Kauli za Maalim Seif zazua jambo Zanzibar

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Akizungumza na waandishi wa Habari juzi, Maalim Seif alifichua njama alizoziita ovu dhidi ya chama chake zilizoandaliwa na msururu wa viongozi wa CCM. Katika tuhuma hizo alifika mbali kwa kumtaja Katibu Mkuu wa CCM ndugu Bashiru kuhusika kwenye mikakati hiyo baadhi ya shutuma ni hizi.

i. Ndugu Bashiru kuiagiza SMZ kupeleka mswaada wa Dharura ili kuwazuiya wagombea waliohamia kwenye vyama chini ya miaka mitatu wasiwe na sifa za kugombea tuhuma hizi zikihusishwa kuwalenga wanachama wa ACT waliohamia kutoka CUF.

ii. CCM kushirikiana na CUF Lipumba kuleta vurumai Zanzibar kwa kisingizio cha kutwaa mali za CUF zilizoporwa ingawa kuna kesi mahakamani

iii. Njama za kuleta vurumai hio lengo ni kuwakamata viongozi wa ACT ili kuwafungulia kesi na kuwaweka ndani.

Mara baada ya kauli hizo Maalim Seif alifika mbali zaidi kwa kuwataka wanachama wao nchi nzima hasa Zanzibar kulinda mali zao na kuwa tayari kwa lolote.

KINACHOENDELEA.
Siku zote kwa siasa za Zanzibar Maalim Seif akitia neno hubadili mwelekeo wa mambo kwa haraka.

Kwanza ziara ya Dr Bashiru na kilichokusudiwa kinaonekana kupwaya baada ya kauli za Maalim Seif.

Kinachoendelea ni tahadhari zaidi, CCM kupitia jumuiya zake wanatoa matamko ya Kulaani yaani ziara imefunikwa na kauli za Maalim Seif.

Mipango ovu iliyokusudiwa kufanywa na CUF kwa kutumia kivuli cha Ziara ya Dr Bashiru imevurugika baada ya kukutana na zahma ya wana ACT huko Pemba.

Vyombo vya Ulinzi vinalazimika kuwa na TAHADHARI ZAIDI.

MWELEKEO

Inaonekana CCM inatafuta njia ya kupita katikati baina ya CUF yaLipumba ambayo haina wafuasi tena Zanzibar dhidi ya ACT yenye nguvu. Kauli za Dr Bashiru kuwa sasa CCM itachukuwa majimbo Pemba ni ushahidi wa njama hizo. Kiukweli CCM Pemba haina chake zaidi ya Udola tu.

Nadhani Mpango mkakati ni kutumiwa CUF walau kwa kivuli cha jina na wala sio uhalisia

Jee CCM na CUF zitafanikiwa?

Hili litapata jibu kwa MUJIBU WA WAKATI.
CCM ijiandae kuivuruga Zanzibar. Watu kule wamejeruhiwa sana na wana mafundo kwenye nafsi zao. Ushiriki wa akina Halifa na wenzao hautakuwa na afya yoyote Pemba na Unguja yake. Huu mwega ni wa makaratasi. CCM haijapata mwega mzuri.

Kama ni kutumia Dola sawa hayo yalishazoeleka lkn Dola ilitumika mpaka ikaonekana umuhjmu wa Maridhiano itakuwa ajabu kurudisha yaliyopita ingawa hayashangazi.

Kiufupi kauli za Maalim Seif zimeamsha siasa Zanzibar, zimetibua mipango ovu, zimefichua nia mbaya na kuibua mikakati iliyofichwa.

Kitendo cha Katibu Mkuu Khalifa wa CUF kukiri kwamba wana nia ya kutwaa mali zao hadharani na kukiri juzi walifanya kile alichokiita " Road show" ya namna watakavyozitwaa mali za CUF ndani ya ziara ya Ndugu Bashiru na kushindwa kufikia azma baada ya kukutana na zahma ya ACT sio tu nia ovu lakini kunaifedhehesha CCM kama itakuwa ilitowa baraka kutumiwa ziara hiyo kama kinga.

Ukweli unabaki pale pale Maalim Seif ni jabali la siasa za Zanzibar kiasi akitia neno tu kunatikisika kila mahali.

Wafuatiliaji wetu wako makini kutupasha kinachoendelea maana kwa sasa kuna sindikizo kutoka kwa jumuiya za CCM kutaka Maalim Seif achukuliwe hatua zinazoitwa za Uchochezi.

Wakati hayo yakiendelea kuna umakini mkubwa ili kuzuiya zahma yoyote ambayo inaweza kutokea

Kishada
 
Haiwezekani uhamie mwaka Huu halafu ugombee uongozi? Haiwezekani

Km unatumika na Mabeberu tutajuaje

Wapewe kipindi cha uangalizi kwanza
 
Maalimu Seif asijifiche kwenye kichaka cha CCM kutafuta huruma kwa watu. ACT ya Maalimu Zanzibar inajua uovu ilioufanya wakati wa kujitoa CUF.

Bahati nzuri CUF waliweka wazi msimamo wao juu ya mali zao zilizoporwa na ACT. Hawautaka kufanya fujo ya kuzirejesha ali waliamua kutumia njia ya amani kwenda mahakamani. Na uamuzi wa mahakama ukitoka hauna simile na Serikali kutumia vyombo vyake vya ulinzi itasimamia maamuzi ya mahakama ndio sheria inavyotaka.

Kuropoka kwa Maalimu ni dalili ya kuona kile kinachokuja mbele yake, magari, ofisi na samani zilizonunuliwa kwa ruzuku ya CUF haziwezi kuhamishwa kwa wanachama kuhama.

Aidha sheria ya uchaguzi wa JMT ni moja, inayotumika T/Bara ndiyo itumikayo T/visiwani kwa Urais na Ubunge. Kama sheria hiyo imeshafanyiwa marekebisho na bunge na kupitishwa ni lazima kwa upande wa visiwani iidhinishwe na baraza la wawakilishi. Hilo Maalimu hawezi kulizuia.
 
Maalim anajua ameyakoroga anatafuta wa kumlaumu

Wale waliokua wakihama kutoka CHADEMA kwenda Ccm walienda kugombea nafasi za Uongozi baada ya muda gani?
Ndio maana baada ya hapo sheria imetungwa na kupitishwa bungeni, Zitto akiwa mshiriki asijifanye hajui.
 
Akizungumza na waandishi wa Habari juzi, Maalim Seif alifichua njama alizoziita ovu dhidi ya chama chake zilizoandaliwa na msururu wa viongozi wa CCM. Katika tuhuma hizo alifika mbali kwa kumtaja Katibu Mkuu wa CCM ndugu Bashiru kuhusika kwenye mikakati hiyo baadhi ya shutuma ni hizi.

i. Ndugu Bashiru kuiagiza SMZ kupeleka mswaada wa Dharura ili kuwazuiya wagombea waliohamia kwenye vyama chini ya miaka mitatu wasiwe na sifa za kugombea tuhuma hizi zikihusishwa kuwalenga wanachama wa ACT waliohamia kutoka CUF.

ii. CCM kushirikiana na CUF Lipumba kuleta vurumai Zanzibar kwa kisingizio cha kutwaa mali za CUF zilizoporwa ingawa kuna kesi mahakamani

iii. Njama za kuleta vurumai hio lengo ni kuwakamata viongozi wa ACT ili kuwafungulia kesi na kuwaweka ndani.

Mara baada ya kauli hizo Maalim Seif alifika mbali zaidi kwa kuwataka wanachama wao nchi nzima hasa Zanzibar kulinda mali zao na kuwa tayari kwa lolote.

KINACHOENDELEA.
Siku zote kwa siasa za Zanzibar Maalim Seif akitia neno hubadili mwelekeo wa mambo kwa haraka.

Kwanza ziara ya Dr Bashiru na kilichokusudiwa kinaonekana kupwaya baada ya kauli za Maalim Seif.

Kinachoendelea ni tahadhari zaidi, CCM kupitia jumuiya zake wanatoa matamko ya Kulaani yaani ziara imefunikwa na kauli za Maalim Seif.

Mipango ovu iliyokusudiwa kufanywa na CUF kwa kutumia kivuli cha Ziara ya Dr Bashiru imevurugika baada ya kukutana na zahma ya wana ACT huko Pemba.

Vyombo vya Ulinzi vinalazimika kuwa na TAHADHARI ZAIDI.

MWELEKEO

Inaonekana CCM inatafuta njia ya kupita katikati baina ya CUF yaLipumba ambayo haina wafuasi tena Zanzibar dhidi ya ACT yenye nguvu. Kauli za Dr Bashiru kuwa sasa CCM itachukuwa majimbo Pemba ni ushahidi wa njama hizo. Kiukweli CCM Pemba haina chake zaidi ya Udola tu.

Nadhani Mpango mkakati ni kutumiwa CUF walau kwa kivuli cha jina na wala sio uhalisia

Jee CCM na CUF zitafanikiwa?

Hili litapata jibu kwa MUJIBU WA WAKATI.
CCM ijiandae kuivuruga Zanzibar. Watu kule wamejeruhiwa sana na wana mafundo kwenye nafsi zao. Ushiriki wa akina Halifa na wenzao hautakuwa na afya yoyote Pemba na Unguja yake. Huu mwega ni wa makaratasi. CCM haijapata mwega mzuri.

Kama ni kutumia Dola sawa hayo yalishazoeleka lkn Dola ilitumika mpaka ikaonekana umuhjmu wa Maridhiano itakuwa ajabu kurudisha yaliyopita ingawa hayashangazi.

Kiufupi kauli za Maalim Seif zimeamsha siasa Zanzibar, zimetibua mipango ovu, zimefichua nia mbaya na kuibua mikakati iliyofichwa.

Kitendo cha Katibu Mkuu Khalifa wa CUF kukiri kwamba wana nia ya kutwaa mali zao hadharani na kukiri juzi walifanya kile alichokiita " Road show" ya namna watakavyozitwaa mali za CUF ndani ya ziara ya Ndugu Bashiru na kushindwa kufikia azma baada ya kukutana na zahma ya ACT sio tu nia ovu lakini kunaifedhehesha CCM kama itakuwa ilitowa baraka kutumiwa ziara hiyo kama kinga.

Ukweli unabaki pale pale Maalim Seif ni jabali la siasa za Zanzibar kiasi akitia neno tu kunatikisika kila mahali.

Wafuatiliaji wetu wako makini kutupasha kinachoendelea maana kwa sasa kuna sindikizo kutoka kwa jumuiya za CCM kutaka Maalim Seif achukuliwe hatua zinazoitwa za Uchochezi.

Wakati hayo yakiendelea kuna umakini mkubwa ili kuzuiya zahma yoyote ambayo inaweza kutokea

Kishada
Mimi naamini Maalim Seif ni Rais wa Zanzibar
 
Maalimu Seif asijifiche kwenye kichaka cha CCM kutafuta huruma kwa watu. ACT ya Maalimu Zanzibar inajua uovu ilioufanya wakati wa kujitoa CUF.

Bahati nzuri CUF waliweka wazi msimamo wao juu ya mali zao zilizoporwa na ACT. Hawautaka kufanya fujo ya kuzirejesha ali waliamua kutumia njia ya amani kwenda mahakamani. Na uamuzi wa mahakama ukitoka hauna simile na Serikali kutumia vyombo vyake vya ulinzi itasimamia maamuzi ya mahakama ndio sheria inavyotaka.

Kuropoka kwa Maalimu ni dalili ya kuona kile kinachokuja mbele yake, magari, ofisi na samani zilizonunuliwa kwa ruzuku ya CUF haziwezi kuhamishwa kwa wanachama kuhama.

Aidha sheria ya uchaguzi wa JMT ni moja, inayotumika T/Bara ndiyo itumikayo T/visiwani kwa Urais na Ubunge. Kama sheria hiyo imeshafanyiwa marekebisho na bunge na kupitishwa ni lazima kwa upande wa visiwani iidhinishwe na baraza la wawakilishi. Hilo Maalimu hawezi kulizuia.

Kwanza nimefurahi kwa kujikita kwenye mada.

Kinachoshangaza kesi iko mahakamani maamuzi bado hao jamaa wanakwenda kuvamia ofisi za watu kwa kisingizio cha kutwaa mali ambazo hawana ushahidi nazo. Hapa kunazungumzwa ofisi ambazo nyingi ni mali za watu za kujitolea na hakukuwa na mkataba wowote. Kama kuna magari ya CUF yatathibitishwa mahakamani na sio uvamizi.

Pili Uwakilishi na nafasi ya Urais wa Zanzibar sio ya muungano. Ishu ya Ubunge achana nayo hapa. Lakini kwa faida ya wengi jee Sheria ya Ubunge nasemaje linapokuja suala la kuhama chama ? tusadie hapa kwa faida ya wengi.

Tatu ina maana umeshajuwa kuwa mahakama itawapa ushindi CUF ? kuhusu mali zao kabla kesi haijafika mwisho. Ninachojuwa CUF ilipata msaada wa ofisi na magari ya watu binafsi kutokana na mapenzi yao, walipohama walihama na mapenzi yao. Yale yatakayothibitishwa ni ya CUF watapewa hakuna haja ya vurugu mzee.

Unazungumziaje huo ushirika wa CUF Lipumba kutumika na CCM?
 
Alipotimuliwa CUF na wanachama alidhani Cuf itayumba

Huko alipoenda amebaki peke yake

Anatamani arudi Cuf ila milango imefungwa
Twambie kayakoroga vipi ? ili tufaidike na maelezo yako.
 
Back
Top Bottom