Kauli ya Warioba kuwa Iddi Amin aliua Watanzania wachache kuliko serikali ya Samia; Jeshi lijitazame sana

Warioba kapata wapi takwimu hizo?
Za vita ya dhidi ya nduli zipo na ni rahisi kuzipata kwa sababu zilihusisha vita rasmi na wanajeshi huandikishwa.
Changamoto ipo kwenye vurugu wakati na baada ya uchaguzi October 29, 2025 kwa kuwa wahusika hawana taarifa rasmi, hawakuandikishwa na hakuna nia ya kisiasa kupata ukweli.
Hata hivyo, kutaja idadi yaweza na faida kisiasa kuliko kutotaja kunakoweza kusababisha hasara zaidi.
 
Kama ni sura Halisi ya Shetani na Wikipedia inasema aliua WaTz elfu 5.

Je huyu aliyeua zaid ya elfu 5 tumuiteje?.
Huyu aliyeua waTz 5000 ndiye shetani mwenye mkia mrefu sana.

Vita vya Idd Amini pamoja na ukubwa wake na siliha zote nzito nzito zilizotumika kwa muda takribani wa miezi saba ya moto na miaka miwili ya baridi, viliua wanajeshi 460+ na makaburi yao yapo pale Kaboya yanahesabika.

Sasa huyu wa 5000 makaburi alienda kuzikia wapi?
 

Taarifaza ndani ya Serikali na jeshi, Tanzania ilupoteza wanajeshi 337 kwenye vita kati ya Tanzania na Uganda. LAKINI jeshi la Amin lilidai kuwa idadi hiyo ni ndogo kuliko uhalisia, wakidai kuwa waliwaua askari wa Tanzania 1,000.
Conclusion:
Iwe 337 au 1,000 kama adui alivyodai, bado hiyo idadi ni kidogo sana ukilingamisha idadi ya waliouawa na huyu dhalimu.
Soma hata hii taarifa ya vyombo vinavyojishughulisha na taarifa za kivita:

Tanzania's soldier losses in the Uganda-Tanzania War (Kagera War, 1978-79) were relatively light, with estimates varying, but sources suggest around 373 killed (TPDF) and lighter casualties among the militia, though exact figures are debated, with claims of thousands of Ugandan/Libyan deaths versus fewer Tanzanian losses. While Ugandan and Libyan sides suffered heavily, Tanzanian casualties were considered minor compared to their enemy's, with some reports saying "light" losses, despite initial Ugandan claims of 1,000 Tanzanian dead.
 
Kama jeshi la TZ halitosafisha doa hili kuna hatari wananchi kuja kulidharau kama Waganda walivyodharau jeshi la Amini.

Kitu cha Kwanza Jeshi linapaswa kuingilia kati kuzuia Utekaji wa wananchi. Utekaji umevuka viwango vya kuwa mambo ya kipolisi, sasa hivi limeshakuwa tishio la nchi!
 
Vita vya Uganda TPDF walipata msaada mkubwa kutoka kwa waganda waliochoshwa na Iddi Amin , mgawanyiko ulikua mkubwa na ngome kuu aliyobaki nayo Amin ilikuwa ni askari wachache kijijini kwao Koboko ambapo alikimbilia baada ya kutoka Kampala.

Sasa je leo hii jeshi la nchi jirani likitaka kumuondoa "self imposed ruler " wananchi wataacha kulipa ushirikiano? Ilhali mtu huyu aliyeua maelfu ya watanganyika atakua amebaki na kikundi kidogo cha watu wanaomuunga mkono huku wengi wakiwa wanatoa ushirikiano wa majeshi ya wageni kusonga mbele na kumkaribia?

Historia ina tabia ya kujirudia na haihulizi ila kwa namna yoyote Tangayika ile tuliyoijua ilipotezwa October 29.
 
Wakati wa maadamano ulimuona Wambura akija kwenye TV na kuzungumza operesheni?. Ila tulimuona CDF Mkunda ndo alikuja front. Hii inaonyesha kuwa yeye ndo alikuwa incharge wa vyombo vyote
Wambura alitangaza kwenye tv watu wote wasitoke ndani, kutakuwa na opreration maalum.

Sasa hiyo operataion maalum ndo uliyozaa risasi ambazo zingine ziliwafuata watu majumban mwao
 
Warioba kapata wapi takwi

Warioba kapata wapi takwimu hizo?
Wewe Binti, rank ya Warioba siyo ya kukosa taarifa nyeti za serikali kutokana na nafasi nyeti alizohudumia wakati wake. Rank ya Makamu wa pili wa rais na waziri mkuu siyo vyeo vidogo vya kushindwa kupata nyeti za nchi kwa wakati sahihi. Elewa!
 
it always start as small problem, kuna haja ya kujiuliza kama wazee hawa hawakuona hatari ya mifumo waliyo tengeneza? au wanachotafuta ni kipi hasa?
wao pia walifanya the same wakati ya operation ya vijii vya ujamaa.

 
Hapa tumepata kwa urahisi kabisa iladi ya waliouwawa kwenye vita dhidi ya nduli idd amini.
Wakati na baada ya uchaguzi October 29,2025 waliouwawa wangapi? Serikali na vyombo vya ulinzi vitoe idadi tuondoke kwenye hapo. Vinginevyo kila mmoja atatoa idadi yake na itakubalika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…