Mkuu Bujibuji, sio kwamba wamekosa sifa. Kama ni umri angalia Ali Hassan Mwinyi alikuwa na umri gani alipokuwa Raisi wa Tanzania. Kina Joe Bidden wana umri gani?
Haki ya umri aliyo nayo Magufuli ni katika kuunda baraza lake la mawaziri. Ana uhuru wote hapo, hata kuchagua mawaziri wanaovalia suruali matakoni. Lakini suala la raisi ajae atakuwa na umri gani sio lake kabisa, ni la CCM na wananchi kwa ujumla.
Suala la umri Magufuli anatumia kama kisingizio tu cha kutaka kuwaondoa Kabudi na Lukuvi mapema kwenye kinyang'aniro cha raisi ajae ili amtengenezee njia mtu wake. Sasa utaona reaction ya chini chini ndani ya CCM, na pia reaction ya Kabudi na Lukuvi. Ni vita!