Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Hapa kuna tatizo. Si kawaida Rais, Waziri Mkuu na Waziri kutofautiana wakati wote wanatumikia serikali moja na wana kila fursa ya kuweza kuwasiliana kabla ya kutoa msimamo. Naona hapa Rais amechemsha kweli kweli. Anaonyesha alivyo mtupu kwa kiwango kikubwa. Nadhani ingekuwa vizuri wahusika wote wajiuzulu. Nasema hivi kuepuka mmoja kutumia mamlaka yake kuwaumiza wengine. Hapa kuna tatizo. Rais hata hajui sheria inasema nini! Je anapata faida gani au amepewa kitu au hii biashara ni ya watu wake au ndugu zake?Katiba yetu inampa Rais mamlaka makubwa sana nchi hii. Rais ni kama Mungu kwa mujibu wa katiba yetu.
Mawaziri wanatwezwa lkn hawana cha kufanya. Wakijuzulu "mungu" anaweza kutafsiri hatua hii kama dharau na kuamua kuwashughulikia. Wanalazimika kuipokea kauli ya "mungu mtu" kwa mikono miwili.
Rais Magufuli aliwaita mawaziri Dr. Philip Mpango na Prof. Kabudi WAPUMBAVU mbele ya hadhara. Wakapokea kauli hii kwa mikono miwili. Sote tukabakia tumeduwaa. Ni kwasababu hawakuwa na la kufanya mawaziri hawa. Walimwogopa "mungu" na malaika wake
Rais Samia ametamka hadharani kwamba uamuzi wa Prof. Mkenda kuzuia sukari toka nje ni NONSENSE. Sote tumebaki tumepigwa na butwaa. Hana la kufanya Prof. huyu akirogwa kujiuzulu "Mungu" ama malaika wake watamshughulikia.
Tuiangalie upya Katiba yetu inayomjenga mtu kuwa "Mungu".