Kauli za LATRA kuhusu namba za magari, kuelekea 17 Machi zimelenga kumhujumu Mama?

Kauli za LATRA kuhusu namba za magari, kuelekea 17 Machi zimelenga kumhujumu Mama?

Kumekuwa na matamko tata kutokea LATRA kuhusu magari yenye namba D na E kufanywa ndiyo yaliyo magari pekee.

Hali hii si ya kuvumiliwa hata kidogo. Kesho itakuwa gari kuingia Dar na labda hata kuthubutu tu kuwapo Tanzania ni F na G peke yake. Nani ajuaye?

Ni kawaida kwa wanaojidhania kuwa wako salama au kuwa haiwahusu kuonekana wakikenua (meno nje) wasijue ukiukwaki wa haki za wengine ni sawa na kula nyama ya mtu.

"Taratibu haitakuwa magari ya abiria peke yake, kama tukichagua kukaa kimya."

Kwani kwenye gari kinachogomba ni namba za usajili au ubora wake? Vipi kama mtu alinunua gari lake zamani akaamua kuliweka ndani bila kulitumia hata kwa miaka 20? Hilo nalo LATRA hawalitaki?

Kwanini LATRA wangependa watu kununua magari mapya (kama mazuzu tu) hata kama waliyo nayo ni mazima? Au kwanini LATRA wangependa wamiliki wa magari kuyatupa au kuyaondoa magari yao kimkumbo mkumbo tu hata kama ni mazima?

Kwani LATRA wamekuwa na maslahi gani kwenye biashara ya magari? Kwamba wamekuwa madalali, washirika au wauza magari? Kwani hata magari haya yanatengenezwa hapa nchini? Vipi kuwa mawakala wa mabeberu?

"Ikumbukwe kununua gari au chochote na hasa inapokuwa si kutoka kwenye viwanda vya ndani ni kuwaneemesha mabeberu.'

Cuba yenye kutupa sisi misaada, ni moja ya nchi za kizalendo zenye kujua umuhimu wa kutunza kila walivyo navyo; ili kuepuka unyonywaji na hasa huu wa kupitia katika manunuzi yasiyo ya lazima kutoka nje:

View attachment 2934577

Pichani ndiyo yaliyo magari katika ya maana yaliyojazana kwenye barabara bora kabisa za Havana, Cuba. Magari ya miaka 1950s huko. Spares zake zote ni kutokea katika soko lao la ndani.

Huku kufunguliwa kwetu nchi kwa lazima ya kununua nje, ni ili mabeberu yavune yawezavyo, si ndiko alikokupinga sana bwana JPM (RIP)?

"LATRA mnataka magari mapya pasipo na sababu? Vipi, kwani mmeahidiwa nini na nani wenzetu?"

Kwa hakika kuelekea 17 March mnatufanya kumkumbuka sana shujaa wetu yule tuliyembeza wengine bila kujua. Kwa hakika angekuwapo huu upuuzi wa D na E usingekuwapo.

Pumzika kwa amani baba Magufuli uliowaachia nchi leo wanatusukuma kwa mabeberu kama vipi tukakamuliwe kweli kweli.

"Kwa hakika kwa mema tutakumbuka."
Hv ht ukiisoma mwenyewe unaelewa ulichoandika?
 
Hv ht ukiisoma mwenyewe unaelewa ulichoandika?

Wameelewa wangapi? Huoni mwenye matatizo ni wewe?

Angalizo:

Ukienda kwa vinyozi 5 wote wanakunyoa vibaya, chukua muda kukiangalia kichwa chako; yawezekana ndicho chenye nundu!
 
1. Siwezi kufurahia kifo cha mtu. Huwezi kulIona hilo popote.

2. Kwamba nilikuwa na taabu na mengine yake yakiwamo kuhusu corona, chanjo, kutekana, kukandamiza demokrasia nk. Kulikoni nisimbumuke kwa mema?

3. Sang'udi, Manjagata, Etwege na genge zima la Wana chattle tulindane ndugu zangu.

4. Zaidi sana kwenye mada kuko wazi kuhusu hata wale waliokuwa na tofauti naye:

Kwa hakika kuelekea 17 March mnatufanya kumkumbuka sana shujaa wetu yule tuliyembeza wengine bila kujua. Kwa hakika angekuwapo huu upuuzi wa D na E usingekuwapo.

Pumzika kwa amani baba Magufuli uliowaachia nchi leo wanatusukuma kwa mabeberu kama vipi tukakamuliwe kweli kweli.

"Kwa hakika kwa mema tutakumbuka."

5. Kulikoni kuniwekea mihemko isiyokuwa yangu ndugu?
Nadhani utakumbuka nilivyokuwa nakuasa kuwa JPM atakumbukwa kuliko waliomfuatia Mwalimu. Nitakuletea hapa comments hizo hapo baadaye. Ila barikiwa kwa kuliona hili. Bado akina Retired na wenzake
 
Haya ndio matokeo ya watz kutokujitambua na kupenda ushabiki au uchawa badala ya kuwakemea watawala ambao kila kukicha hubuni jinsi ya kuwanyonga na kuwafanya wazidi kuwa maskini
 
Siyo kweli mkuu.

Hilo tangazo ni rpute mpya ya magari yanayoingia Mwenge Stendi.

Siyo kwa magari yote kaka.
 
Nadhani utakumbuka nilivyokuwa nakuasa kuwa JPM atakumbukwa kuliko waliomfuatia Mwalimu. Nitakuletea hapa comments hizo hapo baadaye. Ila barikiwa kwa kuliona hili. Bado akina Retired na wenzake

1. Ninao uhakika hutaiona yangu moja yenye tuhuma yoyote dhidi yangu kama ulivyoziweka hapa.

2. All in all JPM asingekubaliana na upuuzi huu.

3. Kwa hakika katika mema: "atakumbukwa kama kwa yale mengine.

4. Maisha ni hadithi.

Uwe na siku njema.
 
Kama tatizo ni rushwa kwanini TAKUKURU au serikali wangali ofisini?

Mawazo yangu "mwanzo wa ngoma ni lele." Tusipokomaa kesho itakuwa F na G. Keshokutwa magari yote yakiwamo binafsi.

Muda wa kuwakomalia ilikuwa sasa. Tusikubali haki ya mtu yeyote kuchezewa.

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote

Walapo nyama ya mtu huwa hawataachi.
Mtaburuzwa sana sababu hamjui haki zenu endelezeni uchawa kama ndugu yenu mwashambwa
 
Ni namna ya kivivu ya kufanya kazi.

Njia sahihi ilikuwa kukagua gari, lakini LATRA wanajua itatembea rushwa na kila gari itakayokaguliwa itaonekana inafaa.

Kwahiyo kukata mzizi wa fitna ni kumaliza tatizo la rushwa, jambo ambalo ni 'unrealistic'.

Mwisho wa siku wanalazimika kwenda na hiyo short-cut ya kivivu ya kuyachuja magari kwa namba za usajili (uzee).
Tanzania ina shida, uchakavu au uzamani wa gari hautegei namba ya usajiri bali mwaka ambao chombo hicho kimetengenezwa pamoja na matumizi/matunzo
 
Siyo kweli mkuu.

Hilo tangazo ni rpute mpya ya magari yanayoingia Mwenge Stendi.

Siyo kwa magari yote kaka.

Mada umeisoma? Mwanzo wa ngoma ni lele. Unajua hili wakifanikiwa wataishia wapi?

1b847c_5415749b717047fd87eb26fac9310d1a_mv2.jpg

Kama magari ya miaka 1950s yanatembea America sisi nani?

Ubora wa gari ni namba ya usajili?
 
Mama yenu kila kitu anahujumiwa, nini maana ya kuwa mama sasa??!!, ana macho kila mahali lakini haoni, ana masikio kila mahali lakini hasikii, ni kipofu na kiziwi, hatoshi hapo alipo. Hii nchi haiwezi kuendeshwa kwa kurembua rembua, we need a Benevolent dictator, hizo 4R zake hazina uhalisia kwenye nchi ya dunia ya 3
Si nilisema JPm hatoshi?subirini sasa akili ziwasogee.mnadhani mko salama wakati ni swala la muda tu
 
Umezunguuka sana kumbe lengo lako ni kumtaja mungu wako aliyekufa 17,march!
 
Mada umeisoma? Mwanzo wa ngoma ni lele. Unajua hili wakifanikiwa wataishia wapi?

View attachment 2935104

Kama magari ya miaka 1950s yanatembea America sisi nani?

Ubora wa gari ni namba ya usajili?
Gari ili ipate leseni ya Latra ni lazima iwe na VIR (Vehicle inspection report) , so licha ya namba lakini zinakaguliwa pia.

Mbona TRA wanakataa gari za zaidi ya 0 nyuma kuingia nchini else ulipie uchakavu wa gari husika?

Latra wameset standards kwa maana kubwa , zije hizo za DTA kuja mbele lakini pia Ukaguzi unafanywa na Mamlaka husika ya ùkaguzi (Trqffic) kwa ajili ya kuangalia road worthiness.

Mwenge stend hayatakiwi magari makuukuu kwa sasa, acheni siasa
 
1. Standards kama ni za kijinga au za kibaguzi kuzikataa ni wajibu siyo siasa; labda kama wao wana agenda ya siasa kinyemela.

2. Kwamba tokea mamlaka ya ukaguzi, road worthiness gari limefuzu.

3. #2 hapo ila limekwama Kwa sababu namba siyo D au E?

4. #3 hapo, kwani zinazobeba watu ni namba au gari?

5. Mambo ya kibaguzi au kijinga si mpeleke mashambani mwenu huko.

6. Ngoja tuone; Mama achague kusuka au kunyoa; Ubabaishaji kama huu Kwa dhamana yetu haukubaliki!
 
Ugumu wa nchi hii tunauendekeza wenyewe kwa kuyaona na bado tukaendelea kujidanganya kuwa hayatuhusu. Hadi pale yatakapotukuta malangoni.
Sijaona tamko la LATRA kama unalo please share ili niweze kutoa maoni yangu kwa usahihi
 
Sijaona tamko la LATRA kama unalo please share ili niweze kutoa maoni yangu kwa usahihi

1. Mkuu lisenwalo lipo kama halipo laja.

2. Kimsingi yapo mawili yanayoongelewa nao hawajakanusha:

a) kuuingia city center liwe DZA kwenda mbele.
b) kuingia Mwenge Stendi, kwa mujibu wa mheshimiwa Leak (bila shaka mwenzao huyo) ni DTX kwa kwenda mbele.

3. Angalia nukuu hizi:

a) Daladala rasmi kurudi upya katikati ya Jiji la Dar-es-salaam mara baada ya mradi wa mwendokasi kushindwa kutoa huduma ipasavyo

IMG_20240315_132515.jpg

b)
IMG_20240315_131417.jpg

Siyo Bure!
 
Back
Top Bottom