Kama kuna mtanzania anadhani hilo li nonsense ni kwa ajili ya waziri basi amepotea.
Hilo tusi ni la jumla jumla kwa baraza zima na watendaji woote na wananchi
Muwage mnacomment kwa kuchuja habari kwanza.
Chukua hotuba ya waziri Mkenda inayozungumzia masuala ya mashamba ya miwa, viwanda vya sukari, uhaba wa sukari na utaratibu wa uagizwaji na uingizwaji wa sukari.
Ukitoka kuisikiliza hiyo, chukua hotuba ya rais Samia aliyoitoa Chato wakati wa ziara ya rais M7, utaelewa dhahiri mtoa mada alichomaanisha.
Tukichukulia sura ya rais na baraza lake la mawaziri ni mfano wa familia moja ya ndoa, mtu na mke wake kiutendaji.
Hatutegemei mke wa mtu azungumze jambo, halafu baadaye atoke mumewe hadharani kuliponda ama kulikanusha jambo hilo!
Majirani tutashangaa na kuona dosari iliyo wazi katika familia hiyo!
Haiwezekani jambo moja linalopikwa katika chumba kimoja likatoka na maelezo tofauti ya msigano!
Kwa mantiki ya mfano nilioutoa ni kwamba waziri hawezi kukurupuka kutoa msimamo wa serikali bila baraka za rais, never on earth!
Ikitokea msigano wa wazi hivyo, yampasa waziri kujitathimini na kubwaga manyanga ili kulinda hadhi yake!
Sent using
Jamii Forums mobile app