Malema sio ANC.
 
Siyo suala la kufurahia kifo chake, bali kuonesha uhalisia wa historia aliyoitengeneza yeye mwenyewe.
uko sahihi kabisa 100% ndiyo maana historia yako itakuhukumu kama ulifanya mabaya tutakukumbuka kwa ubaya wako kama umefanya mema tutakukumbuka kwa wema WAKO , ndiyo maana jino la Patrick Lumumba lilizikwa kwa heshima zoote DRC......
 
Alichoandika ni ukweli ila kwakuwa tunapenda unafiki basi sawa.
Ila Julius Malema anafaa kuendelea kuwa mwanaharakati siku akipewa uraisi ataiua S.A kabisa.
Julius Malema hana hadhi ya kuwa hata diwani. Akipewa Urais yule hakai hata mwaka kwa S.A ilivyo, ni mwehu kwa vitu vingi sana
 
Wakoloni walikuwa wabaya, lakini tawala nyingi za Afrika, ni afadhali ya wakoloni.

Leo hii, kimbilio la Waafrika wanaodhulumiwa na watawala, imekuwa kwa wakoloni. Tukitaka kujenga barabara, madarasa, vituo vya afya, kwa kwenda kuomba ni kwa wakoloni. Kule Seychelles, kuna kisiwa, wananchi wake wamegoma kuwa taifa huru, wameamua kuwa sehemu ya Ufaransa.

Afrika Kusini iliyokaliwa na makaburu kwa miaka mingi ndiyo nchi yenye uchumi mzuri kuliko mataifa karibia yote ya Afrika.

Kumlaani marehemu, ambaye mpaka kifo chake, serikali imeendelea kuyasaidia makoloni yake, siyo uungwana. Kama tusingekuwa wanafiki, tulistahili kuwalaani watawala wetu, waafrika wenzetu, ambao wanajiona ni bora zaidi kuliko wananchi wenzao, hasa wale wenye fikra tofauti na zao.

Queen Elizabeth, na marehemu wengine wote, Mungu mwenye huruma, kwa yale mazuri waliyoyafanya kwaajili ya hinadamu wenzao, awajalie pumziko jema na furaha ya milele. Sote tu mavumbi, mavumbini tutarudi.
 
Amewaza kama mimi kwa asilimia 100.
Jamaa sio mnafiki wala mpigania tumbo lake kama hawa, jamaa haendekezi siasa za majitaka kuchafua wenzake ili apate umaarufu kama walivyofanya hawa kwa Lowasa.

Jamaa hana muda wa kuwalaghai wafuasi wake kuwa anapambania masilahi yao afu nyuma ya pazia anakwenda kulamba asali kama hawa. Kifupi jamaa hufanya siasa zenye kueleweka na husimamia kile anachokiamini na kamwe hajawahi kunadilika badili kama hawa wa kwetu.
 

Attachments

  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    24.9 KB · Views: 4
  • images (31).jpeg
    images (31).jpeg
    15.7 KB · Views: 4
Kwenye Nchi za Watu wanaojitambua, hiyo statement ya EFF ipo on point. Anapofariki Mtu kama queen Elizabeth ambaye alikuwa kiongozi kila kilichofanyika kwa macho yake kinaanikwa hadharani, hakuna haja ya ku-sugarcote. Wanaopaswa angalau kufunika kombe labda ni statement ya Serikali. Watu kama Malema wanatakiwa kuwepo ili kukikumbusha kizazi kuwa kuna wakati tulipitia kipindi kigumu sana. Ukisoma historia ya Kenya kuhusu ukoloni wa Waingereza inasikitisha sana. Nafikiri Tanzania hatukupata uzoefu wa aina hiyo kutoka kwa Waingereza ndiyo maana tunashangaa statement ya EFF.

Historia huwa haina kulemba kwa sababu yalitokea, na wanayoyaeleza yaliyotokea hawana uwezo wa kutia mkono kueleza vinginevyo
 
Wadau hamjamboni nyote?

Alichoandika Malema muda mfupi uliopita kinahuzunisha sana hususani wakati huu wa msiba mzito wa Mkuu wa Taifa la Uingereza na Jumuiya ya Madola

Hebu someni wenyewe alichoandika:

"We do not mourn the death of Elizabeth, because to us her death is a reminder of a very tragic period in this country and Africa's history.... If there is really life and justice after death, may Elizabeth and her ancestors get what they deserve."

Binafsi sijafurahishwa na kauli yake ambayo kimsingi inatakiwa kulaaniwa dunia nzima.

Namuombea kwa Mungu apumzike kwa amani kiongozi wetu wa Jumuiya ya Madola.

Vita amevipiga na mwendo ameumaliza.

View attachment 2350759
Wakati waafrika wakinyanyaswa kama mbwa kwenye nchi zao Zimbabwe na Afrika kusini Uingereza iliunga mkono tawala zile katili.

Kwa anayejua machungu waliyopitia wenzetu huko hawezi kuushangaa msimamo wa Malema.

Nami naiunga mkono kauli yake
 
Mazuri yzo mbona huyasemi? Wa.mewaletea shule hospitali na teknolojia kibao zinazowanufaisha lakini kutokana na upambqvu wenu bado mko kwenye lindi la umaskini wa kutupwa halafu unasinguzia wazungu!

Hao watumwq, mlikuwa mnakamatana wenyewe . Mikataba mibovu .mnayoingia inatokana na ujinga wenu halafu mnalaumu wazungu.

Hata leo hii ikipigwa kura kwa uwazi waafrika wengi watachagua kurudi kutawaliwa na wazungu.. wakoloni wameondoka zaidi ya miaka sitini lakini failure zenu bado mnawatupia wazungu.
Hakuna mazuri yanayoweza kuhalalisha uovu dhidi ya wengine.
Ni ujinga wa kiwango cha juu kubadilishana uovu na unayoyaita mazuri.
 
Matatizo ya waafrika yanatokana na waafrika wenyewe kwa kuendekeza unafiki, ubinafsi uliopitiliza, kujikomba, uchawa, uzandiki, uzembe, kutowajibika, tamaa, poor reasoning, poor innovation, na mambo ya hovyo hovyo kama ulozi, kucheza mangoma na kushinda kwenye vilabu vya pombe za kienyeji. Mzungu anafanya ambacho anaona ni sahihi kwake kwa ajili ya maslahi yake na kizazi chake.........poor Malema!​
 
Mawazo ya sampuli yake ni sawa mtu kuwa nayo, lakini kuyaleta wakati huu ni kutafuta umaarufu usiokuwa na maana, kwangu siku zote kuipiga teke maiti ni upungufu wa akili kwa yule anayeipiga.
Nakazia," kupiga teke maiti ni upungufu wa akili"
 
Kwenye Nchi za Watu wanaojitambua, hiyo statement ya EFF ipo on point. Anapofariki Mtu kama queen Elizabeth ambaye alikuwa kiongozi kila kilichofanyika kwa macho yake kinaanikwa hadharani, hakuna haja ya ku-sugarcote. Wanaopaswa angalau kufunika kombe labda ni statement ya Serikali. Watu kama Malema wanatakiwa kuwepo ili kukikumbusha kizazi kuwa kuna wakati tulipitia kipindi kigumu sana. Ukisoma historia ya Kenya kuhusu ukoloni wa Waingereza inasikitisha sana. Nafikiri Tanzania hatukupata uzoefu wa aina hiyo kutoka kwa Waingereza ndiyo maana tunashangaa statement ya EFF.

Historia huwa haina kulemba kwa sababu yalitokea, na wanayoyaeleza yaliyotokea hawana uwezo wa kutia mkono kueleza vinginevyo
Sawa mkuu je Mr.Malema alitoa tamko kama hilo baada ya King wa wazulu kufariki dunia?,maana naye hakua clean kwenye maisha yake, alitoa kauli iliyosababisha wageni wa kiafrika kuuawa,afriphobia yenye mchanganyiko wa xenophobic, King wa wazulu amehodhi almost ardhi yote ya Ile province but malema amefyata mkia wake, reason wazulu sio target rahisi ila queens!,malema haishi manzese au tandale au kinondoni shamba, anapiga kelele na mwisho wa siku anakimbilia kwenye makazi ya wazungu yaliyo chini ya opposition party, DA maana kuko smart na safe, why assisting kule seshogo, alex?
 
Back
Top Bottom