Kauli ya Samia 'Who are You' ilikuwa siyo ya kiungwana wala kidiplomasia, tunatengwa na dunia

Kauli ya Samia 'Who are You' ilikuwa siyo ya kiungwana wala kidiplomasia, tunatengwa na dunia

Katika dunia ya sasa yenye msukosuko wa mawazo na taarifa zinazokuja kwa kasi, tunahitaji kukumbuka mambo ya msingi. Watu wanahitaji amani kuliko fujo, kwa sababu amani inatupa nafasi ya kuishi vizuri, kufanya kazi, kutafuta riziki, na kufurahia maisha bila hofu. Vijana tunahitaji mwelekeo na akili ya kutafakari kuliko kauli za uchochezi, kwa sababu bila mwongozo sahihi tunaweza kupotezwa na hasira za muda mfupi na kuharibu mustakabali wetu wenyewe. Nchi yetu inahitaji umoja kuliko mgawanyiko, kwa sababu tukigawanyika tunapoteza nguvu yetu kama taifa, lakini tukikaa pamoja tunakuwa na uwezo wa kushinda changamoto nyingi kuliko tunavyodhani. Hii ndiyo nguvu ya utashi wa kibinadamu, kuchagua kilicho bora, kutanguliza utu, na kulinda amani inayotuwezesha kuendelea kusonga mbele.
Amani ya kufunga wapinzani,better shut up
 
Katiba yetu ni takataka, yaani mtu mmoja kwa ujinga wake tu anatukost watu ml 62+...hiii ni maajabu!!.
Achilia mbali maisha ya watu kupotea oct 29!.
Ila wabongo bwana si nyie ndo mlishitaki kwa kuawaandika mabarua, mkawatag kwenye mitandao, mkasifia CNN na kibara wao Mkenya Lary. Mlitegemea matokeo gani. Jana mmemshangilia mange kwa ujinga wake mwingine now mnalaumu katiba. Si katibaa hii hii iliwaleta hao wanaotaka kuondoka... Si ni katiba hii ilijenga diplomasia ??

Mliyataka tulieni dawa iingie siku nyingine fikirini nje ya box kabla ya kushikiwa akili na wapumbavu wachache.
 
Hebu rudia tena kusoma ulichoandika.
 
Kauli yako inali-cost taifa, kila nchi inafanyia review uhusiano wetu, walianza USA, EU, Sweden leo Canada hatujui nani watafuata, soon athari zake tutaziona kwenye uchumi.

Maadui tulionao, ujinga, maradhi, umasikini, siasa safi na CCM, wanatutosha, kauli zako zisituongezee maadui wengine.

Ulitukuta na marafiki zetu wadau wa maendeleo tangu tupate uhuru, wanatusaidia kwenye bajeti, miradi, diplomasia, tafadhali tuache nao salama siku utakaporudi Kizimkazi, sisi Watanganyika hatuna wajomba wa Oman kwamba watatusaidia.
Huu uhusiano ni kwa Tanganyika tu au mpaka Zanzibar
 
Dunia imeikataa tanganyika
harambee na michango ya ccm labda zitaokoa jahazi tutakuwa kweye uchumi wa kati

mama anaupiga mwingi
mama anafungua nchi
mama nywe nywe nywiny nywiny kmynk

Ngoja niendelee kuvuta ganja hapa nimesahau hata mada inahusu nini
 
Maneno ya ubabe kama yale hata Putin mwenyewe au Xi Jinping hawezi kuyasema hadharani! Sasa yeye sijui alipata wapi ujasiri. Nadhani lack of exposure imechangia.

Dunia ya leo inahitaji matumizi makubwa ya akili, maarifa na ujuzi! Na siyo vichambo na majigambo yasiyo na kichwa wala miguu. I think you will understand me Madam Who are you?
Kuna jambo watu tunashindwa kuelewa Hawa watu wa ngozi nyeupe ni wakorofi ndiyo lakini ndani yao Wana roho ya utu ukilinganisha na waarabu au wachina
European wao wapo radhi kuchangia huduma za kijamii kama wahisan tu lakini sio kwa mchina, Mrusi au Muarabu hivi viumbe vitatu ni namba nyingne wao wapo kwa ajiri ya faida tu hasa huwa wanalenga kwenye biashara
Wapo radhi waje nchini kwako wafanye biashara ila sio kwa ajiri ya kukupa ufadhiri katika jambo fulani
 
Kauli yako inali-cost taifa, kila nchi inafanyia review uhusiano wetu, walianza USA, EU, Sweden leo Canada hatujui nani watafuata, soon athari zake tutaziona kwenye uchumi.

Maadui tulionao, ujinga, maradhi, umasikini, siasa safi na CCM, wanatutosha, kauli zako zisituongezee maadui wengine.

Ulitukuta na marafiki zetu wadau wa maendeleo tangu tupate uhuru, wanatusaidia kwenye bajeti, miradi, diplomasia, tafadhali tuache nao salama siku utakaporudi Kizimkazi, sisi Watanganyika hatuna wajomba wa Oman kwamba watatusaidia.

Kikwete kamtia kiburi.
Anadhani jumuiya ya kimataifa ni kama sisi watanzania wanyonge, ambao anatuua na kisha kusema mlitaka nifanyaje. Wenzie wanajibu mapigo…
 
Back
Top Bottom