Sensei Tai
Senior Member
- May 26, 2022
- 168
- 466
Nakumbuka kuna siku Waziri mkuu alisema wazi kwamba vijana ambao hawana ajira ndio wapewe kipaumbele katika kupata ajira za Sensa
Kwasasa ukipitia mitandaoni utaona kila mtu ni sawa na muamba ngoma ambae huvutia kamba upande wake .
Kuna watumishi wa umma ambao wanajiona wao ni bora sana kiasi kwamba wanahisi wao ndio wanastahili kufanya hii kazi na kuna wale vijana ambao ni graduates na hawana ajira ambao pia nao wanaona kwamba hizi kazi ni bora wangepewa wao sababu hawana ajira.
Binafsi naona hizi ajira wangepewa tu vijana ambao hawana ajira sababu inaweza ikawa ndo kama njia ya wao kujipatia angalau mitaji ya biashara.
Watumishi wana mishahara kila mwezi, hata kama ni midogo kiasi gani lakini inawasaidia kuendesha maisha tofauti na kijana ambae hana ajira ambapo kwake kila kukicha ni afadhali ta jana.
Nina inani kabisa kwamba serikali yetu ni sikivu na itaenda kutenda haki.