Haiwezekani uhamie mwaka Huu halafu ugombee uongozi? Haiwezekani
Km unatumika na Mabeberu tutajuaje
Wapewe kipindi cha uangalizi kwanza
Hahaha kaka unajua maana HIZBU??
Haiwezekani uhamie mwaka Huu halafu ugombee uongozi? Haiwezekani
Km unatumika na Mabeberu tutajuaje
Wapewe kipindi cha uangalizi kwanza
Soma tena mada unufaike.Alipotimuliwa CUF na wanachama alidhani Cuf itayumba
Huko alipoenda amebaki peke yake
Anatamani arudi Cuf ila milango imefungwa
Soma tena mada unufaike.
Yaani hao viongozi wa CUF unaosema Maalim anatafuta kurudi milangoi imefungwa, ndio wanatumia kivuli cha Dr bashiru kujipendekleza kwa wapemba. Walikusudia kiujificha ili wakidhibitiwa CCM iseme Imevamiwa na ACT. Bila kujiegemeza na CCM, CUF lipumba haiwezi kusogelea Pemba. Trust me.
Mkuu Kishada! Kwani hii nayo inahitaji jibu la maandishi? Nilisema humu JF kwamba upinzani Zanzibar haujawahi kutetereka si kwa njama wala hila; na hii itaendelea kwa miongo mingi ijayo. Wapinzani wa Zanzibar wanaangalia maslahi yanchi kwanza na sio kitu kingine chochote, na hili ndilo linalowafanya kuwa na nguvu ya ajabu!Jee CCM na CUF zitafanikiwa?
Mkuu unazungumzia uchaguzi wa Muungano au wa Zanzibar? Kwa ule wa Zanzibar hayo unayoyasema sivyo yalivyo. Jaribu sana kukumbuka unapozungumzia mambo ya Zanzibar. Zanzibar ina taratibu zake inapokuja kwenye mambo ambayo sio ya Muungano.Aidha sheria ya uchaguzi wa JMT ni moja, inayotumika T/Bara ndiyo itumikayo T/visiwani kwa Urais na Ubunge. Kama sheria hiyo imeshafanyiwa marekebisho na bunge na kupitishwa ni lazima kwa upande wa visiwani iidhinishwe na baraza la wawakilishi.
Maalim seif, Freeman Mbowe na Proffessor Lipumba ndio wanaokwamisha juhudi za kuitoa CCM madarkani!Akizungumza na waandishi wa Habari juzi, Maalim Seif alifichua njama alizoziita ovu dhidi ya chama chake zilizoandaliwa na msururu wa viongozi wa CCM. Katika tuhuma hizo alifika mbali kwa kumtaja Katibu Mkuu wa CCM ndugu Bashiru kuhusika kwenye mikakati hiyo baadhi ya shutuma ni hizi.
i. Ndugu Bashiru kuiagiza SMZ kupeleka mswaada wa Dharura ili kuwazuiya wagombea waliohamia kwenye vyama chini ya miaka mitatu wasiwe na sifa za kugombea tuhuma hizi zikihusishwa kuwalenga wanachama wa ACT waliohamia kutoka CUF.
ii. CCM kushirikiana na CUF Lipumba kuleta vurumai Zanzibar kwa kisingizio cha kutwaa mali za CUF zilizoporwa ingawa kuna kesi mahakamani
iii. Njama za kuleta vurumai hio lengo ni kuwakamata viongozi wa ACT ili kuwafungulia kesi na kuwaweka ndani.
Mara baada ya kauli hizo Maalim Seif alifika mbali zaidi kwa kuwataka wanachama wao nchi nzima hasa Zanzibar kulinda mali zao na kuwa tayari kwa lolote.
KINACHOENDELEA.
Siku zote kwa siasa za Zanzibar Maalim Seif akitia neno hubadili mwelekeo wa mambo kwa haraka.
Kwanza ziara ya Dr Bashiru na kilichokusudiwa kinaonekana kupwaya baada ya kauli za Maalim Seif.
Kinachoendelea ni tahadhari zaidi, CCM kupitia jumuiya zake wanatoa matamko ya Kulaani yaani ziara imefunikwa na kauli za Maalim Seif.
Mipango ovu iliyokusudiwa kufanywa na CUF kwa kutumia kivuli cha Ziara ya Dr Bashiru imevurugika baada ya kukutana na zahma ya wana ACT huko Pemba.
Vyombo vya Ulinzi vinalazimika kuwa na TAHADHARI ZAIDI.
MWELEKEO
Inaonekana CCM inatafuta njia ya kupita katikati baina ya CUF yaLipumba ambayo haina wafuasi tena Zanzibar dhidi ya ACT yenye nguvu. Kauli za Dr Bashiru kuwa sasa CCM itachukuwa majimbo Pemba ni ushahidi wa njama hizo. Kiukweli CCM Pemba haina chake zaidi ya Udola tu.
Nadhani Mpango mkakati ni kutumiwa CUF walau kwa kivuli cha jina na wala sio uhalisia
Jee CCM na CUF zitafanikiwa?
Hili litapata jibu kwa MUJIBU WA WAKATI.
CCM ijiandae kuivuruga Zanzibar. Watu kule wamejeruhiwa sana na wana mafundo kwenye nafsi zao. Ushiriki wa akina Halifa na wenzao hautakuwa na afya yoyote Pemba na Unguja yake. Huu mwega ni wa makaratasi. CCM haijapata mwega mzuri.
Kama ni kutumia Dola sawa hayo yalishazoeleka lkn Dola ilitumika mpaka ikaonekana umuhjmu wa Maridhiano itakuwa ajabu kurudisha yaliyopita ingawa hayashangazi.
Kiufupi kauli za Maalim Seif zimeamsha siasa Zanzibar, zimetibua mipango ovu, zimefichua nia mbaya na kuibua mikakati iliyofichwa.
Kitendo cha Katibu Mkuu Khalifa wa CUF kukiri kwamba wana nia ya kutwaa mali zao hadharani na kukiri juzi walifanya kile alichokiita " Road show" ya namna watakavyozitwaa mali za CUF ndani ya ziara ya Ndugu Bashiru na kushindwa kufikia azma baada ya kukutana na zahma ya ACT sio tu nia ovu lakini kunaifedhehesha CCM kama itakuwa ilitowa baraka kutumiwa ziara hiyo kama kinga.
Ukweli unabaki pale pale Maalim Seif ni jabali la siasa za Zanzibar kiasi akitia neno tu kunatikisika kila mahali.
Wafuatiliaji wetu wako makini kutupasha kinachoendelea maana kwa sasa kuna sindikizo kutoka kwa jumuiya za CCM kutaka Maalim Seif achukuliwe hatua zinazoitwa za Uchochezi.
Wakati hayo yakiendelea kuna umakini mkubwa ili kuzuiya zahma yoyote ambayo inaweza kutokea
Kishada
Mimi na wewe nani haijui Pemba, Au mkuu ulimkusudia mwengine?Wewe hujui pemba tulia
Wacha uwbege wako.Haiwezekani uhamie mwaka Huu halafu ugombee uongozi? Haiwezekani
Km unatumika na Mabeberu tutajuaje
Wapewe kipindi cha uangalizi kwanza
Wankupenda wewe na má. Má yakoSema anapendwa na ma hizbu
Wazanzibar Wengi hawamkubali
MALI KAMA ZIPI? CCM BANA MNAPENDA KUPITIA MLANGO WA NYUMA KUHALALISHA MAAOVU YENU.Maalimu Seif asijifiche kwenye kichaka cha CCM kutafuta huruma kwa watu. ACT ya Maalimu Zanzibar inajua uovu ilioufanya wakati wa kujitoa CUF.
Bahati nzuri CUF waliweka wazi msimamo wao juu ya mali zao zilizoporwa na ACT. Hawautaka kufanya fujo ya kuzirejesha ali waliamua kutumia njia ya amani kwenda mahakamani. Na uamuzi wa mahakama ukitoka hauna simile na Serikali kutumia vyombo vyake vya ulinzi itasimamia maamuzi ya mahakama ndio sheria inavyotaka.
Kuropoka kwa Maalimu ni dalili ya kuona kile kinachokuja mbele yake, magari, ofisi na samani zilizonunuliwa kwa ruzuku ya CUF haziwezi kuhamishwa kwa wanachama kuhama.
Aidha sheria ya uchaguzi wa JMT ni moja, inayotumika T/Bara ndiyo itumikayo T/visiwani kwa Urais na Ubunge. Kama sheria hiyo imeshafanyiwa marekebisho na bunge na kupitishwa ni lazima kwa upande wa visiwani iidhinishwe na baraza la wawakilishi. Hilo Maalimu hawezi kulizuia.
Ndio maana nimeeleza, kwa suala la uchaguzi wa Wabunge (sio wawakilishi) unasimamiwa kwa sheria ya NEC, lakini sheria ya vyama vya siasa na kanuni zake ni moja bara na visiwani .Mkuu unazungumzia uchaguzi wa Muungano au wa Zanzibar? Kwa ule wa Zanzibar hayo unayoyasema sivyo yalivyo. Jaribu sana kukumbuka unapozungumzia mambo ya Zanzibar. Zanzibar ina taratibu zake inapokuja kwenye mambo ambayo sio ya Muungano.
Mimi na wewe nani haijui Pemba, Au mkuu ulimkusudia mwengine?
Suburi mahakama ya ZANZIBAR itatoa jibu.MALI KAMA ZIPI? CCM BANA MNAPENDA KUPITIA MLANGO WA NYUMA KUHALALISHA MAAOVU YENU.
Wewe ndio huijui pemba na nyamaza sana. Muulize huyo kibaraka wenu katibu WA cuf akueleze baada ya kukubali kuwa na lipumba yaliotakakumkuta huko mjini kwao.Wewe hujui pemba tulia
Mali nyingi zilizokuwa zikitumika ni za watu binafsi walipoondoka cuf nazo walichukuwa kilicho chao watachukua halafu waone kitachowakuta hawo cufccm.Suburi mahakama ya ZANZIBAR itatoa jibu.
Kama walivyopewa wachimia matumbo kina Waitara na wenzweHaiwezekani uhamie mwaka Huu halafu ugombee uongozi? Haiwezekani
Km unatumika na Mabeberu tutajuaje
Wapewe kipindi cha uangalizi kwanza