Akizungumza na waandishi wa Habari juzi, Maalim Seif alifichua njama alizoziita ovu dhidi ya chama chake zilizoandaliwa na msururu wa viongozi wa CCM. Katika tuhuma hizo alifika mbali kwa kumtaja Katibu Mkuu wa CCM ndugu Bashiru kuhusika kwenye mikakati hiyo baadhi ya shutuma ni hizi.
i. Ndugu Bashiru kuiagiza SMZ kupeleka mswaada wa Dharura ili kuwazuiya wagombea waliohamia kwenye vyama chini ya miaka mitatu wasiwe na sifa za kugombea tuhuma hizi zikihusishwa kuwalenga wanachama wa ACT waliohamia kutoka CUF.
ii. CCM kushirikiana na CUF Lipumba kuleta vurumai Zanzibar kwa kisingizio cha kutwaa mali za CUF zilizoporwa ingawa kuna kesi mahakamani
iii. Njama za kuleta vurumai hio lengo ni kuwakamata viongozi wa ACT ili kuwafungulia kesi na kuwaweka ndani.
Mara baada ya kauli hizo Maalim Seif alifika mbali zaidi kwa kuwataka wanachama wao nchi nzima hasa Zanzibar kulinda mali zao na kuwa tayari kwa lolote.
KINACHOENDELEA.
Siku zote kwa siasa za Zanzibar Maalim Seif akitia neno hubadili mwelekeo wa mambo kwa haraka.
Kwanza ziara ya Dr Bashiru na kilichokusudiwa kinaonekana kupwaya baada ya kauli za Maalim Seif.
Kinachoendelea ni tahadhari zaidi, CCM kupitia jumuiya zake wanatoa matamko ya Kulaani yaani ziara imefunikwa na kauli za Maalim Seif.
Mipango ovu iliyokusudiwa kufanywa na CUF kwa kutumia kivuli cha Ziara ya Dr Bashiru imevurugika baada ya kukutana na zahma ya wana ACT huko Pemba.
Vyombo vya Ulinzi vinalazimika kuwa na TAHADHARI ZAIDI.
MWELEKEO
Inaonekana CCM inatafuta njia ya kupita katikati baina ya CUF yaLipumba ambayo haina wafuasi tena Zanzibar dhidi ya ACT yenye nguvu. Kauli za Dr Bashiru kuwa sasa CCM itachukuwa majimbo Pemba ni ushahidi wa njama hizo. Kiukweli CCM Pemba haina chake zaidi ya Udola tu.
Nadhani Mpango mkakati ni kutumiwa CUF walau kwa kivuli cha jina na wala sio uhalisia
Jee CCM na CUF zitafanikiwa?
Hili litapata jibu kwa MUJIBU WA WAKATI.
CCM ijiandae kuivuruga Zanzibar. Watu kule wamejeruhiwa sana na wana mafundo kwenye nafsi zao. Ushiriki wa akina Halifa na wenzao hautakuwa na afya yoyote Pemba na Unguja yake. Huu mwega ni wa makaratasi. CCM haijapata mwega mzuri.
Kama ni kutumia Dola sawa hayo yalishazoeleka lkn Dola ilitumika mpaka ikaonekana umuhjmu wa Maridhiano itakuwa ajabu kurudisha yaliyopita ingawa hayashangazi.
Kiufupi kauli za Maalim Seif zimeamsha siasa Zanzibar, zimetibua mipango ovu, zimefichua nia mbaya na kuibua mikakati iliyofichwa.
Kitendo cha Katibu Mkuu Khalifa wa CUF kukiri kwamba wana nia ya kutwaa mali zao hadharani na kukiri juzi walifanya kile alichokiita " Road show" ya namna watakavyozitwaa mali za CUF ndani ya ziara ya Ndugu Bashiru na kushindwa kufikia azma baada ya kukutana na zahma ya ACT sio tu nia ovu lakini kunaifedhehesha CCM kama itakuwa ilitowa baraka kutumiwa ziara hiyo kama kinga.
Ukweli unabaki pale pale Maalim Seif ni jabali la siasa za Zanzibar kiasi akitia neno tu kunatikisika kila mahali.
Wafuatiliaji wetu wako makini kutupasha kinachoendelea maana kwa sasa kuna sindikizo kutoka kwa jumuiya za CCM kutaka Maalim Seif achukuliwe hatua zinazoitwa za Uchochezi.
Wakati hayo yakiendelea kuna umakini mkubwa ili kuzuiya zahma yoyote ambayo inaweza kutokea
Kishada