Bora ungekaa kimya.
Huna evidence ya blacks kuwauza wazungu utumwani
Mkuu ushahidi upo mwingi, kasome kuhusu
THE BARBARY SLAVE TRADE utajionea majanga. Waliohusika ni waislamu waliotoka uhuspania (Muslim Spain) baada ya kufukuzwa na Malkia Isabella na mume wake. Wengi wao kati ya wauza watumwa walikuwa ni Arabs and Berbers, ambao waliishi maeneo ya Morocco, Tunisia, Algeria na Libya.
Japo ukweli ambao wanakataa kuusema ni kwamba kwenye Barbary Slave Trade hata watumwa weusi (Bantu) kutoka Afrika Magharibi walikamatwa na kuuzwa pia, siyo wazungu peke yao. Ambacho napingana na watu ni kusema
The Barbary Slave Trade ndiyo utumwa mbaya kuwahi kutokea duniani. Hili halina ukweli hata kidogo. Utumwa wa Bahari ya Atlantiki (The Atlantic Slave Trade) hauna mfano mpaka leo hii....
Ambacho watu wengi wanakisahau ni kwamba mataifa ya Ulaya kama Uingereza, Ufaransa, Uhispania na Ureno yamefika hapa yalipo leo kwasababu ya biashara ya utumwa na ukoloni . Nikupe mfano hai tu, mwaka 2013 kama sikosei kuna familia imekuwa tajiri nchini Uingereza kwasababu wamelipwa fidia na serikali ya Uingereza. Fidia hii ilidumu kwa zaidi ya miaka 200, ambapo meli za familia hiyo zilizosafirisha watumwa zilipata hitilafu na kuzama. Sasa wamelipwa mamilioni ya fedha kipindi hiki ambacho utumwa ni biashara haramu (Hebu fikiria).....
Wakati Uingereza wanavamia India na kuanzisha koloni (The British Raj), taifa la India lilikuwa linachangia zaidi ya asilimia 40% ya GDP ya dunia hii. Lakini wakati wanaondoka waliicha India ikichangia asilimia 4% tu ya GDP. Takwimu za kitaalamu zinasema tokea mwaka 1740-1947 Uingereza imechota nchini India peke yake utajiri wa dola za kimarekani zaidi ya Trilioni 40. Huu utajiri uliwawezesha waingereza kuwa na utajiri wa ziada (Surplus Capital) ambao ulidumu kwa miongo mitatu hata baada ya Ukoloni kuisha nchini India na Pakistani.....
Ikumbukwe kufika mwaka 1923, Uingereza ilikuwa inamiliki asilimia 23% ya ardhi ya dunia yote pamoja na watu wake. Hii ni karibia na robo ya ardhi ya dunia. Hebu tujiulize walichota utajiri mkubwa kiasi gani hawa watu. Halafu kuna watu wanadhania haya ni mambo madogo tu, lakini ukweli ni kwamba madhara ya ukoloni yapo mpaka leo na yataendelea kuathiri vizazi vingi vijavyo. Kuna faida nyingine ya ukoloni ambayo dunia imeipata japo hawataki kuizungumzia, ni hii hapa:
Bila makoloni,
The Allied Powers (Uingereza, Marekani na Urusi) wasingeshinda kabisa vita ya pili ya dunia. Makoloni ndiyo yalichangia wanajeshi na rasilimali ambazo zilisaidia kuendesha mtambo wa vita (War Machine) wa nchi za Magharibi. India peke yake ilitoa wanajeshi wasiopungua milioni mbili na laki tano (2,500,000). Wanahistoria wanasema Mfalme George wa Uingereza alipoenda kukagua gwaride la kijeshi kwenye koloni la India alitembea kwa mguu kwa masaa yasiyopungua matatu. Hebu fikiria jeshi lilikuwa ni kubwa kiasi gani.....Sasa hapo bado wanajeshi kutoka Afrika.....
Hili jeshi la India ndiyo lilikuwa jeshi la kwanza kabisa kuweza kulipiga jeshi la Japan (The Imperial Japanese Army) ambalo ndilo lilikuwa jeshi bora kabisa duniani kipindi hicho. Oparesheni hii ya kijeshi iliitwa U-GO
(Operation U-GO), ambapo wajapani walishindwa kabisa kuvamia India huku wanajeshi 53,000 wa Japani wakiuwawa na kupotea. Marekani na Uingereza wote na silaha zao nzito, walishindwa kupambana na Japan kule Pasifiki, lakini wanajeshi wa India na Nepal wenye silaha duni waliweza. Kama India ingeunga kwa Ufalme wa Japan, sidhani kama Mataifa ya Magharibi yangeshinda vita ya dunia kirahisi........
MWISHO KABISA: ukoloni wa Uingereza umeliachia taifa la India kovu ambalo sidhani kama litapona. Mpaka leo hii India ndiyo nchi inayoongoza kwa watu wengi kuumwa ugonjwa wa kisukari (It's A World's Diabetes Capital). Unafahamu tatizo ni nini ???
UKOLONI WA UINGEREZA. Mwaka 1943 wakati vita ya pili inaendelea Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchill aliwanyang'anywa wahindi mazao yao ya chakula na kuyapeleka Ulaya kwenye vita na nchini kwake, huku akiacha wahindi wakiwa hawana chakula. Njaa ilizuka na walikufa wahindi wasiopungua milioni 4, huku mamilioni wakiumwa magonjwa hatari. Waziri Mkuu wa Uingereza alipoulizwa akasema "
Ni nani aliwaashauri wahindi wazaliane kwa wingi kama sungura"
Madaktari wa India baada ya kufanya tafiti wamefahamu kwamba ile njaa ilisababisha mabadiliko makubwa kwenye seli (Massive Genetic Alteration/Mutations) za wahindi wengi, kitu ambacho kilipeleka wahindi wengi wawe na kisukari cha kurithi. Mpaka leo hii vijana wadogo wanakufa, huku wakina
Harry Windsor na
Merghan Markle wanakula bata tu kule Marekani......
Anyone who downgrades slavery, colonialism or any form racial oppression is suffering from a very dangerous malady called Megalomania......