Kauli za kuwaita mawaziri wapumbavu ama nonsense zitafutwa na Katiba Mpya

Hata katiba mpya ikiwepo mawaziri wataburuzwa na kutukanwa tu. Ni masuala ya kibinadamu zaidi.
Hoja yangu ni kwamba umungu mtu wa rais ukipunguzwa waziri atakuwa huru kutumia utashi wake wa kujiuzulu ama kubakia ktk nafasi yake endapo patatokea misigano kati yake na rais.

Lkn kwasasa wanogopa kushughulikiwa
 
Hivi kumbe bila Sukari maisha yanakuwa hatarini. Kweli mwanadamu na mazoea. Najua hata siku kukosekane Majani ya chai kutachimbika
 
Kutukana au kutoa lugha kali mtu anapoghafilika ipo sana tu kwa watu wengi, hata huyo waziri huenda huwa anawakaripia watendaji wa chini yake, sasa kwa rais inakuwaje ajabu kutoa lugha kali endapo kuna jambo limefanyika kinyume na alivyotarajia.........hata mwalimu Nyerere alikuwa anachukizwa balaa hadi unaona sura inabadilika, Mkapa hivyo hivyo, kikwete na Magu, labda mzee ruksa ndo ulikuwa huoni akionyesha sura ya ukali au kuongea lugha kali.......kwa hiyo leteni jingine, siyo kukomaa na jambo ambalo halina mashiko yoyote.​
 
Ndiyo hajabwaga manyanga sasa unafanyaje?
 
Point kubwa sana umeongea
 
Ndiyo hajabwaga manyanga sasa unafanyaje?
Mtoa mada kalisemea hilo.

Kubwaga manyanga kwa siasa za Tz, kwa watawala inatafsiriwa kuwa ni kiburi na majigambo na si kuwajibika kisiasa na mifano ipo.

Angalia wale wazee makada wa sisiem waliojiondoa kwenda upinzani walichukuliwaje?

Utatengenezewa zengwe wewe hadi basi bila sababu za msingi!

Ndiyo maana wateule wote pamoja na yote ya udhalilishaji wa kinyadhifa wanaofanyiwa, hawaondoki wanamuangalia mteuzi wao atakavyoamua!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachojua kuanzia awamu ya 5, tumeshuhudia unyumbu kwenye uongozi serikalini, 'herding behaviour', Herding behaviour is an occurrence of thoughtful people suspending their individual reasoning because of fear, in this case fearing their leaders
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…