Kauli ya RC Chalamila ''Mtu akifia Polisi wanasema polisi kaua, lakini ikiwa ni hospitali ni mipango ya Mungu'' siyo ya kiungwana

Kauli ya RC Chalamila ''Mtu akifia Polisi wanasema polisi kaua, lakini ikiwa ni hospitali ni mipango ya Mungu'' siyo ya kiungwana

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Akiongea wakati wa kukabidhi magari manne ya wagonjwa kwenye hafla iliyofanyika Hospitali ya Rufaa ya Amana wakati wa hafla ya kukabidhi Chalamila amesema "Hii sekata ina Umungu ndani yake, leo nikifa mikononi mwa Polisi watu watasema Polisi wameuwa, lakini Hospitali wanasema ni mipango ya Mungu"

Chalamila amesema kutokana na umuhimu wa sekta ya afya kuwa ya kipekee mtu hata akifa Hospitalini ndugu sio rahisi kwenda mahakamani kulalamika tofauti na mtu anaefia mikononi mwa Jeshi la Polisi watu uenda Mahakamani.

1000005278.jpg
 
Mh rais anapaswa kutambua kabisa kuwa huyu bwana ni mtu aliyechanganyikiwa,hafai kabisa kuwa RC,mbona nchi hii ina watu wengi tu wenye sifa za uongozi,hafai huyu mtu,sasa na sisi walimu tuanze kuuwa wanafunzi wetu maana hospital pia wanakufa, mtu hajui tofauti kati ya kituo cha polisi na hospital,huyu hafai kuwa kiongozi
 
Washauri wanamuyumbisha Rais kwenye maamuzi. Alikuwa amechukuwa uamuzi sahihi wa kumpumzisha huyu mropokaji, sijuhi ni nini kilimshawawishi kumrudisha huyu mtu aliyeweza kuongea na jpm akiwa marehemu!!!
 
Back
Top Bottom